Jukwaa La Kiswahili

Karibu kwenye jukwaa letu la Kiswahili

Mafumbo

Posted by robert kibui - Nov 27, 2019


Naomba jibu la hili fumbo. Sio kawaida yangu nitembee pekee yangu, napokuwa na wenzangu wengi huchanganyikiwa, kukosekana kwangu kwenye shughuli mingi ni hatari sana, kuwepo kwangu mara nyingi ni mambo yote.

Funzo la saa

Posted by Kennedy madaga - Oct 09, 2019


Katika somo la kiswahili,mafunzo ya saa hukanganya sana,je ni sahihi kusema saa nane au saa mbili unaporejelea 2.00?

UHAKIKI WA KIMAUDHUI NA KIFANI WA KIDAGAA KIMEMWOZEA

Posted by MARTIN KIPRONO CHERUIYOT - Nov 01, 2017


UHAKIKI WA KIMAUDHUI NA KIFANI WA KIDAGAA KIMEMWOZEA NA MARTIN KIPRONO CHERUIYOT Tasnifu hii imetolewa ili kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Nairobi Novemba 2017 i UNGAMO Tasnifu hii ni kazi yangu mwenyewe na haijatolewa kwa mahitaji ya shahada katika chuo kikuu kingine chochote. ____________________________ ___________________ RONO PAULINE Tarehe (Mtahiniwa) Tasnifu hii imetolewa kutahiniwa kwa idhini yetu tukiwa wasimamizi wa kazi hii tulioteuliwa na Chuo Kikuu cha Nairobi. ____________________________ ___________________ Dkt. EVANS M. MBUTHIA Tarehe ____________________________ ___________________ Dkt. FRANCIS MWANGANGI MUSYOKA Tarehe ii TABARUKU Tasnifu hii naitabarukia mamangu Julia Mbugua kwa kunilea na kunisomesha. Mungu azidi kumuongezea miaka mingi duniani. iii SHUKRANI Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa uwezo na subira ya kung’ang’ana na masomo haya hadi mwisho. Shukrani za dhati ziwaendee wasimamizi wangu Dkt. Mbuthia na Dkt. Musyoka kwa mawaidha yao mufti ambayo yalichangia katika ufanisi wa kazi hii. Ningependa pia kumshukuru mume wangu Vincent Rono na wanangu Nancy, Edwin, Sammy na mjukuu wangu Lionell kwa kunivumilia nilipolazimika kujitosa kwenye masomo haya. Shukrani zangu pia ziwaendee wanafunzi wenzangu kama vile Rael Onchangu, Kenguru na Chacha kwa kunihimiza hadi nikafikisha safari hii kwenye kikomo. iv MUHTASARI Tasnifu hii ilishughulikia uhakiki wa kifani na kimaudhui wa Kidagaa Kimemwozea ya Ken Walibora(2012). Tuliangalia maudhui na tulinuia kuonyesha mbinu zilizotumiwa katika kuwaumba wahusika na jinsi wahusika vijana walivyopigania kuondoa ukoloni mambo leo katika nchi ya Tomoko. Pamoja na hayo tulishughulikia nadharia tete ya uhakiki ambayo ni mhimili wa utafiti huu. Sababu za kuchagua mada pia zimeelezwa. Kazi yetu iliangazia maudhui, fani na wahusika. Kwa vile kuna njia nyingi za kuwasiri wahusika sisi tumejibana kwa wahusika wakuu, wasaidizi na wajenzi. Misingi ya nadharia za uhalisia wa kijamaa na umuundo imezingatiwa katika uhakiki wetu. Nadharia ya uhalisia wa kijamaa ni kwa mujibu wa wanafalsafa kama vile George Lukacs, Marxim Gorky, Zandnov na wengineo. Nadharia ya umuundo ni kwa mujibu wa Ferdinand De Saussure. Nadharia hii kuchunguza vipengele vya kazi ya sanaa, jinsi vinavyohusiana hadi kuikamilisha kazi hiyo. Huangalia namna sehemu mbalimbali za kazi ya sanaa zimefungamana. Mbinu za utafiti tulizotumia ni za maktabani ambapo tulirejelea makala mbalimbali yakiwemo majarida, tasnifu na vitabu kadha wa kadha. v YALIYOMO UKURASA UNGAMO ..................................................................................................................................................... i TABARUKU ................................................................................................................................................ ii SHUKRANI ................................................................................................................................................. iii MUHTASARI .............................................................................................................................................. iv SURA YA KWANZA ................................................................................................................................. 1 1.0 UTANGULIZI ........................................................................................................................................ 1 1.1 TATIZO LA UTAFITI ........................................................................................................................... 2 1.2 MADHUMUNI YA UTAFITI................................................................................................................ 3 1.3 MASWALI YA UTAFITI ...................................................................................................................... 3 1.4 NADHARIA TETE .............................................................................. Error! Bookmark not defined. 1.5 SABABU ZA KUCHAGUA MADA ..................................................................................................... 3 1.6 UPEO NA MIPAKA ............................................................................................................................... 4 1.7 MSINGI WA KINADHARIA ................................................................................................................ 8 1.7.1 UHALISIA WA KIJAMAA ................................................................................................................ 8 1.7.1.1 MIHIMILI YA UHALISIA WA KIJAMAA ............................................................................... 8 1.7.2 UMUUNDO ..................................................................................................................................... 9 1.8 MBINU ZA UTAFITI ......................................................................................................................... 11 SURA YA PILI: MAUDHUI KATIKA KIDAGAA KIMEMWOZEA ............................................... 12 2.0 UTANGULIZI ...................................................................................................................................... 12 2.1 DHANA YA MAUDHUI ..................................................................................................................... 12 2.1.1 UOZO WA VIONGOZI ................................................................................................................ 14 2.1.2 UTABAKA .................................................................................................................................... 15 2.1.3 UMUHIMU WA ELIMU .............................................................................................................. 16 vi 2.1.4 ULITIMA ....................................................................................................................................... 17 2.1.5 MALEZI ........................................................................................................................................ 18 2.1.6 NAFASI YA MWANAMKE....................................................................................................... 19 2.1.7 UASI .............................................................................................................................................. 20 2.1.8 MADHARA YA ULEVI ............................................................................................................... 21 2.1.9 UJAMAA ....................................................................................................................................... 22 2.2.0 TAMAA ......................................................................................................................................... 22 2.2.1 UTU .............................................................................................................................................. 23 2.2.2 UKOSEFU WA HAKI .................................................................................................................. 24 2.2.3 USHIRIKIANO ............................................................................................................................. 25 2.2.4 UMUHIMU WA MABADILIKO ................................................................................................. 26 2.3 KIMALIZIO ......................................................................................................................................... 26 SURA YA TATU: SWALA LA UHUSIKA NA WAHUSIKA KATIKA RIWAYA. ......................... 28 3.0 UTANGULIZI ...................................................................................................................................... 28 3.1 UHUSIKA............................................................................................................................................. 28 3.2 UANISHAJI WA WAHUSIKA ........................................................................................................... 30 3.3 NJIA NYINGINE ZA KUWASAWIRI WAHUSIKA ......................................................................... 32 3.3.1 MHUSIKA WA JADI ................................................................................................................... 32 3.3.2 MHUSIKA WA KIMUUNDO NA KIMTINDO ......................................................................... 33 3.3.3 MHUSIKA WA KIHALISI ........................................................................................................... 33 3.3.4 MHUSIKA WA KISASA .............................................................................................................. 34 3.4 MBINU ZA USAWIRI WA WAHUSIKA. ......................................................................................... 35 3.5 KIMALIZIO ......................................................................................................................................... 39 vii SURA YA NNE: WAHUSIKA KATIKA KIDAGAA KIMEMWOZEA ............................................ 40 4.1 WAHUSIKA WAKUU ........................................................................................................................ 40 4.1.1 UTANGULIZI ............................................................................................................................... 40 4.1.2 MTEMI NASABA BORA. ............................................................................................................ 40 4.1.3 AMANI .......................................................................................................................................... 44 4.1.4 HITIMISHO ................................................................................................................................... 47 4.2 WAHUSIKA WASAIDIZI ................................................................................................................... 48 4.2 .1 UTANGULIZI .............................................................................................................................. 48 4.2.2 MWALIMU MAJISIFU MAJIMAREFU ..................................................................................... 48 4.2.3 IMANI............................................................................................................................................ 50 4.2.4MADHUBUTI ................................................................................................................................ 52 4.2.5MZEE MATUKO WEYE ............................................................................................................... 54 4.2.6 MASHAKA ................................................................................................................................... 56 4.2.7 DJ BOB .......................................................................................................................................... 56 4.2.8 BI ZUHURA .................................................................................................................................. 57 4.2.9BI DORA ........................................................................................................................................ 59 4.2.10 HITIMISHO ................................................................................................................................. 59 4.3 WAHUSIKA WAJENZI ...................................................................................................................... 60 4.3.1 UTANGULIZI ............................................................................................................................... 60 4.3.2 BEN BELLA .................................................................................................................................. 60 4.3.3 BWANA MAOZI .......................................................................................................................... 61 4.3.4. OSCAR KAMBONA (GADDAFI) .............................................................................................. 61 4.3.5 LOWELA ....................................................................................................................................... 62 viii 4.3.6 CHICHIRI HAMADI .................................................................................................................... 62 4.3.7 BI MAOZI ..................................................................................................................................... 63 4.3.8MWINYI HATIBU MUTEMBEZI ................................................................................................ 63 4.3.9MICHELLE .................................................................................................................................... 63 4.3.10 YUSUFU...................................................................................................................................... 64 4.3.11 FAO.............................................................................................................................................. 64 4.3.12 UHURU ....................................................................................................................................... 64 4.3.13 CHWECHWE MAKWECHE (HORSE POWER) ...................................................................... 65 4.3.14 BALOZI ....................................................................................................................................... 65 4.3.15MAMA IMANI ............................................................................................................................. 66 4.3.16 MAC ARTHUR KUTO ............................................................................................................... 66 4.3.17 KIMALIZIO............................................................................................................................... 66 SURA YA TANO:HITIMISHO NA MAPENDEKEZO ....................................................................... 67 5.0 UTANGULIZI ...................................................................................................................................... 67 5.1 MUHTASARI ...................................................................................................................................... 67 5.2 HITIMISHO ....................................................................................................................................... 68 5.3 MAPENDEKEZO .............................................................................................................................. 69 MAREJELEO ............................................................................................................................................. 71 1 SURA YA KWANZA 1.0 UTANGULIZI Tasnifu hii inashughulikia maudhui na fani katika Kidagaa Kimemwozea ya Ken Walibora (2012). Kwa mujibu wa Wamitila (2008:52) maudhui ni dhana pana inayoweza kuelezewa kwa jinsi mbili ambazo kimsingi zinahusiana. Kwanza, maudhui ni jumla ya masuala au mambo yanayoshughulikiwa katika kazi za kifasihi. Masuala haya hutokana na jinsi mtunzi au mwandishi anavyoikuza mada ambayo ni msingi wa utunzi wa kazi yake. Jinsi ya pili ni kutumia maudhui kukirejelea kiwango cha kimaana cha matini au kazi ya kifasihi. Maudhui hujumlisha vipengele vingine kadha kama vile dhamira, falsafa, itikadi na msimamo wa mwandishi pamoja an maadili na mafunzo yanayopatikana katika kazi ya fasihi. Dhamira na maudhui havitokezi tu katika kazi ya kifasihi bali ni zao la mahusiano na maingiliano ya vipengele na mbinu kadha katika kazi inayohusika. Kulingana na Wamitila (2008:524-527) uelewekaji wa dhamira kwa njia ya kikamilifu unategemea; maudhui na wahusika, sauti ya msimulizi, mandhari, msuko, mtazamo, mtindo, mwingiliano matini na mengineo. Katika Kidagaa Kimemwozea, maudhui mengi yameweza kujitokeza kama vile ufisadi, ukatili, ulevi, uasi, utabaka, ujamaa, ushirikiano, uzembe, uozo unaendelezwa na viongozi, tamaa, malezi, utu, umaskini na mengineo. Wahusika ni viumbe wanaopatikana katika hadithi yoyote ile. Viumbe hawa huwa sehemu ya kazi nzima. Wahusika ni ‘binadamu’ wanaopatikana katika kazi za kifasihi na ambao wana sifa za kimaadili, kitabia, kiitikadi, kifalsafa ambazo hutambulishwa na wanayoyasema na wanayoyatenda na pia kutokana na maelezo ya mwandishi (Wamitila 2002; 18) 2 1.1 TATIZO LA UTAFITI Bara la Afrika limekumbwa na matatizo mengi sana kutokana na athari za ukoloni mamboleo. Ni ukweli bayana ya kwamba uhuru wa bendera katika nchi nyingi haukuleta mabadiliko yaliyokusudiwa. Baadhi ya nchi zinaonekana kuwa huru lakini uchumi na siasa zake zinaendeshwa na mataifa ya kigeni. Baada ya wazungu kuondoka, palizuka viongozi waovu sana. Walihakikisha kwamba wamejinyakulia vyote vilivyokuwa vya wazungu kama vile mashamba na majumba makubwa. Pamoja na hayo waliendeleza dhana ya kutumikiwa na wachochole kwa malipo duni. Uhuru wa bendera kwa hivyo ukawa hauna maana tena. Kidagaa kimemwozea ni riwaya ya watu kujisaka na kujitafuta. Katika kujisaka huku wanang’amua makosa yao kama tuelezwavyo, yanamhusu kila mtawala katili ambaye daima huwa na umma uliomruhusu kutekeleza ukatili wake. Mwandishi ametuchorea hali halisi za wanyonge wanyongwao, tena katika ardhi yao wenyewe, kwani migogoro na vita mbalimbali vina misingi katika ardhi. Mwandishi wa Kidagaa Kimemwozea amewatumia wahusika kama kipazasauti ili kufikisha ujumbe aliokusudia. Wahusika wanaotumiwa wanawakilisha watu halisi katika jamii. Wanasokomoko wamekadamizwa na kuumizwa kwa muda mrefu sana. Mali yote wanayochuma inawaendea mabwanyenye na wanabaki kuwa mafukara kila uchao. Wanasokomoko wanaafikia uamuzi kuwa hawana budi ila kuanza vita vya ukombozi pasina matumizi ya silaha zozote Mwandishi amelisawiri swala hili kwa njia inayoafikiana na ukweli wa kijamii. Katika jamii lengwa ni dhahiri kwamba viongozi wa nchi walidhihirisa ubinafsi uliokidhiri. Kutokana na hayo mateso, wanapata ni bayana kwamba ukombozi wa kweli unahitajika haraka iwezekanavyo ili kuepuka madhara zaidi. 3 1.2 MADHUMUNI YA UTAFITI Utafiti huu unanuia; i. Kuonyesha mbinu ambazo zilizotumiwa katika kuwaumba waahusika katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. ii. Kufafanua masuala anuwai ambayo mwandishi ameyashughulikia katika kazi yake. 1.3 MASWALI YA UTAFITI Utafiti huu unaongozwa na maswali ya utafiti yafuatayo. i) Ni mbinu zipi zilitumiwa kuwaumba wahusika katika Kidagaa Kimemwozea? ii) Je, ni vipi mwandishi ameshughulikia maswala anuwai katika kazi yake? 1.4 SABABU ZA KUCHAGUA MADA Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea ilichapishwa mwaka (2012) na kwa hivyo haijashughulikiwa na wahakiki wengi. Riwaya hii inazungumzia ukoloni mamboleo na madhara yake katika nchi nyingi za Kiafrika. Waafrika wengi waliamini kwamba baada ya wakoloni kuondoka wangeweza kujitawala na kujiendeleza tena. Hili halikuafikiwa kwa sababu watawala wapya walionyesha uovu zaidi hata kuliko wakoloni. Kwa hivyo, uhuru katika nchi nyingi haukuleta mabadiliko yaliyokusudiwa na kuwa uhuru wa kupeperusha bendera tu. Waandishi wengi wa Afrika Mashariki wamechangia swala hili la kuvunjika kwa matumaini kwa watu wa majanibu haya kutokana na usaliti wa viongozi wao wapya Ken Walibora katika riwaya yake ya kidagaa kimemwozea amesawiri swala hili kwa kina na kuonyesha namna wanyonge kwa ushirikiano wanavyoweza kujinasua kutokana na hali hii ngumu. 4 Kazi yetu imepata msukumo kutokana na ukweli kwamba mataifa changa bado yamo kwenye mapambano ya kutatua matatizo yao mengi na kwa kuwa Ken Walibora katika riwaya hii ya Kidagaa Kimemwozea ameyamulika maswala haya kwa kina tulionelea kazi hii kama mwafaka kwa utafiti wetu. 1.5 UPEO NA MIPAKA Tumejikita katika Kidagaa Kimemwozea ya Ken Walibora. Tumechunguza suala la maudhui na fani. Kwa upande wa fani tumeshughulikia kipengele cha wahusika pekee. Tumegawanya wahusika katika makundi matatu. Wahusika wakuu, wasaidizi na wajenzi. Tumezingatia nadharia mbili umuundo na uhalisia wa kijamaa. 1.6 YALIYOANDIKWA KUHUSU SOMO HILI Kimani, N (1987) alishughulikia maudhui ya mapinduzi katika riwaya za kisiwani Zanzibar. Aliangazia mambo yote muhimu yaliyopelekea kutokea kwa mapinduzi kwa wakati huo. Kazi hii ilitupatia mwanga wa kutuwezesha kuyamulika mambo yaliyopelekea mapinduzi katika Kidagaa Kimemwozea. Lugano (1989) anaonyesha juhudi za mhusika wa kike za kujikomboa zinavyokatizwa kutokana na maonevu ya jamii yake. Wanadhulumiwa katika misingi ya nafasi wanazozichukua katika riwaya na jinsi nafasi zao zinavyoweza kutumiwa kama misingi ya kufasiri maonevu. Ameonyesha vile suala la udhalimu dhidi ya wanawake lilivyopewa kipaumbele na pumzi mpya za kuendeleza harakati zao. Muindi, A (1990) alichanganua usawiri wa wahusika makahaba katika vitabu vya Said A Mohamed. Wahusika hawa wamepewa wasifu kimaumbile unaooana na majukumu walivyosawiririwa kuyatekeleza. 5 Ndungu, N. (1996) alishughulikia uhakiki wa fani katika riwaya za Katama Mkangi. Riwaya hizi ni pamoja na Ukiwa, Mafuta na Walenisi.Katika sura ya tatu alichanganua jinsi baadhi ya wahusika wameumbwa na majukumu yao. Aligusia kuhusu mbinu zilizotumika kuwaumba wahusika hao kama vile majazi, kidrama na nyinginezo. Kurger (1998) alichanganua riwaya na hadithi fupi. Aliongea kuhusu usawiri wa wahusika wa kike na akatetea wahusika wakuu. Alilalamika kwamba ni vigumu kupata kazi za kifasihi ambapo wahusika wakuu ni wanawake, mara nyingi huwa wahusika wajenzi. Aligusia pia kuhusu waandishi wa kazi za kifasihi ambapo wahusika wa kike ni wachache. Hata hivyo mabadiliko yametokea na baadhi ya waandishi wamewapatia wahusika wa kike nyadhifa muhimu katika kazi zao. k.m Utengano (1980), Tumaini (2006), Rosa Mistika (1971), Nguvu ya sala (1999), Mwisho wa Kosa (1987) n.k. Pia waandishi wa kike wamejitokeza kwa wingi, kama vile Clara Momanyi, Z. Burhani na wengine wengi. Mongeri,O. (2000) alishughulikia baadhi ya wahusika katika kazi za Shaaban Robert akimnukuu Mbughuni (1978:99). alisema kwamba wahusika katika hadithi hufanana na binadamu lakini si binadamu. Kinyume cha maadili ni uovu, ambao una chanzo chake katika ukosefu wa mafunzo. Anatoa mfano wa Hasidi na Mwivu katika riwaya ya Adili na Nduguze, wanadhihirisha uovu kwa sababu waliyapuuza mafunzo ya kimaadili na hivyo basi kufanya mioyo yao kudumaa. Anaonyesha tabia za wahusika waovu. Momanyi, C. (2000:23-24) swala la mhusika wa kike katika fasihi ya Kiswahili linabainisha tofauti kati ya mhusika wa kike na mhusika wa kiume kwa hali mbalimbali. Mulila A.K (2005) aliandika kuhusu muala na mshikamano katika Kiswahili: umuhimu wake katika uchanganuzi wa riwaya ya Vipuli vya Figo. Sura ya tatu iligusia usawiri na majukumu ya 6 wahusika. Mulila alisema, uthabiti wa uhusika ni jambo ambalo huchangia mshikamano wa matini.Haitoshi riwaya kuwa na wahusika tu, wahusika hawa ambao ni mahsusi kwa riwaya fulani, lazima watekeleze majukumu yao ya kisanaa katika riwaya hiyo. Otieno, O.N (2005), anazungumzia kuhusu matilaba na utendi wa malengo na wahusika. Kimsingi uumbaji wa wahusika na mahusiano yao wenyewe kwa wenyewe, na yale wanayoyaeleza na kuamini kwa kiasi fulani ni ufunguo muhimu wa kubainisha matilaba ya mwanadamu kwa kuwa humithilisha jamii halisi ya ulimwengu tunamoishi. Katola,E (2006) aligusia masuala yanayomhusu mhusika wa kike. Asema kwamba mhusika huyu anadhulumiwa sana na anapewa nafasi ya pili baada ya mwanamume. Yeye aliyataja maonevu yote ya kimwili yanayofanyiwa wanawake kwa jumla. Traore (2008:63-72) uchunguzi wake unajikita katika suala la familia na jamii katika riwaya sita zifuatazo za Said Ahmed Mohamed. Asali Chungu (1978), Dunia Mti Mkavu (1980), Utengano (1980). Kiza katika Nuru (1988), Tata za Asumini (1990), Babu Alipofufuka (2001), katika uchunguzi wake alipata kuwa katika karibu riwaya zote matatizo ya kifamilia na nafasi ya mwanamke ni maudhui yanayosababisha matatizo makubwa kwa wahusika wa kike. Hii inadhihirika katika wahusika kama Maimuna katika Utengano, Semeni katika Asali Chungu. Asumini Katika Tata za Asumini na Bi Kikuba katika Babu Alipofufuka. Maudhui haya yamejitokeza katika Kidagaa Kimemwozea na yanawamullika wanawake kama vile Dora, Zuhura, Imani, Lowela na wengineo. Traore anachunguza wahusika katika muktadha wa kifamilia katika jamii husika, ameonyesha namna ambavyo mifumo ya kifamilia na kijamii inavyowaathiri wahusika kimawazo. Uchanganuzi huu ulitusaidia kuchunguza uumbaji wa wahusika na matukio yanayowapa hamasa kutenda wanavyotenda na athari ya vitendo vyao kwa wahusika wengine. 7 Wanyonyi, C.M (2011) alishughulikia uhakiki wa riwaya ya Nyuso za Mwanamke: mtazamo wa kisaikolojia changanuzi. Hii ni kazi iliyosheheni uchangamano wa kimsuko, kihusika, kimtindo na kisimulizi. Alishugulikia wahusika wanaosumbuka kimawazo kutokana na mitagusano wanayokumbana nayo, wao wenyewe au na wahusika wengine. Hali hii ya kutatizika huku kwa wahusika hutokana na kudhibitiwa na sheria za kaida za kijamii zinazowanyima uhuru wa kujiamulia hasa kuhusu suala la uana. Wahusika wa kike wamepewa nafasi ya chini lakini juhudi zao za kujikwamua hazifui dafu lakini katika kazi hii mhusika Nana anaonyesha kufaulu kujikwamua na kujipata kutokana na juhudi zake. Hata hivyo, Wanyonyi ameshughulikia baadhi tu ya wahusika lakini sisi tumeshughulikia wahusika wote katika riwaya Kidagaa Kimemwozea mhusika Imani ameonyesha juhudi za kujikwamua. Mirikau S. A (2011) anadai kwamba, ni muhimu kuyahusisha masuala ya fasihi na masuala mapana ya jamii kwa sababu katika hali fulani fulani, tajriba za maisha halisi zinaathiri jinsi wahusika wa kifasihi wanavyosawiriwa. Kwa upande mwingine, usawiri wa wahusika katika fasihi ni kielelzo cha falsafa tawala katika jamii maalum. Kwa kujikita katika uelewa huu, kazi hii inajitwika jukumu la kutafiti jinsi wahusika wamesawiriwa na kujitokeza katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea na jinsi mwandishi mwenyewe anavyoielewa na kuishughulikia. Maudhui ya mapinduzi na ambadiliko ni bayana katika kazi nyingi. Nafasi ya mwanamke katika jamii imepewa kipaumbele na wahakiki wengi na hili linaonyesha kwamba ukombozi wa mwanamke bado haujapatikana. 8 Wahusika ni muhimu katika fasihi yoyote ile kwa kuwa huwa msingi muhimu wa matukio yanayoisukuma hadithi, huwa jira ya kuendelezwa kwa dhamira na nguzo muhimu ya ulimwengu wa hadithi. Kazi ambazo zimeandikwa kwa misingi ya “uhalisia wa kirasimu” huwa na sifa za mfanano mkubwa kati ya wahusika na binadamu kuliko zilizoandikwa kwa mitindo ya kiusasa au kimajaribio. 1.7 MSINGI WA KINADHARIA Utafiti huu unaongozwa na nadharia mbili ya uhalisia wa kijamaa na umuundo. 1.7.1 UHALISIA WA KIJAMAA Uhalisia wa kijamaa ni nadharia ya kutunga na kuhakiki kazi za kifasihi inayonuia kuonyesha jamii katika uyakinifu wake na kuonyesha hatua zake za kimabadiliko. Baadhi ya waasisi wa nadharia hii ni George Lukacs, Marxim Gorki, Zhadnov na wengine wengi. Mawazo yao yamekuwa na umuhimu mkubwa katika mapambano ya wanajamii ya kutaka kuboresha hali yao ya maisha. Mapambano haya ni baina ya matabaka mawili ya mabwanyenye na wachochole. Wachochole wanashirikishwa katika kuzalisha mali lakini faida yote inawaendea mabwanyenye. Hali hii ndio inayoleta mkinzano katika jamii na hautaisha mpaka mfumo wa uzalishaji mali uwe mikononi mwa wafanyikazi walio wengi. Maxim Gorki, mmojawapo wa waasisi wa uhalisia wa kijamaa, alisema kwamba mambo yote mazuri yanayotamanika ulimwenguni yameumbwa au kuelewa na binadamu. Anashikilia kwamba maisha ni matendo. Lengo la kuishi ni kukuza na kusambaza vipawa vitakavyomwezesha mtu kupigana na kushinda pingamizi dhidi yake. Pia adumishe afya yake ili aweze kuishi kwa furaha, na afurahie uwezo wake wa kudhibiti na kuitawala dunia. 9 1.7.1.1 MIHIMILI YA UHALISIA WA KIJAMAA Kulingana na Wafula na Njogu (2007) wahusika wa kimaendeleo; ni wahusika wanaonuia kuipindua na kuibadilisha hali yao ya maisha. Ni wahusika wenye nia ya kumiliki njia kuu za kuzalisha mali katika jamii yao. Kulingana na waandishi hawa uhalisia wa kijamaa unahusishwa na misimamo ifuatayo: i. Pamoja na kusawiri matukio kihistoria, wahusika hutekeleza matendo yao kitabaka. Hufanya hivi kimakusudi au bila kufahamu la mno ni kwamba tabaka la wanyonge hujifungata masombo kujipa mamlaka na nguvu za kiuchumi. ii. Uhalisia wa kijamaa huzingatia maslahi ya wachochole. Hawa ni mafukara wa ulimwengu wenye nia ya kuimarisha udikteta wa makabwela. iii. Binadamu huonyeshwa kiuyakinifu wahusika ambao hutumiwa kama vipasa sauti vya watunzi hupuliziwa uhai mathalan wanadamu wa kawaida wanaoishi katika ulimwengu tunaofahamikiwa nao. iv. Huonyesha matumaini juu ya kizazi cha binadamu. Hii inamaanisha kwamba mtu atakuwa mshindi au ni mshindi dhidi ya unyonyaji na unyanyasaji wa aina yoyote. v. Lugha inayotumiwa katika uhalisia wa kijamaa inaendeleza malengo na mapendekezo ya walio wengi katika jamii. Ni lugha rahisi inayoeleweka na maskini. Kwa mujibu wa nadharia hii fasihi inapaswa kumsaidia binadamu ajikomboe na apate matumaini maishani. Pia, iwe ni ya kiyakinifu, na isaidie katika kuielekeza jamii kutoka katika uozo hadi maisha mazuri zaidi. Mfumo mpya ambao hauna matabaka utaweza kufufuliwa kupitia mabadiliko hayo. 1.7.2 UMUUNDO Robert Scholes (1974:60) Structuralism in Literature anaelezea kwamba msingi wa umuundo ni urasimu na hivyo kutilia mkazo umuhimu ulioko kati ya nadharia hizi mbili. Baadhi ya wataalamu waliohusika na urasimu ni walewale walihusika na kuendeleza nadharia ya umuundo. 10 Kama vile Roman Jakobson na Rene Wellek. Umuundo uliibuka katika miaka ya (1940-1950) hasa kutokana na jitihada za wana-isimu wa shule ya Prague. Wafula na Njogu (2007:97-102) wanasema kwamba, umuundo unapinga wazo la kijadi linalodai kwamba fasihi ni tokeo la mchango wa maudhui na fani.Dhana ya kimapokeo kuhusu fasihi inasema kwamba fasihi ni umbo lenye viungo viwili, Maudhui na fani na kwamba viungo hivi vyaweza kutenganishwa. Hapa, muundo unafananishwa na mtindo ukimaanisha lugha inayotumika katika maandishi au mazungumzo ya kifasihi (Leech& Short, 1981) Umuundo unashikilia kwamba dunia ni umbo lisiloweza kugawika. Dunia haikuundwa kwa viungo vinavyoweza kutenganishwa na kujisimamia bali imeundwa kutokana na mahusiano ya miundo. Hii miundo inapaswa kufikiriwa kijumla (Scholes, 1974; Hawkes,1977; Culler; 2003) Kabla ya umuundo kutumiwa katika fasihi, ulijaribiwa kwa mafanikio makubwa na mwanaisimu Ferdinand de Saussure katika kuzungumzia muundo wa lugha, alisema kuwa lugha ina sehemu mbili zinazojidhihrisha katika usemaji: Lugha dhahiri na lugha dhahania. Kwa jumla, kama ambavyo muundo wa lugha ni mfumo, muundo wa fasihi una vipengele vinavyotegemeana na vinavyoelezwa katika muktadha wa vipengele vingine. Katika kazi ya fasihi kuna vitendo vya kisanaa kama vile maudhui, ploti, wahusika muktadha na lugha. Hakuna kipengele cha fasihi kati ya hivi kitakachoelezwa vizuri katika upekee wake. Lazima kielezwe kwa kuzingatia, kuwepo kwa jukumu la vipengele vingine. Katika, kwa mfano, kuzungumza ploti, wahusika watashirikishwa na lugha yao kuzingatiwa. Nadharia ya umuundo husisitiza vipengele vya kazi ya sanaa, jinsi vinavyohusiana hadi kuikamilisha kazi hiyo. Huangalia namna sehemu mbalimbali za kazi ya sanaa zimefungamana. Riwaya, kwa mfano, huangaliwa kama zao linalojitosheleza. Riwaya ina msuko wahusika na mbinu mbalimbali za kusimulia ambazo huingiliana na kuchangiana. Mambo hayo ndiyo hufanya riwaya kuwa muundo unaojitosheleza. 11 1.8 MBINU ZA UTAFITI Utafiti huu ni wa maktabani. Tumetumia mbinu kadha kama vile kusoma riwaya ya Kidagaa kimemwozea kwa uzingatifu mkubwa ili tuweze kuichanganua vyema. Maandishi yanayoelezea nadharia za uhalisia na umuundo yalikuwa nguzo muhimu katika utafiti na uelewa wa ndani wa nadharia ili tuwe na mwongozo bora wa kazi yetu. Tulidurusu vitabu, tasnifu na makala yanayohusiana na utafiti wetu.Udurusu huu na usomaji wa kina tuliyoufanya ulituwezesha kutazama riwaya katika misingi ya nadharia tulizoziteua. 12 SURA YA PILI MAUDHUI KATIKA KIDAGAA KIMEMWOZEA 2.0 UTANGULIZI Katika sura hii tutashughulikia maudhui kama yanavyojitokeza katika Kidagaa Kimemwozea. Mwandishi ameangazia mambo mengi anayoyaona katika jamii yake. Baadhi ya mambo haya ni uozo wa viongozi ambao umekithiri sana kila uchao. Viongozi wamekadamiza na kuwanyanyasa wananchi na hawana huruma hata kidogo. Wamejinyakulia mali yote na kuwaacha wananchi kwenye umaskini wa hali ya juu wamenyanganywa mashamba na kuachwa katika dhiki ya njaa. Mtemi Nasaba Bora ndiye anayeongoza katika uovu huu. Wananchi wameshindwa la kufanya ila kumtazama tu. Wanajamii wameanza kutafuta njia za kuungana ili waweze kushirikiana katika shughuli mbalimbali za mabadiliko na hatimaye ukombozi. Vijana wanajitolea kuikomboa jamii kutokana na uovu huu na tunaona bidii zao zikifua dafu. Miongoni mwao ni Amani, Madhubuti, Imani na wengineo. Maudhui mengine yaliyojadiliwa katika ka kazi hii ni kama vile ufisadi, ukatili, ulevi, uasi, utabaka , ujamaa, ushirikiano, uzembe, tama, malezi, utu, umaskini, uozo unaoendelezwa na viongozi na mengineo. 2.1 DHANA YA MAUDHUI Kulingana na Kimani na Chimerah (1999:21-23) maudhui ni ujumbe wa jumla kuhusu matukio, kitu, wahusika au hali ya maisha kama yanavyojitokeza katika kazi za kifasihi.Maudhui ni sehemu ya maana na huingiliana na mada. Ni katika maingiliano baina ya mada na maudhui ambapo ukweli uliokusudiwa na mwandishi hujitokeza. Ukweli wa Mtemi Nasaba Bora, Katika Kidaga kimemwozea haupatikani katika wahusika, vitendo au mandhari peke yake. Ukweli upo katika ubainishaji wa ukadamizaji wa ukoloni mamboleo na ulazima wa ukombozi katika mazingira ya unyanyasaji. 13 Maudhui ni mawazo ya jumla, mawazo mapana yanayowasilishwa katika wakati maalum kadri kazi inavyoendelea. Utoaji muhtasari wa masimulizi ni hatua ya mwanzo tu. Kauli za jumla lazima ziunganishe mada na kipengele maalum cha usimulizi. Kauli za jumla lazima zifungamanishwe na kazi yenyewe. Maudhui ni maana ya ndani ya kazi ya fasihi. Katika Kidagaa Kimemwozea tumepata kwamba kuna mvutano baina ya pande mbili nazo ni matabaka mawili ya kijamii. Matabaka haya yanapimana nguvu na kuvutana, kwa sababu tabaka moja la juu la akina Mtemi Nasaba Bora limekamia kuvuna matunda yote ya uhuru na hivyo kulisahau tabaka jingine la chini la akina Amani. Tabaka la chini linadai haki yake na linatisha kutumia nguvu, ikibidi. Suala la ukandamizaji na mivutano ya kitabaka linalojitokeza kwa uwazi. Kulingana na Wamitila (2002:53-54) neno dhamira hutumiwa kurejelea suala fulani au ujumbe au lengo la kazi hiyo. Dhamira ni ile jumla ya maana anayoivumbua mwandishi aandikapo na jumla ya maana anayoitambua msomaji katika usomaji wake. Tunaweza kuivumbua maana ya kazi fulani kwa kuisoma kazi hiyo kwa kina na makini, huku tukiuelewa na kuungamua uhusiano wa visehemu mbalimbali pamoja na jinsi visehemu hivyo vinavyohusiana na kazi nzima na kuvijaza kitu kimoja. Dhamira kwa upande wake haiyahusishi majibu bali huzua maswali. Dhamira pia huingiliana na vipengele vingine vya kazi kifasihi ili kuunda kitu kimoja. Vipengele hivi ni pamoja na dhamira na wahusika, msuko, uhamasishaji, mandhari, mtindo, thamani toni na kadhalika. Dhamira ni lengo au shabaha ya kazi ya fasihi kwa mfano katika Kidagaa Kimemwozea dhamira ya mwandishi ni kuonyesha namna utawala mbaya huwapelekea wanyonge kuwa na ilhamu ya kujinasua kutoka uongozi mwovu, na hivyo kutafuta ukombozi. Wana-uhalisia wanaamini kuwa 14 dhamira ya kazi, usawiri wa wahusika,matumizi ya lugha na mandhari ya kazi ya kifashi lazima yaonyeshe na yaafikiane na uhalisi wa maisha. 2.1.1 UOZO WA VIONGOZI Maovu ya viongozi wa nchi ya Tomoko ni mengi mno. Viongozi wabovu husababisha mateso yasiyoneneka kwa raia wake. Katika Kidagaa Kimemwozea tunapata kuwa vijana wawili Amani na Imani wote waliteseka mno kutokana na uovu wa Mtemi Nasaba Bora. Pia yeye ndiye aliyepanga njama za kuuawa kwa Chichiri Hamadi ili anyakue shamba lake. Kifo hicho baada ya kutekelezwa na majambazi waliotumiwa na Nasaba Bora, kilisingiziwa Yusufu mwanawe Hamadi. Hila hizo zilimfanya Yusufu afungwe jela kifungo cha maisha ingawaje hakuwa na hatia. Mtemi alipokuwa waziri wa ardhi alibadilisha hati za wamiliki halali na kuunda (kughushi) zake. (uk. 15) Alitumia hati ghushi kudai sehemu hizo. Udhalimu huu ndio uliomfanya mama Imani apigwe na askari katili. Kipigo hicho kilipelekea kifo chake. Mwanawe Oscar Kambona aliathirika na kitendo hicho na kutoroka nyumbani. Uovu huo uliotendwa kwa amri ya Mtemi ndio uliopelekea Oscar kuwa mhalifu na kutumia mihadarati na kupelekea kufungwa kwake. Viongozi wa Tomoko walikuwa hawana huruma na afya ya wananchi hata kidogo. Jinsi walivyotumia pesa za msaada wa Uingereza wa kujenga zahanati kubwa ni dhihirisho tosha. “Zahanati ya Nasaba Bora ilijengwa kwa auni ya fedha kutoka kwa serikali ya Uingereza. Uingereza ilitumaini kuwa zingetumika kujenga hospitali kuu. Zilipoingia mikononi mwa Waafrika wasimamizi zikapata matumizi mengine muhimu. Akali ndogo sana ilitumika kujenga zahanat ndogo iliyopewa jina la mojawapo wa wasimamizi wake, yaani Mtemi Nasaba Bora. Akali kubwa ikaingia mifukoni mwa wasimamizi hao.” (uk 144). Ukweli ni kuwa walijenga kizahanati kidogo na fedha hizo zilibadilishiwa matumizi na viongozi wabovu na hatimaye lengo halikufikiwa. 15 Nasaba Bora baada ya kurithi mali na tabia za kizungu aliendelea na tabia yake ya rushwa. Alihonga watu wengi sana baada ya kumuua Chichiri Hamadi. “Ilibidi kulipa fedha nyingi za kadhongo, kuwalipa polisi, makarani wa mahakama, majaji, wajue tena mti hauendi ila kwa nyenzo.”(uk 150). Hii ilikuwa tabia yake, maana alipotaka Madhubuti apate kazi jeshini alifanya yayo hayo. Wakuu hao walikwenda zao na tita zuri la noti mfukoni kila mmoja. 2.1.2 UTABAKA Katika kazi hii, mtunzi amesawiri na kuwasilisha uhalisi wa utabaka katika jamii iliyozingatiwa. Watu katika riwaya hii wamegawika katika tabaka mbili kuu, kundi la wenye mali tele na kundi la wachochole. Awali, tabaka la wenye mali lilikuwa la wazungu lakini baada ya kupata uhuru, baadhi ya wananchi wa Tomoko waliingia katika kundi hilo. Baada ya uhuru, hali ilibaki kuwa hiyo hiyo ila wazungu kina Major Noon (Majununi) waliondoka na kuwaachia wenyeji nafasi hii. Nafasi ya Major Noon ilichukuliwa na Mtemi. Mtemi anaendeleza unyanyasaji na ubaguzi kwa watu walio wanyonge. Aliishi katika jumba la kifahari mno na alikuwa na mashamba na watumishi. Licha ya mali hizo alikuwa na mshahara. Alikuwa na mazoea ya kuwatumia na kuwafukuza wafanyi kazi wake. Amani mfanyikazi wake alikuwa akiishi katika kibanda ilhali yeye aliishi kwenye kasri. Alimlipa mshahara wa kijungumeko na maisha ya Amani yakawa yasiyotamanika. Watu wa tabaka la chini waliteseka kwa kuishi kwenye maskani duni, mshahara duni, ukosefu wa mavazi, chakula bora na kadhalika. Matajiri walitumia uwezo wao katika kuwanyanyasa watoto wadogo. Kwa mfano DJ mwenye miaka kumi badala ya kupelekwa shule aliajiriwa kuchunga ng’ombe kwa Maozi. DJ alikuwa na kaptula moja tu. Utabaka pia umejidhihirisha vizuri wakati wa sherehe za sikukuu ya Wazalendo. Wageni wateule pamoja na wenyeji wenye mamlaka kama Mtemi, walikuwa wameketi kwenye viti, 16 kwenye banda lililotandaziwa tarubai ilhali wenyeji kama vile Amani walisimama uwanjani jua likiwa paa lao. Enzi za ukoloni wazungu walikuwa wanaaishi katika eneo lao pekee. Pia kulikuwa na maeneo au sehemu zilizotengewa watu weusi kwa mfano Baraka, Ulitima, Umoja na Mabondeni. Watu wa sehemu hizo ndio waliokuwa wanatumikia tabaka la juu kwa mishahara duni. Tabaka la juu lilikuwa la wazungu wakati wa ukoloni. Hawa walimiliki ardhi kubwa. Walipanda mazao ya biashara na kufuga mifugo ya kisasa. Waafrika hawakuruhusiwa hata kidogo kuendesha shughuli hizo kama mwaafrika alitaka kufanya shughuli hizo alitakiwa kuzifanyia nje ya Sokomoko. 2.1.3 UMUHIMU WA ELIMU Elimu ni muhimu sana maishani. Katika nchi nyingi za kiafrika mwandishi anaonyesha kuwa elimu inayopewa kipaumbele ni ile ya darasani. Suala hili limejidhihirisha vizuri kupitia Mwalimu Majisifu aliyepelekwa ng’ambo na marehemu babake kupata shahada. Mtemi alisoma mpaka darasa la nane. Alisomesha Madhubuti hadi chuo kikuu huko Urusi. Pia alimsomesha Mashaka japo aliamua kujiingiza katika mapenzi na kuishia kidato cha tatu. Amani alipokuwa chuoni aliongoza darasani. Lakini kutokana na wivu wa wanafunzi wenzake, alifanyiwa hila na kufungwa jela. Amani wakati alipokuwa akitoa hotuba ya kumpokea kaimu wa Mtemi aliwahimiza watu wajipatie “elimu” ili waweze kushinda katika mapambano. Amani alisema, “Mimi nashauri hivi, hatua ya kwanza ni Elimu…. Elimu ya kujielewa sisi ni nani…” (uk. 158). Aliwaambia kuwa ile elimu anayoipigania upatu si ile ya shahada zipatikanazo vyuoni, bali anataka elimu ya kujitambua kuwa wao ni nani, wanatoka wapi, wanaelekea wapi na wangerejeshaje utu kutoka kwa wapokonyaji? 17 Katika nchi ya Wangwani watu walimiminika katika chuo cha Mkokotoni kwa sababu ya kiu ya kupata maarifa zaidi kutoka kwa Mwalimu Majisifu. Chichiri Hamadi alikuwa mhadhiri wa chuo kikuu huko London. Kwa hivyo ni bayana elimu katika riwaya hii inachukuliwa kuwa na utenda kazi tofauti. Kuna wale wanavutiwa nayo kwa kuwa wangependa kuitumia kupata ajira lakini wengine wanaichukulia kama chombo cha kumkomboa mwanadamu. 2.1.4 ULITIMA Ulitima ni hali ya kuwa katika shida kuu za kiuchumi. Ni uchochole au ukata unaotokana na udhaifu wa maisha. Kutokana na ukoloni mamboleo wananchi wengi wa Tomoko walikuwa maskini. Uhuru wao ulikuwa wa bendera tu. Hali hiyo ilisabababishwa na mfumo mbovu wa utawala. Mama yake DJ alikuwa maskini. Ili kujikimu kimaisha yeye na familia yake alilazimika kupika pombe haramu kwenye mtaa wa Madongoporomoka mjini Songoa. Bila shaka mtaa huo ulikuwa na watu maskini wenye nyumba mbovu. Watoto wengi walikatisha masomo yao kwa kukosa karo. Mfano, Imani na kaka zake walishindwa kuendelea na shule baada ya mama yao kushindwa kumudu gharama za masomo. Watoto walioajiriwa kuchunga ng’ombe walikuwa wanavaa vazi moja tu la kaptula. Pamoja na hayo DJ alikuwa na utapiamlo. Ulitima mkubwa unadhihirika katika kibanda cha Amani huko Sokomoko katika shamba la Mtemi. Wakati mmoja alipotaka kubadilisha nguo, ilimbidi amwombe Imani ageuke kando au afumbe macho ili abadilishe. Kibanda kilikuwa kidogo mno bila chumba cha stara. Hata kabla ya kuja Sokomoko Amani alikuwa maskini. Umaskini wake ulizidi baada ya kifo cha mama 18 yake. Alitembea kwa miguu kutoka kwao Ulitima hadi Sokomoko kwa ukosefu wa fedha za nauli. 2.1.5 MALEZI Wazazi wana jukumu kubwa katika malezi ya watoto wao kwa sababu watoto wanahitaji kujengewa msingi imara katika maisha yao ya baadaye. Kwa mfano, baba yake Mtemi alijaribu kuwalea vizuri Mtemi na Mwalimu Majisifu. Aliwapa maadili kutoka Bibilia japo hawakuyatekeleza katika maisha yao ya baadaye. Dora alihangaika kuwalea watoto ambao walikuwa taahira. Alifanya kazi hiyo bila malalamishi. Aliwalinda mapacha hao ambao walinusurika kutupwa mtoni na Mwalimu Majisifu. Mama yake Amani alijitoa kwa hali na mali akamlea Amani vizuri. Alimpa mahitaji yote ya kimsingi ikiwa ni pamoja na kumsomesha hadi chuo kikuu. Kadhalika mamake Imani baada ya kifo cha mumewe alichukua jukumu la kutunza watoto alioachiwa. Watoto hao walikuwa ni pamoja na Oscar, Chwechwe na Imani. Pia baba yao Mtembezi alikuwa na mpango wa kuwapa watoto wake malezi ikiwa ni pamoja na kuwaachia urithi. Alifanya kazi kwa bidii kwa Majununi akanunua shamba Baraka. Kuna baadhi ya wazazi wengine walioshindwa kutoa malezi yafaayo kwa watoto. Watoto wao walipotoka kwa mfano, Ben Bella mtoto wa Maozi alikuwa mwizi na hakuzingatia ulezi aliopewa. Lowela binti Maozi alionyesha ukosefu wa malezi bora kwani alikuwa anatembea na Mtemi. Lowela alipata mimba na kuificha kwa kuwa alifahamu kuwa kitendo kile siyo kizuri na ni kinyume cha maadili aliyopewa. Amani na Imani walijaribu kumlea mtoto Uhuru na ingawa hakuwa wao kiuhalisia. Mtoto Uhuru aliaga baadaye kwa kukosa matibabu katika zahanati ya Nasaba Bora. 19 2.1.6 NAFASI YA MWANAMKE Katika ndoa za kitamaduni, mwanamke yu chini ya mumewe. Hapaswi kupinga anayotenda mumewe. Ndoa hizi hupatikana katika jamii ambazo taasubi ya kiume imezagaa. Katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea mwanamke amepewa nafasi chanya na hasi. Mwanamke ni mtu mwenye huruma. Haya yanadhihiririshwa na Bi Zuhura, alionekana kuwa na huruma kwa watu kwa mfano, alimhurumia DJ Bob baada ya kungatwa na mbwa. Alikuwa akiwasaidia Amani na Imani kwa siri ili waweze kumlea mtoto Uhuru. Imani pia ana huruma, alimwonea huruma mtoto Uhuru ndiyo maana aliamua kulea akishirikiana na Amani. Ni mvumilivu, Dora alitimiza majukumu yake ya ulezi na kuwapenda wanawe waliokuwa walemavu. Alivumilia pia matusi ya Majisifu, ulevi wake na kutowajibika kwake. Uvumilivu unaonekana pia kwa Bi. Zuhura, alivumilia ukali na ukware wa Mtemi. Mwanamke ni msaidizi. Anatakiwa apewe nafasi muhimu kama mwanamume katika jamii. Hili linadhihirishwa na Imani aliyekuwa na msimamo kamili na kushiriki katika harakati za kupata uhuru wa pili kutoka kwa wakoloni weusi, wanawake pia ni wazalendo. Tuliona jinsi walivyohudhuria sikukuu za Wazalendo wakiwemo vikongwe na waja wazito. Mwanamke amechorwa kama mkombozi, Imani alishirikiana bega kwa bega na Amani katika kuibadilisha jamii kimtazamo na kimatendo Aliukomboa umma wa Sokomoko kwa kuvunja imani potofu ya kutoyanywa maji ya mto Kiberenge. Kwa upande ule mwingine mwanamke amechorwa kama chombo cha starehe. Mtemi alikuwa akijistarehesha na Lowela mwanafunzi wa shule ya Kinondani. Pia hana huruma, aliweza kumtelekeza mtoto mlangoni kwa Amani, mtoto aliyemzaa yeye mwenyewe. Katika 20 barua yake kwa Mtemi alikuwa anaringia umbo lake la kisichana na kumkashifu Bi Zuhura. “Je, kweli nalinganishika na yule ajuza wako mwenye manyama tembweretembwere kama ya nguruwe?” (uk. 105-106) Dora alinyanyaswa kwa kuzaa watoto walemavu. Mwanamke anakumbwa na uonevu unaotokana na hali za kibayolojia ambazo hana uwezo nazo. Pia, Dora alituhumiwa na mwalimu Majisifu kuwa yeye ndiye chanzo cha kuzaa watoto walemavu. Mwalimu alifikiria kuwa mke wake yawezekana ndiye mwenye dhambi na laana. Kwa hivyo mzigo wote wa ulezi aliutupia mke wake. 2.1.7 UASI Maudhui ya uasi yanajitokeza kupita kwa Madhubuti mwanawe Mtemi anayerudi masomoni kutoka Urusi. Madhubuti alionyesha dalili za uasi alipomwandikia babaye barua akiwa masomoni Urusi. Alielezea kutopendezwa na matendo na mienendo yake. Miongoni mwa mambo mengi barua yake ilisema yafuatatayo. “ Naomba mradi wa kunitafutia ajira jeshini au popote usitishwe, sitaki ajira ipatikanayo kwa mirungura au ushawishi wa kisiasa …” (uk 87 – 88). Barua hii ilimuudhi sana Mtemi, aliona kuwa mwanawe ambaye amegharamika hadi kufikia chuo kikuu cha ng’ambo na ambaye ni tegemeo lake kuu, hana shukrani. Madhubuti aliondoka pia kutoka kasri la Majununi la babake na kujiunga na Amani katika kibanda chake. Pia alibadilisha jina lake kutoka Madhubuti Nasaba Bora na kujiita Madhubuti Zuhura, Alikataa katakata uhusiano wowote na babake. Alitamani ajiue kinasaba na azaliwe upya. Alimlaumu na kumlaani babake wakati wa mazungumzo yake na Amani. Alisema, “Mtemi ni mfano bora wa hawa wasaliti wanaoteketeza na kuyatatiza matumaini ya bara zima” (uk 115) Alikataa kabisa wazo la babake la kujiunga na jeshi na badala yake, alitafuta kazi yake mwenyewe huko Songoa, kazi ambayo haikuwa na mchango wa babake katika kuitafuta. 21 Mashaka alikataa mpango wa wazazi wake wa kumsomesha katika shule ya upili ya Nasaba Bora na anarudi kukaa nyumbani. 2.1.8 MADHARA YA ULEVI Ulevi hupelekea mtu kutoelewana na wenzake, kutowajibika, kukosa heshima na kuonekana mjinga katika jamii. Yeyote anayeshiriki ulevi, hasa wa kupindukia, ana hatari ya kuhusishwa na sifa hizi mbaya zilizotajwa. Unywaji wa pombe katika jamii husababisha madhara mengi sana. Walevi hasa wale wenye madaraka maofisini hushindwa kutekeleza wajibu wao na hatimaye kufukuzwa kazi au kurudisha nyuma maendeleo ya jamii. Kuna visa vingi vya ulevi katika riwaya na aghalabu vinahusishwa na Mwalimu Majisifu. Mwalimu alikuwa na kazi nyingi na nzuri sana kutokana na usomi wake. Aliwahi kuwa mkurugenzi wa idara ya forodha , aliwahi kuhudumu katika redio na televisheni ya Tomoko na kuwa mwenyekiti wa Baraza la Taifa na mhariri wa gazeti la Tomoko. Pia aliwahi kuwa mhadhiri wa chuo cha ualimu na mkurugenzi katika benki kuu ya Tomoko. Kutokana na ulevi wa pombe alijisahau kimajukumu na kuondolewa katika kazi kubwa na kubaki kuwa mwalimu tu. Alikuwa amepata nafasi hizo kutokana na masomo yake. Alikuwa na shahada mbili alizozipata huko ngambo. Alipofika alisifiwa sana kama mzalendo halisi. Yeye hakubaki huko ngambo kama wanatomoko wengine. Sifa hizi zote ziliondolewa kutokana na tabia yake ya kulewa chakari. Mtemi alimlaumu kwa kulewa na kulala mtaroni siku ya sherehe ya sikukuu ya Wazalendo. Alikuwa amemwachia bibi yake mzigo wote wa kuwalea watoto wao. 22 Alikataa kunywa chai aliyoandaliwa na Bi Zuhura shemejiye kwa sababu hakuwa na hamu na chai. Hamu yake ilikuwa ni pombe tu. Pamoja na ulevi wa pombe pia panajitokeza uraibu wa bangi. Ben Bella ana uraibu wa bangi na mara nyingi alishikwa na kufungwa. Aidha, Gadafi alifungwa kwa ajili ya utumizi wa mihadarati. 2.1.9 UJAMAA Maudhui ya ujamaa yanadhihirika kupitia Madhubuti ambaye alisomea Urusi. Urusi ndiyo nchi iliyokuwa na mfumo na ukomunisti. Madhubuti hakupendezwa na mienendo ya baba yake ya kunyakua na kuhodhi mali bali alipendelea kuleta mapinduzi ambayo yangeangamiza ubinafsi na ubepari na kuanzisha ujamaa. Vitendo vya Amani vinadhihiriaha mielekeo ya kiujamaa. Amani aliporejeshewa shamba la Majununi hakulitwaa na kulihodhi peke yake. Badala yake alilikatakata vipande vipande na kugawia watu waliohitaji. Alimpa Madhubuti ekari hamsini, naye Madhubuti alikatakata vipande vipande na kugawia maskini. Alimpa Matuko Weye jumba la Majununi naye akabaki katika kibanda. Alipoanza mradi wa nyumba yake, watu wote walishirikiana kumsaidia na baada ya muda mfupi, nyumba ilikwisha. Mifano hii ni dhihirisho ya mielekeo ya kiujamaa ambayo husisitiza ushirikiano kinyume cha ukapitalisti ambao hupalilia ubinafsi 2.2.0 TAMAA Maudhui ya tamaa yanapatikana kupitia Mtemi Nasaba Bora na Mwalimu Majisifu. Mtemi alikuwa na tamaa ya mali ndiposa aliwanyanganya watu ardhi ili ajinufaishe.Hali hii ndiyo iliyomfanya Mtemi afanye mkakati wa kuwaua Chichiri Hamadi na mwanawe Yusufu ili kunyakua ardhi. Alikuwa na tamaa ya kuheshimiwa kupita kiasi. Jina lake lilitumiwa Maksudi katika huduma mbalimbali za kijamii kama vile zahanati, daraja, shule na alikuwa na mpango 23 wa kubadilisha mto Kiberenge. Pia alikuwa na tamaa ya kimwili. Mara nyingi alimdanganya mkewe kwamba anaenda kushughulikia migogoro ya shamba lakini kiuhalisia alikuwa na macho ya nje. Alikuwa na mpenzi kwa jina Lowela na hata alimpa shamba alilonyanganya mjane-mama yake Imani. Alimtamani msichana mlemavu katika matwana. Alijaribu kumshawishi awe rafiki yake. Alibadilisha nia yake alipogundua ulemavu wake. Mwalimu Majisifu naye alikuwa mtu wa kupenda sifa kupindukia. Hali hiyo ndiyo iliyopelekea kutafuta kujenga jina kwa kuiba miswada ya wenyewe na kuwahadaa kuwa ilikataliwa. Alichapisha riwaya ya Kidagaa Kimemwozea ingawa haikuwa yake ili apate sifa. Yeye na Mtemi Nasaba walijutia baadaye tamaa zao na ndipo ukweli wa methali tamaa mbele mauti nyuma ukadhihirika. 2.2.1 UTU Utu maana yake ni hali ya huruma na kumjali binadamu mwenzake kama wewe mwenyewe. Kile usichopenda kutendewa hakitendi kwa mwenzako. Kuna mifano mingi ya utu katika Kidagaa Kimemwozea. Mwalimu Majisifu baada ya kuaibika katika Chuo Kikuu cha Mkokotoni na kujifunza kutokana na matendo mema ya Imani alianza kuwa na utu. Alianza kuwahurumia watu wote walioonewa naye kama Imani.Amani, Dora na wote walioteseka kwa njia moja au nyingine kutokana na uovu wake, Bi Zuhura alikuwa na huruma na utu. Aliwahurumia wafanyikazi wake na kutamani kuwasaidia ingawa mume wake hakumuunga mkono katika suala hilo la utu. Alitaka sana kumsaidia DJ Bob kwa kumpeleka hospitali pale alipongatwa na mbwa Jimmy. Alimhurumia mama aliyekuwa akijifungua njiani wakati alitoka kwenye sherehe za Wazalendo. Alitaka Mtemi asimame wampe 24 msaada. Mtemi alikataa ombi hilo katakata. Alimhurumia mtoto Uhuru akataka kumlea lakini mume wake alikataa. Pamoja na kukataliwa na mume wake bado aliendelea kutoa chupa za maziwa kwa siri ili Amani na Imani waweze kumtunza mtoto. Imani alionyesha utu wa hali ya juu alipowatunza watoto taahira wa Dora. Aliwapenda na kuwathamini, aidha alionyesha utu zaidi alipoenda kuishi na Amani ili amsaidie kulea mtoto Uhuru. Baada ya kifo cha Uhuru alirejea kwa Dora na kuendelea na kazi. DJ Bob alikuwa na utu, alimtafuta Imani ili amjulishe kuhusu ugonjwa wa mtoto Uhuru. DJ ndiye aliyewapeleka Amani na Imani kwa Mtemi na Mwalimu ili wakapate ajira. Utu wake ndio uliomfanya Maozi amchukue kama mwanawe. Madhubuti anaonyesha utu kwa kupinga maovu yote ya baba yake kwa kinywa kipana. Amani naye anaonyesha utu kwa kumpa DJ Bob Shati baada ya kaptula yake kuliwa na fahali. Waliishi na Imani katika chumba kimoja na hakuwahi kumkosea heshima yake kama msichana. Alimheshimu sana. Baada ya kupata shamba lake aliligawanya visehemu na kuwapa waliohitaji. 2.2.2 UKOSEFU WA HAKI Nchi ya Tomoko ilikuwa na watu wengi ambao hawakutendewa haki. Katika nchi yenye ukatili, kula rushwa, uonevu na kila aina ya uovu, maadili ni kitu adimu sana. Amani anayadhihirisha haya kwa kusema, “hata haramu huhalalishwa, ati. Haramu ngapi zimehalalishwa? Chungu nzima.” (uk. 6). Katika nchi yenye sifa kama hizi wakati mwingine hata kuua watu wengine huhalalishwa hutegemea mtendaji ni nani na mtendwa ni nani. Wanasokomoko na watomoko kwa ujumla walikuwa na kiu ya haki. Nasaba Bora alikuwa akiua na kuchukua mali ya wanajamii bila aibu 25 wala hofu yoyote. Aliamrisha askari wake kuwaweka Amani na Imani mahabusu bila kosa. Pia Amani alizingiziwa mtoto asiye wake kwa sababu ya uadimu wa haki. Mwalimu Majisifu aliiba haki ya Amani kwa kumwibia mswada wa kitabu na kukimiliki yeye. Alipata sifa siziso zake na hivyo, kuchukua haki ya Amani. Aliwanyima haki watoto wa shule haki ya kufundishwa. Hata Mashaka alimlalamikia. Alishindwa kutoa mwelekeo mzuri. Wananchi walinyimwa haki ya kuwa na huduma bora za afya. Hospitali ilikuwa ndogo hivyo kukawa na msongamano wa wagonjwa wa kila aina. Wauguzi walimnyima mtoto Uhuru haki ya matibabu naye akafariki. 2.2.3 USHIRIKIANO Ushirikiano ni jambo muhimu sana katika jamii kwa kuwa huletea watu ufanisi. Katika Kidagaa Kimemwozea suala la ushirikiano ni muhimu sana kwa sababu ni kutokana nalo ndipo tumewaona wanajamii wakijinasua kutokana na ukoloni mamboleo. Amani na Imani wanapokutana kisadfa kwenye ukingo wa ziwa Mawewa, unachipuka ushirikiano unaowaongoza kupitia hatua tofauti maishani mwao, hatua ambazo zinawakomaza na kuwapelekea hatua yao ya mwisho ya ufanisi. Pia Amani na Madhubuti wanapokutana wanaanza ushirikiano mara hiyohiyo na ni kupitia ushirikiano huu ndipo wanaweza kuiokoa jamii kutokana na uongozi mwovu. Walakini, pia, kuna ushirikiano wa mizengwe unaokuwa na matokeo mabaya kwa jamii na hatuna budi kuutaja. Mtemi Nasaba anawashika mikononi wahudumu wa idara tofauti za utawala kama vile mahakimu, askari, mawakili, madaktari na kadhalika ambao aliwahonga ili wasimtambue kwa mabaya anayotenda. Kupitia ushirikiano huu anafaulu kuwaangamiza na kuwataabisha watu wengine huku akinyakua mali yao. Lakini kwa vyovyote vile sharti watu wote washirikiane ili tupate ufanisi. 26 2.2.4 UMUHIMU WA MABADILIKO Katika maisha ya kijamii mabadiliko chanya yanatakiwa sana hasa pale jamii inapokuwa haisongi mbele. Baada ya jumuiya ya Sokomoko kujikomboa kutokana na utawala wa wakoloni wazungu, bado walijitokeza “wakoloni” wengine wa kiafrika kama Nasaba Bora na viongozi wengine wachache. Hawa walikuwa vizuizi vikubwa vya kufurahia matunda ya uhuru. Hali hii inaibua wapiganaji wa silaha zisizo bunduki. Watu kama Amani, Imani, Madhubuti walichangia sana kuleta mabadiliko chanya katika jamii ya wanasokomoko. Madhubuti alishirikiana na Amani kuweka mikakati ya kuuangusha utawala wenye dhuluma na kila aina ya uonevu ili wananchi wapate uhuru kamili. Alipokuwa Urusi alimkataza baba yake kuendelea na mikakati ya kumtafutia kazi nyingine. Alitaka kuleta mabadiliko katika upataji ajira. Ajira zisitolewe kwa upendeleo. Ni vyema kuvunja mipaka ya kinasaba, kitabaka, kikabila na kadhallika kama alivyofanya Madhubuti ili mabadiliko kamili yapatikane. 2.3 KIMALIZIO Katika sura ya pili tumeangalia dhana ya maudhui. Tumeona ni vipi maudhui yanavyochangia kuuleta umoja wa kazi inayohusika. Maudhui katika Kidagaa Kimemwozea ni mengi mno. Tumepata kwamba karibu kila jambo ambalo linawaumiza wanajamii wa Sokomoko linahusishwa na Mtemi Nasaba Bora. Ni dhahiri shahiri kwamba uongozi wake ulikuwa umerudisha jamii nyuma katika nyanja sote za maisha. Jamii hii imehangaishwa na utawala mbaya na haina budi ila kupindua na kuibadilisha hali ya maisha yao. Jamii iliyojengwa katika misingi ya utabaka huwafanya watu wote kutaka kudumisha uwezo wao wa kiuchumi na kuishia kuwahangaisha wengine kwa kunyakua mali yao. 27 Wananchi walikuwa wameshindwa kuona maana ya uhuru na hawakuona tofauti yoyote baada ya wazungu kuondoka. Wao walikuwa wamekubali hali hiyo lakini ghafla vijana waliungana na wakakomesha uongozi huo mwovu mara moja. Jamii iliyokuwa imekadamizwa na kunyanyaswa ilisimama wima tena na kuanza jukumu la kujijenga upya. Ama kweli tunapongeza juhudi za vijana hawa kwa maana waliweza kuizidua jamii. 28 SURA YA TATU: SWALA LA UHUSIKA NA WAHUSIKA KATIKA RIWAYA 3.0 UTANGULIZI Sura hii inahusu wahusika katika Kidagaa Kimemwozea (2012). Katika kushughulikia kazi hii tumejikita kwenye dhana ya mhusika na njia tofauti za uainishaji wa wahusika. 3.1 DHANA YA UHUSIKA Wahusika hufafanuliwa kama watu, wanyama au vitu katika fasihi. Msokile (1992:42-43). Wahusika husawiriwa kisanaa na mwandishi ili waweze kuwakilisha dhana mbalimbali za maisha katika jamii. Mwandishi huwasawiri wahusika kwa wasomaji wake kwa kutumia sifa pambanuzi walizonazo, jinsi walivyo, mambo gani hawayapendi na yapi wanayapenda maisha yao na kadhalika. Wahusika hao hutumia misemo, nahau, tamathali za usemi na methali katika mazungumzo yao ili kujenga tabia na hali ya kisanaa. Wahusika wa kazi za sanaa huwa na tabia zinazotofautiana kati yao kwa sababu mbalimbali. Kwanza kabisa inategemea mwandishi ana lengo gani analotaka kuonyesha katika kazi yake ya sanaa. Pili, aina ya kazi ya sanaa inaweza kuathiri aina ya wahusika jinsi walivyosawiriwa, kuaminika kwao, wanavyohusiana wao kwa wao, uwakilishi wao na majina yao. Wahusika katika hadithi ni mhimili mkubwa katika fasihi andishi na hata simulizi. Msokile (1992) akiwanukuu Penina Muhando na Ndyanao Balisdya wanasema kwamba wahusika wanaweza kuumbwa kinafsia, kiakili na kimwili. Kutokana na ujenzi wa aina hii, mhusika huonyesha wasifu wake wa ndani na nje au anaweza kuonyesha mabadiliko yake kila anapokutana na mazingira tofauti. Ataonyesha mabadiliko katika uhalisia wake kwa kuzingatia nguvu zinazomzunguka kama vile za utamaduni, siasa, uchumi na kadhalika. Kwa mujibu wa 29 Wamitila (2008:369) wahusika ni nyenzo kuu katika fasihi kwa sababu wahusika ndiyo jira ya matukio na matendo yanayopatikana katika kazi ya kifasihi inayohusika. Mtazamo wa dhana ya wahusika hutofautiana kutegemea mkabala anaouchukua mhakiki na nadharia ya fasihi inayohusika. Mhusika ni mtendaji katika kazi ya kifasihi na huwa kielelezo cha viumbe wanaopatikana ulimwenguni, ingawa si lazima sifa zote za mhusika zifungamane moja kwa moja na za wanadamu. Hii ndio maana neno “Mhusika” linatumika bali si ‘mtu’ au ‘kiumbe’. Mwelekeo wa kuwahusisha wahusika wa kifasihi na binadamu wanaopatikana katika hali halisi huathiri kwa kiasi fulani matarajio ya usawiri wa uhusika. Upo mwelekeo mkubwa wa kuwachunguza wahusika wa kifasihi kwa kuwafungamanisha na binadamu halisi na hata, labda kutokana na athari za mielekeo ya kimaadili, tukitarajia kuwa wahusika hasa wale wakuu watakuwa na maadili fulani. Hata hivyo, tunakubaliana na Milani Kundera (2007) kuwa, wahusika wa kifasihi hawahitaji kupendwa kutokana na maadili yao bali wanachotakiwa kufanywa ni kueleweka. Matendo yanayopatikana katika kazi ya kifasihi huhusishwa na wahusika. Matendo hayo ni nguzo kuu ya dhamira na maudhui yanayoendelezwa katika kazi inayohusika. Kulingana na Njogu na Chimerah (1999:45) wahusika ni sehemu ya fani na ni viumbe wa sanaa wanaobuniwa kutokana na mazingira ya msanii. Mazingira haya yaweza kuwa ya kijiografia, kihistoria, kijamii, kitamaduni au ya kisiasa. Wahusika hujadiliwa kwa namna wanavyoingiliana na maudhui na hili hujitokeza kutokana na maneno, tabia na matendo yao, yaani kulingana na hulka yao. Wahusika wa aina yoyote wawe watu au viumbe hurejelea na huakisi sifa na tabia za binadamu katika jamii husika. 30 3.2 UANISHAJI WA WAHUSIKA Kuna njia nyingi za kuwaainisha wahusika katika riwaya. Wahusika wana sifa zinazofungamana na majukumu fulani na tofauti. Hali hii ina maana kuwa wahusika hao watakuwa na sifa zinazofungamana na majukumu yao hayo. Katika kazi hii kwanza tutawaainisha wahusika kupitia njia mbili kuu ambazo ni sifa na nafasi zao katika kazi husika. Baadaye tutaangalia njia nyingine za uainishaji. Kulingana na Njogu na Chimerah (1999) wamewaainisha wahusika wakizingatia kigezo cha sifa kama ifuatavyo, wahusika wa miraba minne na wahusika wa mraba mmoja. Wahusika wa miraba minne wana sifa nyingi. Nyingine zikiwa nzuri na nyingine zikiwa mbaya. Maisha ya wahusika wa aina hii ni mapana katika tajriba na matukio Katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea mhusika Majisifu Majimarefu ni mhusika wa miraba minne. Kwa upande mmoja yeye ni mwovu na kwa upande mwingine ana utu. Kwanza alianza kuwa mwovu lakini baadaye akabadilika na kuwa mwema. Kuhusu wahusika wa mraba mmoja ni kwamba, hawa huwa na sifa moja tu na hawabadiliki. Imani katika Kidagaa Kimemwozea ana nia ya kubadilisha jamii yake kutoka tabaka la chini hadi la juu. Wazo hili analishikilia mpaka mwisho wa hadithi. Kubadilika kwa mhusika mara nyingi hutokana na tabia na matokeo ya tabia hizo. Kwa mujibu wa Wamitila (2002:21-22) ni kwamba amewaainisha wahusika katika makundi mawili akizingatia mawazo ya E. Forster (1927). Makundi haya ni wahusika bapa na wahusika duara. Wahusika duara wanapatikana katika riwaya nyingi za Kiswahili za kisasa. Hawa ni wahusika wanaokaribiana kwa kiasi kikubwa na binadamu wakawaida. Msingi mkuu wa kuwabaini wahusika hawa ni uwezo wao wa kuweza kutustukiza au kutushangaza. Uduara wa wahusika umo kwenye mabadiliko yanayowajia. Mabadiliko haya yaweza kuwa ya kitabia, kimawazo, kijamii, kiukuaji na kadhalika. Matendo na maisha yao yanaongozwa na hali halisi za 31 maisha. Wanajibainisha kwa mapana na marefu yao kihisia na kimatendo. Hawa ndio wahusika wanaovutia zaidi kwa sababu wanaisukuma na kuisongeza mbele riwaya. Kwa mfano, ukimtazama Imani katika Kidagaa Kimemwozea, Utaona kwamba riwaya inapoanza, hana nguvu za kimwili za kuweza kukabiliana na mateso yanayompata. Lakini, polepole anabadilisha nia mara tu anapokutana na Amani karibu na Ziwa Mawewa. Anapevuka kiurazini na kuweza kukabiliana na mfumo wa uzalishaji mali unaomnyanyasa. Kuhusu wahusika bapa ni kwamba hawa hutumiwa na mwandishi kusimamia wazo fulani. Yaani, tangu mwazo hadi mwisho wa hadithi, wahusika hawa wamebuniwa kuzingatia na kutenda matendo yanayoona na sifa walizopewa. Hawabadiliki hata hali za maisha zinapobadilika. Mwandishi anawaelekeza kwa lengo maalumu, hasa kuhusu maadili fulani ya kijamii. Wahusika bapa huwa na sifa za wahusika wa mraba mmoja. Wahusika bapa huwa ni wa aina mbili, wahusika bapa sugu na wahusika bapa vielelezo. Bapa sugu wanajulikana kutokana na maelezo ya msanii. Huwa sugu katika hali zote za maingiliano na wengine na sifa zao au jinsi wanavyoelezwa na mwandishi. Wahusika vielelezo hawabadiliki na hupewa majina ambayo yanaafikiana na matendo na tabia zao. Majina ya wahusika hawa huwa kama kielekezi na kifupisho cha wasifu wao. Kwa kuzingatia mawazo ya E. Forster (1927), Njogu na Chimerah (1999) wameongezea wahusika shinda. Hawa wako baina ya wahusika duara na bapa. Wanategemea wahusika wa aina zote mbili, na wanapelekwa mbele na tabia za hao wengine. Nafasi anayoishika mhusika katika kazi ya kisasihi ni kigezo kingine ambacho tutatumia katika kuwaainisha wahusika. Kulingana na Wamitila (2002:23) kuna wahusika ambao huchukua nafasi kuu au wanayoitawala kazi kifasihi kuanzia mwanzo hadi. Hawa ni wahusika wakuu ambao husheheni hadithi nzima. Matendo na migogoro ya hadithi nzima huwahusu. Kuna wengine ambao wanakuwa kama wasaidizi wa wahusika hao wakuu au hutumiwa kama wajenzi wa maudhui mbalimbali. Hawa ni wahusika wasaidizi na wajenzi. 32 Wahusika wasaidizi huhusiana kwa karibu sana na wahusika wakuu na hutumiwa na mwandishi kumfafanua zaidi mhusika mkuu. Sifa za mhusika mkuu hubainishwa wazi kupitia maingiliano baina yake na wahusika wasaidizi. Wahusika wajenzi hujenga wahusika wakuu na hujenga wahusika wasaidizi kwa hivyo kukamilisha dhamira na maudhui ya mwandishi katika riwaya. Kigezo hiki ndicho tutakachotumia kuwasawiri wahusika katika Kidagaa Kimemwozea. Maelezo kamili yanapatikana katika sura ya nne. Ni muhimu wahusika wazingatie sifa walizopewa na mwandishi kwa sababu sifa hizi zitakuwa hazina maana endapo hazikuungwa mkono na matendo ya wahusika hao. 3.3 NJIA NYINGINE ZA KUWASAWIRI WAHUSIKA Uchunguzi wa historia na maendeleo ya fasihi unadhihirishwa kwa kuwa wahusika wa kifasihi hubadilika kadrii wakati unavyoendelea. Wahusika wanaopatikana katika kazi za kifasihi za miaka ya zamani wanatofautiana kwa kiasi kikubwa na wahusika wanaopatikana katika kazi za fasihi za miaka ya baadaye. Mlacha na Madumulla (1991: 20-24) wanabainisha aina nne kuu za wahusika, mhusika mkwezwa, mhusika wa kihalisi, mhusika wa kisasa na mhusika wa kidhanaishi. Njogu na Chimerah Ufundishaji wa Nadharia (1999:40-44) wanarejelea wahusika wanaozungumziwa na Madumulla. Wamitila (2008: 382-392) amegawanya wahusika katika makundi manne. Mhusika wa jadi, mhusika wa kimuundo au kimtindo, mhusika wa kihalisi na mhusika wa kisasa. 3.3.1 MHUSIKA WA KIJADI Dhana ya kijadi inakwenda na suala la wakati na hasa wakati wa zamani.Mhusika wa aina hii basi ni anayeweza kuelezwa kama mhusika wa zamani. Mtindo huu wa kusawiri wahusika umetumiwa na baadhi ya wanariwaya ingawaje haujatumika katika riwaya hii. 33 3.3.2 MHUSIKA WA KIMUUNDO NA KIMTINDO Mhusika wa kimuundo na kimtindo huainishwa kuhusiana na wahusika wanaorejelewa. Mawazo ya wana muundo kama Vladimir (1999) ni ya kimsingi katika kuwainisha wahusika wa aina hii. Mawazo yake yameendelezwa na wana –Umuundo wa baadaye kama Greimas na wengineo. Kulingana na Wamitila (2008) wahusika wa aina hii wameainishwa kama ifuatavyo: i. Mhusika wa kiuamilifu ambaye anabainishwa kwa kuwa na sifa za aina moja ambazo kimsingi zinapaniwa kumfanya mhusika huyo kuwa chombo cha mwandishi ili kutimiza lengo fulani. Pia anaweza kubainishwa kwa kuangalia nafasi yake kiutendaji, uamilifu wa aina hii unahusishwa na miundo ya kilinganuzi inayopatikana katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. Wahusika kama Amani, Imani, Madhubuti wanapewa uamilifu ambao uafumbatwa na mbinu ya majazi inayotumiwa katika majina yao. ii. Mhusika wa kiishara anatumiwa kiishara, yaani ni sehemu ya uashiriaji katika kazi ya kifashi. Mhusika kama Amani katika Kidagaa Kimemwozea ni ishara ya mabadiliko katika jamii ambayo haiwezi kuuliwa na harakati za utawala mbaya wakuyazuia mabadiliko yenyewe. Ndiye aliyeongoza katika uchunguzi wa nyendo za Nasaba Bora wakiwa na Majisifu kisha wakagundua matendo yake maovu. Kisa cha fahali kumeza nguo (uk.8) ni ishara ya Nasaba Bora aliyokuwa akitafuna ardhi na mali za raia wake bila huruma na kuwaacha maskini.Usimulizi ya mto Kiberenge na maji yake kutonywewa na wakazi wa maeneo yake (uk.3-4) ni ishara kuwa wakati hao huafikiana na maswala fulani bila utafiti au uchunguzi wowote. iii. Wahusika wa kinjozi ni wanao husishwa na fantasia. Hupatikana katika ulimwengu wa ajabu. 3.3.3 MHUSIKA WA KIHALISI Msingi mkuu katika uainishaji wa wahusika wa aina hii ni kanuni ya maisha halisi, kwa kutegemea kanuni ya ushabihi kweli. Mhusika wa kihalisia ana sifa nyingi zinazohusishwa na 34 binadamu katika maisha ya kila siku. Kulingana na Wamitila (2008) : 382-392 tapo hili lina wahusika wa aina tatu, mhusika wa kimapinduzi, mhusika wa kisaikolojia na mhusika wa kidhanaishi. i. Mhusika wa mapinduzi ana sifa zote zinazohusishwa na mtu anayeweza kupatikana katika maisha halisi.Mhusika huyu anasukumwa na kuchochewa na nia ya kutaka kubadilisha jamii yake. Wahusika kama vile Amani, Imani, Madhubuti, Matuko Weye ni mifano mizuri, wanasukumwa na nia a kutaka kuyabadilisha maisha katika jamii yao ambayo inaongozwa na viongozi walafi. Viongozi wao wametiwa shemere na mfumo wa ubepari unaowatia upofu wakuona hali ya wanyonge walio wengi na badala yake kujali kuhusu tabaka la wachache wenye mtaji. ii. Mhusika wa kisaikolojia anaonyeshwa kwa undani zaidi na labda hata misukumo yakisaikolojia yamatendo yake kuonyeshwa kwa njia bayana. Mashaka katika Kidagaa Kimemwozea ni mhusika wakisaikolojia kulingana na yale anayopitia. iii. Mhusika wa kidhanaishi anaakisi sifa kadha zinazohusishwa na falsafa ya udhanaishi ambayo msingi wake ni kudadisi ukweli, furaha na hali ya kuweko maishani (Madumula na Mlacha 1991:23) anamwangalia mhusika huyu kama wa kisasa. Lakini katika kazi hii tunamwagalia kama mhusika wa kihalisi kwa kuwa ana sifa zote za mhusika aliyetawaliwa na kanuni za ushabihikweli. . 3.3.4 MHUSIKA WA KISASA Ni ambaye ana sifa zinazohusishwa na riwaya zinazoandikwa kwenye misingi ya falsafa ya usasa ambayo kwa kufuata mawazo ya udenguzi na baada usasa inaelekea kuitatiza dhana nzima ya mhusika huyo kama binadamu wa kawaida. Katika aina hii moja tunaweza kujumlisha aina kadha za wahusika kama mhusika jumui, mhusika wa kimwingiliano matini na mhusika batili. Mhusika wa kimwingiliano matini anaitwa hivyo kwa kuwa anahusiana na mhusika anayepatikana katika matini iliyotangulia na Mhusika batili hana sifa bayana za utunafsi kama 35 mhusika bali anadhihirishwa kiutendaji katika kazi za matini fulani. Ni mhusika anayeweza kutumiwa kusimamia mtu mwingine. Wafula na Njogu (2007:107) wakizingatia mawazo ya Gustav Jung wanasema kwamba mhusika anaweza angaliwa kama mtu binafsi na maisha yake. Waliorodhesha wahusika kama jaribosi au nguli, kivuli na wengineo. Nguli aghalabu huwa mhusika mkuu mbaye husafiri kwa sababu Fulani. Mara nyingi safari hii huanzia utotoni hadi anapofikia utu uzima. Wakati mwingine hii inaweza kuwa safari ya kikweli ambapo nguli anajizatiti kukisaka kitu au kujisaka mwenyewe.Wahusika kama vile Amani na Imani katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea, wanaandaa safari ya aina hii. Amani alikuwa akienda Sokomoko kumsaka mwizi wa mswada wake wa kitabu cha Kidagaa Kimemwozea, kujaribu kufumbua siri ya kumwokoa amu yake aliyefungwa bila hatia na kukutana na hasimu aliyechangia kuharibika kwa maisha yake. Imani naye anasafiri baada ya kuharibikiwa na mambo huko nyumbani kwao. Mkinzani wa nguli hupambana kuiharibu mipango ya nguli kwa kujaribu kumwangamiza. Aghalabu mhusika huyu huwa mzinzi, mlafi na wakati mwingine huwa tajiri kama vile Mtemi Nasaba Bora. Mikinzani anaweza kuchorwa katika taswira ya mauti. Mauti yanapotisha kutokea huwa yanatisha safari na mafanikio yake. Mtemi Nasaba Bora amefanya maovu mengi sana katika jamii yake na mwishowe anaamua kujinyonga. 3.4 MBINU ZA USAWIRI WA WAHUSIKA. Usawiri mzuri wa wahusika unawafanya wasomaji wajitambulishe nao kwa kuhisi wanavyohisi au kuwaza wanavyowaza. Kuna mbinu kadhaa zinazotumika kuwasawiri wahusika ndizo msingi wa uhusika wa kazi ya kifasihi. Kulingana na Wamitila (2006) kuna njia kadha na tofauti katika kuwasawiri wahusika msanii ana uhuru sio tu wa kuwatumia wahusika fulani, bali na kuteua namna ya kuwawasilisha 36 wahusika wenyewe. Kama wasomaji na wahakiki wa fasihi, tutategemea sifa kadha kuwaelewa wahusika kama vile mienendo na tabia zao, maumbile yao, lugha zao, vionjo vyao, kiwango chao cha elimu, jamii yao na kadhalika. Baadhi ya mbinu zinazotumika ni mbinu ya kimaelezi, kimajazi, ulinganuzi, kidrama, kistiari na nyinginezo. Mbinu zinazotumika ni mbinu ya kimaelezi, mwandishi hutumia mbinu hii kuzieleza na mara nyingine hutoa picha ya maneno inayomwelezea mhusika anayehusika. Mwandishi anakua na nafasi ya kubainisha mapenzi au chuki yake dhidi ya wahusika fulani. Mbinu hii haimpi msomaji nafasi ya kushiriki katika kutathmini tabia ya mhusika fulani. Analazimika kuukubali msimamo na kuridhika na maelezo ya mwandishi. Mbinu nyingine ni ya majazi au matumizi ya majina ya watu au mahali yanayosadifu tabia na maana fulani. Mbinu hii imetumika tangu zamani katika fasihi mbalimbali hasa kwa kuwa majina katika jamii nyingi huwa na maana. Hii inaweza kuelezea kama njia sahihi na nyepesi sana ya uhusika. Waandishi wa kazi za kifasihi huweza kuyatumia majina ya wahusika ambayo huakisi mandhari yao, wasifu wao, tabia zao, itikadi zao, vionjo vyao na kadhalika. Uchunguzi wa majina ya wahusika lazima uhusishwe na msuko, mbinu za utunzi, ucheshi, dhamira au maudhui, itikadi au motifu katika kazi inayohusika. Mbinu ya majazi imetumika kwa mapana na marefu katika riwaya hii. Mwalimu Majisifu Majimarefu. Alisifika kwa usanii wa mashairi nyimbo za taarabu na utunzi wa riwaya iitwayo Kidagaa Kimemwozea. Hii ndio ilikuza sifa zake na akatukuka hadi nchi za nje. Neno Imani lina maana mbili, itikadi ya kitu, kuwa mwema, mpole na huruma. Maana zote hizo zinasadifu tabia za mhusika huyu kama zilivyoonyeshwa katika riwaya. 37 Amani maana yake ni utulivu yaani hali isiyokuwa na vurugu. Jina hilo alilopewa linaonekana kushabihiana na matendo yake. Madhubuti linamaanisha hali ya uimara au nguvu. Mhusika huyu ni kijana bado, ni madhubuti katika malengo yake ya kupinga sera mbaya za uongozi. Kuna majazi ya majina ya mahali kama vile, Sokomoko, Songoa, Baraka, Ulitima na mengineo. Sokomoko ni hali ya utatanishi, fujo au ghasia. Sehemu hii ya Mtemi Nasaba Bora iliingia hali ya utatanishi baada ya ukweli kuhusu Nasaba Bora kujulikana. Songoa ni kama kukamua kitu kwa njia ya kusokota kama vile kunyonga shingo ya kuku. Songoa ukiwa mji mkuu wa Tomoko huonyesha kuwa wananchi walinyanyaswa vibaya. Wahusika watatu walifungwa jela wakatumikia vifungo bila hatia yeyote. Hapa uhuru wao na haki zao zilidhibitiwa,ni sawa uhai unavyotolewa kwa kiumbe. Waliofungwa bila hatia ni Yusufu Hamadi, Amani na DJ Bob. DJ Bob angefungwa miaka minane ni vile alitoroka Sokomoko. Baraka, jina hili linaibua mbinu mbili sawia. Ni majazi na ni kinaya wakati huo huo. Hivyo kuna mbinu mseto. . Baraka ni neema au rehema. Kijiji hiki kilipata neema ya kutoa vijana bora sana kama Chwechwe Makweche mchezaji hodari mno aliyefunga mabao na kuiletea ushindi nchi yake kama kinaya, wahusika kama Imani walifuatwa na balaa badala ya baraka. Mama yao aliuawa kikatili na shamba lao likatwaliwa na Mtemi. Ulitima, kwa maana ya umaskini au ukata. Amani alitoka sehemu yenye ukata. Hali yake ilikuwa ya mtu hohehahe. Mbinu ya ulinganuzi ni njia moja ya jadi ambayo inatumiwa kuonyesha tofauti kati ya vitu viwili na kuviweka vitu hivyo katika muktadha sawa ,kwa njia hii ikiwa pana tofauti kati ya vitu hivyo itajitokeza kwa njia iliyo bayana zaidi. Kazi nyingi zilizoandikwa kwenye misingi ya kimaadili au zenye mwelekeo huo, hutegemea sana mbinu hii kuonyesha tofauti kati ya nguli na hasidi. Katika Kidagaa Kimemwozea kuna wahusika wema na wabaya katika kiasi kikubwa jaala 38 ya wahusika katika riwaya hii imefumbatwa na majina yake kiasi kwamba hatima ya wahusika wenyewe imeamuliwa hata kabla ya wahusika kutenda lolote. Mbinu ya kidrama ni ya usawiri wa wahusika ya kuwaonyesha wakitenda matendo na kuzungumza na kuwaacha wasomaji wawaone na kuzichanganua tabia zao kutokana na matendo au mazungumuzo yao. Kuna mazungumzo yanayotokea baina ya Mwalimu Majisifu na bibi yake Dora nyumbani kwao (uk 44-45). Kupitia mazungumzo yao tunapata ujumbe ufuatao; tabia ya ulevi ya Mwalimu Majisifu, hulka ya utukanifu ya Mwalimu Majisifu, tabia ya maringo ya Mwalimu Majisifu, mtindo wa Mwalimu Majisifu wa kuiba makala za watu kuyachapisha kama yake, dharau ya mwalimu majisifu kwa wanawake, bidii ya Bi. Dora nyumbani kwake, hamu ya Dora kumrudisha kijakazi wake, Imani na shida ya watoto walemavu wa jamii hii. Mazungumzo mengine ni baina ya; Majisifu na mpwa wake Mashaka (uk 47-48), Amani na Wauguzi (76-77), Amani na Mtemi Nasaba (149), Amani na Imani ukingoni mwa ziwa Mawewa( uk.61) na Nasaba Bora na Bi. Zuhura uk (104-105) Mbinu ya kisitiari ni ulinganishi wa moja kwa moja ambao hautambulishwi na matumizi ya maneno ‘kama’ mithili ya, mfano wa na kadhalika. Maneno hutumiwa nje ya maana yake ya kawaida. Mbinu hii inaweza kutumiwa katika usawiri na uendelezaji wa wahusika kwa njia kadha. Katika Kidagaa Kimemwozea. Mbinu hii inajidhihirisha pale ambapo, Mtemi anaondoka baada ya kuhakikisha Amani na Imani wamewekwa mahabusu korokoroni. “…mara tu alipoondoka, mahabusu wale wawili wakaanza kufanyiwa kazi.” Neno kazi hapa limetumiwa kiistiari, halimaanishi kazi ya kawaida maana yake ni ‘mateso’. “…. vita vikesha na mishale kurudishiwa alani” (uk 16) maanake vita vilikwisha na silaha zikawekwa mbali.“nilikuwa nimekwenda ibada kaka” (uk 93) ibada hapa inasimamia ulevi.“nilidhani nimemwoa mke kumbe jamvi la wageni, kila atakaye hulalia.” (Uk 134) Kumbe ni Malaya ambaye huzini na kila mtu na kadhalika. 39 3.5 KIMALIZIO Katika sura ya tatu tumeshughulikia mambo manne muhimu yanayowahusu wahusika. Tumefafanua dhana ya mhusika, baadhi ya mbinu zinazotumiwa kuwasawiri wahusika, njia kadhaa za kuchanganua wahusika na suala la wahusika na maendeleo ya fasihi. Tumegundua kwamba wahusika ni watu au vitu ambavyo waandishi hutumia ili kuibua dhamira na maudhui.Bila wahusika kazi yoyote yafasihi haiwezi kujitosheleza vizuri. Suala la kuainisha wahusika ni tata kwa sababu ni vigumu kutoa kauli ya kijumla kuwa wahusika wote wanaopatikana katika kipindi fulani ni wa aina fulani tu au kuwa changamano zaidi kadiri wakati unavyoendelea. Fasihi pia huwa na vighairi na si ajabu kuwaona wahusika changamano katika kipindi cha baadaye. 40 SURA YA NNE WAHUSIKA KATIKA KIDAGAA KIMEMWOZEA 4.1WAHUSIKA WAKUU 4.1.1 UTANGULIZI Njogu na Chimerah (1999:41) wanasema kuwa wahusika wakuu ndio nguzo za riwaya na wanaosheheni riwaya nzima. Huwa na dhima ya kuisukuma riwaya mbele kwa sababu migogoro na matendo yote muhimu inawahusu. Dhamira kuu ya mwandishi hujitokeza kupitia kwao. Pia msimamo wa mwandishi kuhusu dhamira, matukio na vitushi vya hadithi hujibainisha kupitia kwa matendo yao. Mwingiliano wao na wahusika wengine ndio mbinu ya kufafanua dhamira kuu. Katika Kidaga Kimemwozea matukio muhimu yanawazunguka Mtemi Nasaba Bora na Amani. Tutafafanua jinsi walivyosawiriwa na pia umuhimu wao katika riwaya nzima. 4.1.2 MTEMI NASABA BORA. Ni mmoja kati ya wahusika wakuu katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. Ni mtemi wa Sokomoko katika nchi ya Tomoko. Alipewa cheo kwa kupendelewa na Mudir wa wilaya kwa kuwa walikuwa wa ukoo mmoja. Ni mume wake Bi Zuhura na baba wa Madhubuti na Mashaka ana sifa nyingi zinazomtambulisha. Awali kabisa, yeye ni mnyakuzi, Anatua mali ya watu kwa ukatili na hila. Aliwapangia mauti Chichiri Hamadi na mjane wa mwinyi Hatibu yaani mama Imani. Alihofu upinzani kutoka kwa Yusufu, mwanawe Chichiri Hamadi na akamsingizia kuwa muuaji wa babake na hivyo kuisha kumfunga gerezani bila hatia. Masaibu ya hawa watu yalimpa fursa ya kunyakua mali yao pasipo pingamizi. Unyakuzi unamletea sifa mbaya katika jamii yake na kusababisha upinzani mkali dhidi yake. 41 Mtemi ni mkatili mipango ya mauaji na mateso aliyopanga inadhihirisha kauli hii. Alipomvumania Amani katika chumba chake cha kulala wakiwa na Bi Zuhura aliweza kumpiga kwa bato la bunduki kisha kumchoma kisu chenye makali kuwili. Baadaye alienda kumtupa kando ya mto kwa kudhani amemuua. Pia alijua wazi asili ya mtoto Uhuru, alivyomtupa na hakutaka kumwauni badala yake aliuweka mzigo wa kumlea kwa mfanyi kazi wake Amani. Ukatili wake unadhirika pia pale alipomfunga paka aliyekula kitoweo chake katika gari lake na kumkokota barabarani. Alimkokota kwa gari hadi akafa na kumung’unyuka nyama yote ya mwili. (uk. 23). Pamoja na haya, yeye pia hana utu, kwa mfano, wakati alipotoka kwenye sherehe ya sikukuu ya Wazalendo, alimkuta mjamzito mmoja akijifungua peke yake na hakutoa msaada wowote. Hata alimkataza Bi. Zuhura amsaidie. Alimtaliki mke wake mwaminifu bila huruma. Hakumpa nafasi ya kujitetea. Jibwa lake jimmy lilipomshambulia Bob DJ, Mtemi hakujali, aliona kuwa ni halali yake badala ya kumsaidia. Kitendo cha kumpiga Amani hadi alipozimia na baadaye kumchoma kisu tumboni ni dhihirisho la kukosa utu. Hakumhurumia mtoto Uhuru alipotekelezwa mlangoni mwa mchungaji wake. Mtemi anadhihirika kama mhusika asiyeheshimu taasisi ya ndoa. Japo ana bibi mpole anayemheshimu, yeye humla kivuli na kuendelea kukutana na mahawara wake akisingizia kuwa aenda kutatua matatizo au migororo ya “mashamba” huko nje. Mtoto Uhuru ni matokeo ya kuzini kwake na Lowela binti Maozi. Uzinifu wake unamharibia sifa mbali na kufanya bibi yake atatizike na kuona anapuuzwa. Mwishowe, ukware, japo sio moja kwa moja, unamfanya Mtemi amtaliki mkewe kwa kumshuku kutokuwa mwaminifu. 42 Mtemi ni mtu bahili alikuwa na mamlaka makubwa na alimiliki pesa nyingi lakini hakutaka kutumia, fedha kulitengeneza gari lake. Ni kutokana na ubahili huu ndiposa alishindwa kabisa kulitengenezwa na kurirekebisha na mara kwa mara lilizidi lisukumwe ndipo liwake (uk 50). Alishindwa pia kutunza makochi ya nyumba yake. Amani na Imani walipoingia nyumba yake kwa mara ya kwanza waligundua yalikuwa makuu kuu. “ Walikakaa kwa makochi makongwe……....Yaliyokatikakatika na kujaa vumbi tele.(uk23) paka aliyekula nyama yake ya nguruwe alimwadhibu vikali sana. Ni mtu mpenda sifa kwa sababu taasisi nyingi katika Sokomoko zilipewa jina la Mtemi. Mifano ni uwanja wa Nasaba Bora, Zahanati ya Nasaba Bora, shule ya upili ya Nasaba Bora, shule ya msingi ya Nasaba Bora, daraja la Nasaba Bora na kadhalika. Alipenda sana habari zinazomhusu ziandikwe kwenye magazeti ili kujipatia sifa ingawa hakustahili kusifiwa. Siku moja baada ya sherehe za siku kuu ya wazalendo, Mtemi alitambua kuwa gazeti la Tomoko leo halikuwa na picha na habari kumhusu, jambo hili lilimghabisha na kumfanya alikunje na kulitupa kwenye kapu la taka. (uk.87-88). Kwa hivyo alipenda sana sifa na kutaka kuogopwa na kuabudiwa kama Mungu. Mtemi ni mfisadi, kwanza alikuwa akitumia madaraka yake vibaya mno. Alikuwa mla na mtoa rushwa. Alihonga majaji, polisi na wengineo ili Yusufu afungwe maisha. Ingawa Yusufu hakuwa na hatia. (uk 13) Aidha alihonga maafisa wa jeshi ili mwanawe Madhubuti apate kazi bila kufanya mahojiano. Alikuwa ni dikteta na akiamuru jambo hakuna aliyekuwa akimpinga “neno lake lilikuwa kama sheria” Watu walilazimishwa kuhudhuria sherehe ingawa hawakuelewa hotuba yake kwa maana alikuwa akitumia lugha ya Kiingereza. Askari waliazimia kumwadhibu Imani kwa kukataa kuhudhuria sherehe hizo. Aliamuru askari wamtoe mama Imani shambani mwake kinyume cha 43 sheria. Pia Amani na Imani walipokuwa mahabusu alitoa amri wapigwe. Alikaripia watu vibaya na maneno yake makali. Kwa ukali wake akiamua kitu, ilibidi mkewe Zuhura afuate bila pingamizi. Mtemi hakutunza mazingirra na hata hakuona umuhimu wake. Alishindwa kutunza shamba alilonyakua kwa Chichiri Hamadi. Unyakuzi wa shamba lile ulikuwa ni wa kujilikimbiza mali tele na ulidhamiriwa kumfanya achomoze mbele ya watu kama mtu mashuhuri. Mandhari yake yalikuwa si nadhifu yakilinganishwa na mandhari ya wakati wa majununi. Mabomba ya maji yalikauka na ilibidi ng’ombe wapelekwe mtoni. Wakati wa Majununi mabomba na mifereji ya maji ilikuwa na maji safi ya kunywewa na ngombe. Alikuwa na madharau yasiyo kifani. Amani, DJ na Imani walipoenda kwake kutafuta kazi aliwabeza ifuatavyo: “Mheshimiwa mtemi alipoyasikia majibwa yale yanabweka, akatazama upande wa langoni, kawaona vijana watatu, wavulana wawili namsichana mmoja. Walikuwa ni Amani, Imani na DJ kawaangalia kwa bezo na dharau, uso umepiga mapeto kipajani. Walipokuwa karibu naye akauliza, “mwataka nini?” Pia wakati alipowahutubia watu kwenye sherehe za Wazalendo aliwaona kama vinyangarika. Mtemi ni mbinafsi, hii ilidhihirika wakati mwanawe madhubuti alipopata fursa ya kuenda kusomea Urusi, alilazimisha watu kumtolea mchango wa pesa za kumsomesha huko. Yeye alikuwa na pesa za kutosha lakini alitaka tu kunyanyasa wanasokomoko. Pia pale ambapo alinyakuwa mali ya watu na kumfanya ajilimbikize mali tele yeye binafsi huku watu wengine wakiteseka. Kukataa kuwasaidia watu katika gari lake haja inapotokea kunamdokeza kuwa mtu mbinafsi mno. Mtemi alijutia maisha yake baada ya kugundua uovu wote alioutenda kwa watu mbalimbali hasa kwa kuwapokonya wanyonge haki zao, Mwishoni alitubu na kujiona kuwa hafai kuishi. Alimwambia Amani, “Nipige risasi nife” (uk 147). Mwishowe alijinyonga kwenye mti wa mkuyu. 44 “…. walipokikuta kimba cha mtu kimeoza na kuozeana kikininginia kama bembea mkuyuni, (uk 159) Mtemi ni kielelezo cha uongozi mbaya anawakilisha viongozi wa Kiafrika ambao wanajisahau baada ya kuwa viongozi. Ni kielelezo cha viongozi Waafrika waliorithi maovu ya wakoloni na kuyatenda kwa Waafrika wenzao. Uongozi wao ni mbaya zaidi hata kuliko wa wakoloni. Ametumiwa kuangazia ukweli kuwa viongozi kama hawa wanastahili kung’olewa madarakani haraka iwezekanavyo. Anaonyesha njia ambazo viongozi waovu wanazotumia kulimbikizia mali. Tamaa hii ya kujilimbikizia mali ndio inaletea watu balaa. 4.1.3 AMANI Amani ndiye mhusika mkuu wa pili baada ya Mtemi Nasaba Bora. Yeye ndiye mhusika nguli kulingana na maoni yetu. Ni nguli kwa sababu anatetea masilahi ya wengi, anawakilisha matendo mema na ni shujaa. Huyu ni kijana wa kiume mwenye umri wa miaka ishirini na nne. Ni yatima na alikuwa mkazi wa Ulitima. Alikuwa na matatizo mengi na hivo aliamua kuhama Ulitima na kukimbilia Sokomoko ili kuisaka haki yake kuhusu mswada wake ulioibiwa na pia kutaka kutetea uhuru wa amu yake Yusuf aliyefungwa bila hatia. Alikuwa mjukuu wa Chirchiri Hamadi. Hamadi aliuawa na Mtemi Nasaba Bora ili achukue kasri na shamba lake. Ni mpwa wa Yusuf Hamadi. Amani ni mtu mvumilivu mno. Uvumilivu wake unadhihirika vizuri pale anapotambua kupitia kwa Yusuf amu yake kuwa Mtemi Nasaba Bora ndiye kiini cha matatizo ya jamii yao. Kasha alianzisha uchunguzi wa polepole. Alienda kufanya kazi ya kuchunga ng’ombe ndiposa akapata fursa nzuri ya uchunguzi mpaka alipothibitisha kuwa Mtemi kweli ana hatimiliki ya shamba lao, majununi, na aliichukua hio hatimiliki na zingine. Pia, akiwa katika Chuo Kikuu kabla ya kufungwa, aliweza kusoma kitabu Kidagaa Kimemwozea na ikamjia kuwa ni kitabu kutokana na mswada wake uliokataliwa na kampuni ya uchapishaji. Alianza kufuatilia polepole mpaka alipoishia katika maktaba ya Mwalimu Majisifu na kumfanya aeleze asili ya kitabu hicho. 45 Alitambua kuwa Majisifu aliiba mswada wake na hakuanzisha ugomvi alivumilia tu. Amani alifungwa akiwa katika chuo kikuu kwa kusingiziwa uchochezi. Baada ya kupata mali yao aliamua kurudi chuoni kwa kuwa hakuwa amekamilisha elimu yake. Hakuwa na haraka ya kumuoa Imani sahibu wake wa siku nyingi. Ni mtu mwenye huruma. Alimhurumia sana mtoto Uhuru ndiyo maana alikubali kumlea baada ya kutekelezwa mlangoni kwenye kibanda chake. Pia alimpatia shati BobDJ baada ya kaptula kutafunwa na fahali (uk. 8) Ni mfanyikazi shupavu na mwenye bidii. Alitia bidii kwa kazi yake ya kukama ngombe na akathaminiwa na Bi, Zuhura. Amani ni mtu asiye na tamaa ya mali na mamlaka na tena ni mkarimu alipopata shamba la Majununi (ekari 270) baada ya kumshinda Mtemi Nasaba hakufurahi na kulihidhi peke yake. Alilikatakata vipande vipande na kugawia watu waliomsaidia na pia wahitaji wengine. Pia alipolitwa kasri la Majununi, hakujisifu kwa utajiri na fahari badala yake alilipa Matuko Weye, Mzee aliyepigania malkia wa Uingereza na hakulipwa chochote. Yeye aliendelea kuishi katika kibanda alimokuwa akiishi wakati wa Mtemi Nasaba Bora. Baadaye aliweza kujijengea nyumba yenye vyumba vinne. Amani hakupenda kueleza mambao yake binafsi na kwa hivyo alikuwa msiri mno. Licha ya sahibu yake Imani kumrai amweleze asili yake Amani hakumweleza na alimficha kuhusu usuli wake. Hakumweleza sababu ya kutupa mswada hadi mwishoni kabisa. Aidha, baada ya kufika Sokomoko, Amani anahifadhi siri nyingi, Kwa mfano, hakuonyesha mtu yeyote kuwa: Alimshuku Mtemi kuwa ana hodhi hatimiliki za mashamba ya watu, alimshuku Majisifu kwa kuiba na kuchapisha kazi yake Kidagaa Kimemwozea , alikuwa amesoma hadi chuo kikuu na alikuwa na elimu ya kiwango cha juu. Hata hakumwambia Madhubuti ni mmiliki wa shamba la Majununi na vilivyomo vyote. 46 Ni mwaminifu, yeye alitokea kuwa rafiki mwaminifu kabisa wa Imani. Walitoka naye karibu na ziwa Mawewa hadi Sokomoko halafu walienda kushirikiana wakiwa katika ajira tofauti. Walipendana kusaidiana kama ndugu. Walikaa na Imani chumba kimoja na akamheshimu kama “dada” ingawa hakumjua ndewe wala sikio. Watu wengi waliamini kuwa hao wawili ni ndugu. Amani pia alikuwa rafiki mwaminifu kwa Madhubuti, DJ Bob, Matuko Weye na wengine. Urafiki wake na Madhubuti ulimfanya ahame kutoka kasri la babake hadi katika kibanda cha Amani. Urafiki huo ndio uliopelekea kutambuliwa siri kuu za Mtemi na kwa hivyo kuleta mabadiliko makubwa katika jamii. Urafiki wake na Matuko Weye ulidhibitikia korokoroni walipowekwa na Mtemi. Amani ni mwenye mapenzi ya kweli. Alimpenda Imani kwa dhati. Walivumiliana kwa kila hali; kwa mfano, baada ya kulazimiziwa mtoto wa Lowela aliamua kumchukua akijua kuwa watasaidiana na Imani kumlea. Alimpenda sana mama yake kwa hivyo suala la kushindwa kumzika lilimtia majonzi makuu. Hakuweza kuhudhuria mazishi yake kwa kuwa alikuwa kifungoni. Alifungwa mika mitano bila kosa. Alijitahidi kumtengenezea chapati Bob DJ akiwa hospitalini. Huku ni kujitolea mno kwani alikuwa fukara. Amani anasifa ya usamehevu, alimsamehe Nasaba Bora kwa uovu wote aliomtendea. Pia, alimwombea msamaha wakati Gaddafi alipotaka kumuangamiza. “una bahati kama mtende, kama rafiki yangu Amani asingaliniambia nikuache ungalikuwa marehemu sasa.” (uk. 146). Aidha aliwasamehe wale wanafunzi waliomwonea wivu kisha akafungwa. Alimsamehe mwalimu Majisifu kwa kuiba mswada wake. 47 Ni mtimizaji wa ahadi kwa sababu yale aliyomwahidi DJ Bob aliyatekeleza baada ya kupata mali. Aidha waliahidiana na Imani kuoana na walifunga ndoa baadaye. Amani alileta ukombozi wa Sokomoko baada ya kushirikiana na Madhubuti mtoto wa Mtemi. Madhubuti alikuwa na tumaini kubwa kwake na alimthamini kuliko baba yake. Alikuwa mpiganiaji haki za wanyonge, kwa mfano alipambana ili amu yake Yusufu afunguliwe kutoka jela. Aidha alizuia mashamba ya Nasaba Bora kuuzwa na madalali alipotoa hati miliki halali za wenye mashamba hayo. Amani ni kielelezo cha kizazi kipya ambacho kinafaa kuwa mbegu ya ukombozi na mabadiliko katika jamii. Alitumika kama nyenzo ya kufumbua mafumbo katika riwaya hii. Ni kupitia kwake ndiposa tumeweza kukitegua kitendawili cha Kidagaa Kimemwozea nani na ni kwa nini. Ni kupitia kwake ndio tumetambua kwamba uvumilivu, bidii na ari huzaa matunda mema. Pia, kupitia kwake tumejifunza baadhi ya matatizo yanayowakumba waja na umuhimu wa kuwa mwenye subira ili kuyatatua. Ni kielelezo cha urafiki wa dhati na utu. 4.1.4 KIMALIZIO Tumeona kwamba wahusika hawa wawili wakuu wana sifa nyingi, nyingine zikiwa nzuri na nyingine zikiwa mbaya. Maisha yao ni mapana, katika tajriba na matukio. Mtemi Nasaba Bora aliishi maisha ya kujipenda, kuwadharau na kuwanyanyasa watu lakini hakuwahi pata furaha hata dakika moja ya maisha yake. Mwishowe mambo yanapomwendea mrama anaamua kujinyonga. Amani naye amefanikiwa kukisaka alichonuia.Mafanikio yake hayamfaidi peke yake lakini pamoja na jamii nzima. Watu wa Sokomoko wanafurahia juhudi zake za kuwaletea uhuru wa pili. 48 4.2 WAHUSIKA WASAIDIZI 4.2 .1 UTANGULIZI Katika sura hii tutashughulikia wahusika wadogo kama wanavyojitokeza katika Kidagaa Kimemwozea (2012). Tutachunguza ni vipi wamekuzwa, umuhimu, majukumu na usawiri wao. Tumewagawanya katika matapo mawili kama wahusika wasaidizi na wajenzi. Njogu na Chimerah (1999: 41-42) wanaeleza kuwa, wahusika wasaidizi hutumika ili kumsaidia msomaji amwelewe vyema mhusika mkuu. Ni kupitia kwa maingiliano baina ya mhusika msaidizi na mkuu ndipo tunapata mwanga zaidi kuhusu hulka ya mhusika mkuu. Matapo haya mawili yanategemeana sana. Wahusika wasaidizi pia hutumika katika kukuza baadhi ya maswala katika kazi ya kubuni. Katika kazi hii tumeorodhesha wahusika wasaidizi kama ifuatavyo; Mwalimu Majisifu, Imani, Madhubuti, Mzee Matuko, Mashaka, DJ Bob, Bi Zuhura na Bi Dora. 4.2.2 MWALIMU MAJISIFU MAJIMAREFU Ni nduguye Mtemi Nasaba Bora. Ni mume wa Dora. Alifunza katika shule ya upili ya Nasaba Bora. Majisifu ni mtu aliyependa sifa na pia kujisifu. Bibi yake Dora alipomwita mzembe alikasirika na kujisifu kuwa yeye ni mwandishi mashuhuri. “I am a writer of distinction.” (uk.44) alijiita Shakespeare wa Afrika. Alipotembelewa na mwanafunzi wake Mashaka, alimweleza yafuatayo: “hapana, mimi ndiye mwandishi bora zaidi katika Afrika na miongoni mwa wale bora zaidi ulimwenguni, au sio?” (uk. 48) Haya majisifu yake hayana msingi dhabiti kwa vile ilihidhirika baadaye kuwa alikuwa mwizi wa makala ya mwandishi mwingine. Kwa hivyo hakuwa mbunifu kama alivyodai. Mwalimu Majisifu ni mlevi wa kupindukia. Alilewa mpaka akasahau majukumu yake kama mume na pia kama mwaajiriwa. Alilewa mpaka akavuliwa madaraka. Mara nyingi alipatikana akiwa mlevi hoi, hajifai na wakati mwingine alianguka mitaroni. Alipomtembelea ndugu yake Mtemi siku moja baada ya sherehe za sikukuu ya Wazalendo alikuwa mlevi na shemejiye alipompa chai, Majisifu hakuinywa kwa vile alizoea pombe mpaka hakuwa na hamu ya chai (uk 95). 49 Alipoachana na nduguye baada ya ugomvi kuhusu ulevi, hakuenda shuleni alienda ulevini, pia alikataa chai aliyopika bibi yake Dora, Mashaka alipowatembelea. Sababu ni ile ile, ulevi ulimfanya asitekeleze kazi yake vizuri kama vile kuikimu jamii yake, kufunza shuleni na pia uliishusha heshima yake. Pia, ni mojawapo ya sababu zilizofanya ahasimiane na nduguye, aliposhauriwa apunguze. Aliiba mswada wa Amani wa Kidagaa Kimemwozea kwa hivyo ni mtu mdanganyifu. Hakuandika kitabu kile. Alipopewa mswada wa “Kidagaa Kimemwozea” aliutolesha nakala na akaiweka. Halafu aliurudisha mswada asilia kwa Amani akidai ati ni mbaya na haungeweza kuchapishwa kuwa kitabu. Amani alipata mswada wake uliorudishwa. Hakujua kuwa Majisifu alitoa nakala naye aliusoma na kuutupa katika ziwa Mawewa. Baadaye mwalimu alichukua nakala ya muswada huo na kutuma kwa kampuni nyingine na kuuchapisha kama kazi yake, kumbe sivyo. Hili lilidhihirika wakati alipopewa fursa ya kutoa mhadhara huko Mkokotoni kuhusu hicho kitabu alishindwa kabisa na kuaibika mbele ya umma. Alikuwa mtu asiye na utu kwani alifikiria hata kuwatupa watoto wake mapacha majini kwa sababu walizaliwa viwete. Hakumsaidia Dora mkewe katika ulezi wa watoto punguani na walemavu aliokuwa nao. Alihisi uchungu kwa kupata watoto walemavu na aliwachukia mno. Badala yake alihusudu watu wengine waliokuwa na watoto wazima, wasio na ulemavu wowote. Aliwaita kuwa ni ‘masimbi na mashaza’ yaani mabaki yasiyo na maana. Alimchukia mkewe kwa kumzalia watoto wale na alimlaumu Mungu kwa kupata watoto walemavu na taahira. Aliwachukia watoto wake kabisa na hakuwaona kama binadamu. Majisifu ni mtu mtukanifu. Alikuwa ni karakana ya matusi. Dora alipojaribu kumweleza kuhusu jukumu lake, alimkaripia kwa lugha isiyofaa, “Bloody Bastard” (uk 44). Dora alipomwambia kuwa siri zake zitajulikana, alimkemea na kumwita bwege. (uk 45) alimdhalilisha mkewe na hakumthamini hata kidogo. 50 Ni mkosoaji mkuu, mtu alipoongea lugha isiyofuata kanuni za kisarufi alimkosoa moja kwa moja. Ni mzingativu wa Kiswahili fasaha. Shida ilikuwa kukosoa wengine ilhali alishindwa kukosoa udhaifu wake. Hata hivyo alikuwa msanii na mwimbaji wa taarabu. Baadaye Mwalimu alibadilika na kuwa mwenye huruma. Labda kisa cha kuaibika katika chuo kikuu cha Mkokotoni kilimfanya abadilike na akawa na utu. Alianza kuwaonea watu walioteseka huruma. Kwa mfano, alimwonea Amani huruma na akamtembelea hospitalini. Pia alipotoka hospitalini alimweka katika mji wake na akampa kijakazi wake, Imani kumtunza hadi atakapopata nafuu. Aliwapenda watoto wake na akaanza kuwathamini. Mwalimu Majisifu ndiye asili ya fumbo la Kidagaa Kimewozea. Kupitia kwake tunaelewa matatizo ya waandishi wa vitabu ambayo ni maudhui makuu kitabuni. Maudhui ya ulevi na shida zake yanadhihirika kwake. Na kwamba uraibu wa pombe huleta madhara na kushusha hadhi ya mtu. Anatufanya tutambue kuwa binadamu hukumbwa na matatizo tofauti, baadhi ya kujiletea na mengine ya mazingira. 4.2.3 IMANI Imani ni msichana wa miaka kumi na nne na alikuwa yatima. Ni bintiye Mwinyihatibu Mtembezi na dadao Oscar Kambona (Gaddafi) na Chwechwe Makweche (Horsepower). Alinusurika kifo baada ya nyumba yao kuteketezwa moto na askari wa Nasaba Bora waliotaka kulipora shamba lao. Baada ya hilo aliamua kujitosa ziwani. Alikuwa amekata tamaa na alitaka kukatiza maisha yake kutokana na maovu aliyotendewa. Baada ya kukutana na Amani kisadfa alibatilisha nia yake. 51 Kama Amani, alidhihirika kuwa mvumilivu. Tangu walipokutana ukingoni mwa ziwa Mawewa hata walipokaa Sokomoko. Walipitia katika changamoto tele na wakazikabili kishujaa. Uvumilivu wake ulipata jaribio shadidi hasa alipokuwa kijakazi kwa Mwalimu Majisifu.Mbali na kazi za kawaida za nyumba, alipandikizwa mzigo wa kuwalea watoto wasiojiweza wa familia hiyo wawili wao walikuwa akili punguani na walienda haja ndogo na kubwa palepale na wawili hawangeweza kutembea. Ijapokuwa ni kazi ya kinyaa, Imani aliifanya kwa mapenzi na moyo wake wote mpaka akaishia kupendwa na Dora, mkewe Majisifu, Ama kwa kweli, hapo palikuwa na kujitolea kwingi na kuwa na moyo wa dhati na uvumilivu. Imani ni msichana mwenye bidii. Alifanya kazi yake kwa Majisifu kwa bidii kubwa mpaka Dora na Majisifu walimpenda. Yeye hakuchoshwa na kazi ya kinyaa ya kuwatunza watoto walemavu, kwa hivyo hakukimbia, baada ya muda mfupi kama wafanyi kazi wengine. Aidha, bidii yake ilidhihirika wazi alipohamia kwa Amani kwa muda ili kumtunza mtoto Uhuru. Wakati huo Dora alipata matatizo mengi mpaka akamlilia Imani ili arudi haraka. Pia, bidii hiyo ilidhihirika wakati Mwalimu Majisifu alipodai afunguliwe kutoka katika seli ili aendelee kumsaidia Dora. Kwa hivyo, alikuwa mchapakazi na mwenye idili na ari kazini. Ni msichana mwenye huruma na Imani. Hili lilidhihirika wakati alipokubali kumtunza mtoto Uhuru kana kwamba yeye ndiye mama yake halisi, kumbe sivyo, pia alimhudumia na kumtunza Amani alipokuwa mgonjwa kama kwamba ni mwanawe au nduguye, kumbe sivyo. Amani alipokuwa mgonjwa bila fahamu hospitalini, Imani alimtazama na kumhurumia hata akadondokwa na machozi. Alienda kila siku kumwona hospitalini licha ya kazi tele kwa Mwalimu Majisifu. Aidha alimtembelea DJ Bob hospitalini baada ya kuumwa na mbwa. Aliwapenda walemavu kama watu wengine. Hii iliwafunza watu wengine waliokuwa wabaguzi kama Mwalimu Majisifu. 52 Imani ni mwenye maadili au malezi bora. Aliishi na Amani pamoja wakati wote na hakujiingiza kwenye upotovu wa vijana. Alimtii Dora na kuishi naye vyema kabisa. Uadilifu wake ulichangia kumbadilisha Mwalimu Majisifu mwajiri wake. Alijitokeza kuwa jasiri au shupavu wakati alidhamiria kuishi peke yake nyumbani mwao baada ya kifo cha mama yake na nduguye kutoweka. Pia alimwelezea Majisifu kuhusu wizi wa kitaaluma bila kuhofia. Aidha, alimtaka Amani afanye maamuzi kuhusu kufunga ndoa baina yao baada ya ufanisi wao. Imani ni mwenye hekima. Alimshauri Oscar Kambona aache kumtafuta Mtemi na badala yake arudi Baraka akaishi na Chwechwe Makweche kakaye mcheza mpira na aliyekuwa amevunjika fupa la mguu. Imani ni kiwakilishi cha vijana wa kike waletao mabadiliko chanya katika jamii katika Nyanja mbalimbali. Aidha, ni kielelezo cha vijana wenye maadili ya kuigwa. Ana sifa za huruma, ujasiri, heshima, uzalendo na upendo. Anatusaidia kuelewa usumbufu wa mwanamke katika jamii. Ni kielelezo cha mwenendo wa kusuluhia katika jamii, yaani kuepuka upotovu wa aina yoyote. Pia ni kielelezo cha mapenzi kwa binadamu wengine, pamoja na uvumilivu. Kupitia kwake tunaona kuwa hakuna faida ya kujinyonga ati kwamba umezongwa na kusongwa na matatizo, vumilia na utafute njia za kuyakabili kwa vile zipo. Uvumilivu huzaa matunda mema. Ni kielelezo cha imani ya waadilifu kuwa kazi ni kazi. 4.2.4 MADHUBUTI Madhubuti ni mwanawe Mtemi Nasaba Bora. Alikuwa kifungua mimba. Alikuwa kaka yake Mashaka. Alipelekwa Urusi kwa masomo ya juu. Baada ya masomo alirejea Tomoko. Yeye ni mpiganiaji wa haki za wanyonge na aliupinga vikali unyanyasaji wa baba yake. 53 Alikuwa mwasi, alimwasi babake na akatenda kinyume cha matakwa ya baba mtu. Mfano mzuri wa uasi ni barua aliyomwandikia babake kama angali bado Urusi kumwonya kuwa hakutaka msaada wake uliotokana na njia za upotovu (uk. 87-88). Pili, aliporudi kutoka Urusi alikataa kukaa katika kasri la babake na badala yake alijiunga na Amani kuishi Kibandani. Alipoanza kazi huko Songoa, alianza kufanya uchunguzi wa kutambua visa viovu vya babake. Alikuwa adui mkubwa wa babake hata babake akakula yamini kuwa hakutaka amwite baba tena. Walakini lazima tuelewe kuwa uasi wa Madhubuti kwa babake uliongozwa na uadilifu ilivyokuwa babake alitawaliwa na hulka ya upotovu. Kwa hivyo uasi wa Madhubuti kwa babake ni nafuu kwa jamii nzima. Madhubuti ni kijana aliyesuluhia maishani. Hakujiruhusu kupotoka katika mwenendo wake. Ijapokuwa hakuwa mwerevu sana darasani lakini alijikakamua akapita mitihani yake yote, hali iliyomwongoza kupata nafasi ya kuenda masomoni Urusi. Alipokuwa huko,alimwandikia babake barua dhidi ya kumhusisha na mienendo mipotovu maishani. Aliporudi nyumbani alihama kutoka nyumba yao aliyohisi ina upotovu na kuhamia kwenye kibanda cha Amani alichohisi kinamfaa. Aidha, akiwa Songoa alianzisha uchunguzi kufumbua fumbo la upotovu wa babake. Na baada ya Amani kumpa shamba la ekari hamsini akalikata vipande na kugawia watu wengine waliohitaji. Ni kijana mkakamavu. Alikataa katakata mipango ya babake ya kumtafutia ajira kwa njia ya ufisadi akiwa bado huko Urusi, alipofika Tomoko alishikilia uzi ule ule, aliishia kupata kazi ya uhasibu kupitia kwa juhudi zake za halali. Alipohamia kwa kibanda cha Amani, wazazi wake walimkemea lakini hakubadili nia. Ukakamavu wake ulidhihirika pia katika kila fani ya maisha bila kugeuka. Alichukia unyanyasaji na ukandamizaji wa baba yake hadi akajiita Madhubuti Zuhura. Uchunguzi wake ndio uliosimamisha mali iliyoporwa na Mtemi kutwaliwa na madalali. 54 Madhubuti ni mzindushi. Aliungana na Amani na kuanza kuelemisha umma. Alimwazima Amani vitabu vya kifasihi ili kumpa mwanga zaidi. Alikuwa wa falsafa nzuri za kimapinduzi kutokana na vitabu alivyosoma. Hivi vitabu vya fasihi vilivyoandikwa na wasanii mbali mbali. Madhubuti alikuwa tayari kubatilisha nasaba yake. Aliamua kupinga dhuluma za baba yake ingawa zilimfaidisha yeye. Alieleza hadharani nia ya kuuangamiza ukoo wake. Pia alitaka watu waue utabaka. Hakuthamini maisha bora ya wazazi wake kwenye kasri. Hakulegeza kamba hadi uhuru ulipopatikana. Aliwapigania wananchi haki zao za mashamba yaliyokuwa yamepokonywa na baba yake baada ya mahakama kutaka kuyanadi yakithaniwa ni mali ya Nasaba Bora. Ni kupitia kwake tunapata kusisitiziwa upotovu na upotevu wa Mtemi, na tunajiuliza hivi “ikiwa mwanawe mwenyewe anamwasi sembuse wanajamii wengine?” Pamoja na Amani waliwakilisha ukakamavu wa vijana chipukizi katika kuleta mabadiliko katika jamii. Ni mbegu ya ukombozi katika jamii kutoka katika minyororo ya kikoloni na unyanyasaji wa Nasaba Bora. Alishirikiana na Amani na wakafaulu kuleta uhuru wa pili kwa watu wa Sokomoko. Ni kielelezo cha mwenendo wa usawa maishani. Ni kielelezo cha ufanisi unaotokana na kujitegemea na mtu binafsi. Aidha, ni kielelezo cha elimu bora inayomfanya mhusika ajitambue na kubadilika. 4.2.5 MZEE MATUKO WEYE Alikuwa mzee mwehu aliye na akili razini. Katika wendawazimu wake aliongea mambo mazito yakiwemo maovu ya utawala wa Mtemi Nasaba Bora. Alienda kupigana huko Burma akiwa na akili timamu lakini baada ya kurudi mambo yalimwendea kombo na wala serikali ya Tomoko haikumjali. Hakuwa na umiliki wa kitu chochote. 55 Baadhi ya vitendo vyake ni vya kibinadamu. Alipenda kupiga kwata na kusema “mark time, about turn, left-right,” na kwamba alipita akitoa simulizi za vituko na visa vya vitani na kadhalika. Alipanda jukwaani baada ya hotuba ya Mtemi wakati wa sherehe za sikukuu ya Wazalendo. Kitendo cha kunyakua maikrofoni baada ya Mtemi kuhutubu na kumnyambua Mtemi yamkini ni cha kiwendawazimu. Jukwaani alibainisha uozo wa utawala wa Mtemi Nasaba wa kuwapokonya wananchi mashamba, mali, mabinti na hata wake. Alitaka kuwaonyesha wananchi kuwa bado hawajajitawala. Aliwekwa mahubusu na serikali ya Mtemi baada ya kuzungumza ukweli huo. Ni mtu damisi. Alipenda kufanya mambo ya kuchekesha watu. Mathalani, kule kuita korokoro ikulu yake ni jambo la kuchekesha. Kule kunyakua maikrofoni pia ni jambo la kuchekesha. Alipotambua kwamba Amani na Imani wako rumande pamoja naye alimwambia Amani kwamba anaweza kumfanya kuwa waziri wa ufisadi na magendo akitaka. Hili lilimfanya Amani atake kucheka licha ya balaa yake. Yeye kwa kiasi fulani ni mneni. Ana uwezo na ufundi wa kusema maneno mengi. Kila tunapomkuta anasema. Na nyingi ya hoja alizotoa zina maana, hata askari walipomwachilia na kumwambia aondoke korokoroni, alisema hawezi kuondoka ila waachilie vijana wawili, Amani na Imani wasio na hatia. Alitambua haki za Amani na Imani kutiwa seli bila hatia. Alipewa kasri na Amani baada ya uhuru wa pili kwa kuwa Amani alitambua mchango wake wa kihistoria wa kumpigania mwingereza na kuachwa bila kukumbukwa na serikali ya kikoloni. Matuko Weye ni kielelezo cha namna uongozi ulivyoshindwa kuwaruzuku wahudumu wa zama zile. Ni vyema kutambua raia walioathirika katika mapambano. Ni nyenzo ya kufichua udhaifu wa viongozi na matatizo mengine katika jamii. Uovu wa viongozi ni dhahiri mno hata kwa wasio na akili razini huutambua. Alitumiwa kukamilisha jumuiya. Katika riwaya kuna wabaya, wazuri, wenye elimu, wasio elimu, matajiri, maskini, wenye akili nzuri, wenye kichaa na wengineo. 56 4.2.6 MASHAKA Alikuwa bintiye Mtemi Nasaba Bora na Bi Zuhura. Ni dadake Madhubuti. Ni mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya Nasaba Bora. Alikuwa na ilhamu ya kuwa mwandishi kama amu yake Mwalimu Majisifu lakini hio ndoto haikutimia. Ilionekana kuwa yeye ni mtu aliyezuzuka maishani. Hakuwa na lengo thabiti maishani na alielekea kufuata watu wasio na maana na walioweza kumharibu. Alishawishwa na kuzungwa na Ben Bella kijana aliyebobea upotovu na aliyekuwa amewahi kufungwa jela. Alimpenda kwa dhati na hakujali kuwa Ben ni jambazi. Huyo ndiye alikuwa mwelekezi wake na alipomwacha Mashaka hakuweza kuhimili kishindo hicho na akawa mwehu. Mashaka ni msichana mjinga. Kusuhubiana na mhalifu aliye sugu wa kifungo cha jela ni ujinga. Uamuzi huu uliweza kumwingiza mahali Pabaya. Ujinga wake ulidhihirika hata zaidi alipoamua kuacha shule na kupata msongo wa moyo na akili. Mwishowe aligeuka kuwa mwehu na akaanza kutembea uchi. 4.2.7 DJ BOB Huyu ni kijana mdogo wa miaka kumi. Ni mtoto wa mjane mmoja maskini aliyeishi Madongoporomoka huko Songoa. Aliwahi fungwa katika jela ya watoto wadogo kwa kusingiziwa kuwa ni mwizi. Alitakiwa awemo jela hadi umri wa miaka kumi na nane ndipo aachiliwe huru. Alitoroka jela na kwenda Sokomoko kwa ajili ya kujificha. Walipatana na Amani na Imani kando ya mto Kiberenge baada ya wao kufika Sokomoko. Ndiye aliyewaongoza hadi kwa Mtemi na nduguye mdogo Mwalimu Majisifu. Ni mchungaji wa mifugo wa Maozi, babayao Ben Bella na Lowela. Ni mchangamfu na alielewana na watu kwa haraka sana. Hata ilimbidi atumike kupitisha ujumbe baina ya watu. 57 Aliathirika sana na matumizi ya lugha ya Sheng. Alitumia Sheng kwa madaha na mbwembwe. Matumizi ya lugha hii yalimtambulisha na kumfanya aelewane na vijana wa mjini wa umri wake pamoja na watu wengine. Ni mwaminifu na mtiifu. Tangu wakutane na Amani na Imani waliaminiana hata akawaongoza kutafuta ajira yao ya kwanza baada ya kuwasili Sokomoko. Lowela bintiye Maozi alimtumia kama mjumbe wa kuwasilisha ujumbe wake wa siri kwa Mtemi, jambo ambalo alilitekeleza vizuri kutokana na uaminifu na utiifu wake Bi Maozi alimchukua tu kama mmojawapo wa wanawe japo yeye ni mtwana hapo nyumbani. Ni mraibu wa mchezo wa kandanda. Wakati alipomletea Amani ujumbe kuhusu ugonjwa wa mtoto Uhuru, alibaki uwanjani kushuhudia mechi baina ya timu za Sokomoko. Pia, alipokuwa akiishi mjini Songoa, alizoea kuenda kutazama mechi katika uwanja wa kitaifa. DJ Bob ni mtu jasiri. Alimkabili Mtemi Nasaba Bora na kumkosoa kwa kitendo chake cha kikatili cha kuwafungisha Amani ma Imani ambao hawakuwa na hatia yoyote. Alipata mkasa wa kuumwa na jibwa Jimmy nusura auwawe. Alipokimbilia zahanati ya Nasaba Bora na kutambua haikua na matibabu mwafaka hakusitasita alimuendea rafiki yake ambaye alimpa mitishamba hadi alipopata afueni. 4.2.8 BI ZUHURA Huyu ndiye mke wa Mtemi Nasaba. Ni mama yao Madhubuti na Mashaka. Aliishi kwenye kasri ambalo Mtemi alinyakua.Ni mvumilivu sana.Alivumilia mumewe ambaye alikuwa katili, mkali na mwenye macho ya nje. Alivumilia makaripio na maneno makali ya Mtemi. Aligundua kuwa kitoto kilichookotwa kilimshabihi mumewe na akavumilia tu. 58 Alikuwa na huruma kwa watoto kwani alitaka kumtunza mtoto aliyeletwa na Amani lakini mume wake alikataa.Alikuwa akiwasaidia akina Amani na Imani katika kumkimu mtoto japo kwa uficho ili mume wake asijue. Alimtetea sana DJ alipongatwa na mbwa Jimmy japo Mtemi hakuchukua hatua yoyote. Alimuonea huruma sana mwanamke aliyekuwa anajifungua njiani pekee yake akataka kumsaidiaa. Lakini mumewe alimkataza. Alimhurumia Amani na kumwomba mume wake amsaidie. Ni mshauri mkuu alimpa ushauri mume wake, maoni na maonyo ili kumsaidia awe mtawala mwenye kujali maslahi ya watu wake. DJ alipoomuuliza maswali mengi kuhusu mbwa hakukasirika na badala yake alimwelimisha kuhusu malezi ya mbwa kwa upendo. Alimtahadharisha Mtemi kuhusu Amani na Imani kuwa hawana makosa. Alikuwa na mapenzi ya dhati kwa wanawe. Aliwapenda vyema. Mashaka alipougua alihuzunika mno. Aidha, alishikwa na simanzi kuu Madhubuti alipohama na kwenda kuishi na Amani.Madhubuti alimtambua kuwa na utu ndiyo maana alijiita Madhubuti Bin Zuhura na sio Madhubuti Bin Nasaba Bora. Ni mwanamke mtiifu, hakuwa na macho ya nje ingawa upweke na ukiwa ulikuwa unamtafuna daima. Alipopewa talaka alikubaliana na hali hiyo, akaona afadhali shida zimwondokee za kukandamizwa na Mtemi “Kibanzi banduka name noye”(uk.34). Pia alikuwa msamehevu, alihudhuria mazishi ya mumewe japo alikuwa ameshatalikiwa. Yeye ndiye aliyetafuta kasisi wa kumzika Mtemi. Hakuzua ugomvi wowote alipogundua kuwa mtoto Uhuru alifanana sana na mumewe. Bi Zuhura ni kielelezo cha mtetezi wa wanajamii. Alijaribu kwa vyovyote vile kutetea watu lakini bidii yake iliangukia patupu maanake mumewake hakutaka kusikia chochote kutoka 59 kwake. Ni kielelezo cha wanawake wanaojitenga na uovu wa waume wao wakiwa uongozini. Anaonyesha shida na dhiki za kina mama walioolewa. 4.2.9 BI DORA Huyu ndiye mke wa Mwalimu Majisifu. Alikuwa akiteswa sana na mumewe. Alikuwa hodari sana katika kazi za nyumbani hasa ulezi wa watoto walemavu. Aliachiwa ulezi wa watoto wanne na mumewe. Ana utu kwa maana aliwatetea watoto wake wakati mumewe alipotaka kuwatupa majini. Alimjua mumewe vyema kwamba hakuwa na kipawa cha uandishi na akamtahadharisha ikiwa kweli angeweza kutoa mhadhara katika chuo kikuu. Ukweli huu ulidhibitika mumewe aliposhindwa kweli kutoa mhadhara katika chuo kikuu cha Mkokotoni (uk 121). Alikuwa mvumilivu mno kwa kuwa aliwajibika kumvumilia Mwalimu Majisifu kwa ulevi chakari, Lugha ya karaha, ugomvi, kujigamaba na uvivu. Aidha, aliwavumilia wanawe kwa moyo mmoja bila kusitasita. Alikuwa na uhusiano mzuri na mfanyikazi wake Imani na aliweza kumpenda na kumthamini sana. Yeye ni kielelezo cha wanawake wenye uvumilivu katika ndoa na kiwakilishi cha wale waja wanaokubali mikosi inayomfika mja yeyote. 4.2.10 KIMALIZIO Wahusika wasaidizi wana majukumu mengi kama tulivyoelezea na ni kupitia kwao ndipo tumeweza kupata mwanga zaidi kuhusu wahusika wakuu. Mwandishi amewaumba ili waweze kuamilika katika matendo, maneno na mawazo yao kama watu wanaoishi kweli. Kutokana na mtazamo huu wa wahusika juu ya maisha yao kukua na kubadilika nao. Wahusika wasaidizi ni rahisi kuwatambua kama wawakilishi wa watu fulani katika jamii. Hayo ni baadhi ya mambo ambayo tushaelezea hapo awali. 60 4.3 WAHUSIKA WAJENZI 4.3.1 UTANGULIZI Kulingana na Njogu na Chimerah (1999:42) wahusika wajenzi hubuniwa kwa lengo la kukamilisha dhamira na maudhui ya mwandishi. Wao hujenga wahusika wasaidizi na wakuu. Kundi hili ndilo huwakilisha jamii pana, na matendo yao, angalau huonekana kana kwamba ni ya pembezoni, japo kwa hakika ni muhimu sana katika kuelewa muundo wa jamii. Wahusika hawa hulingana moja kwa moja na wazo au sifa fulani. Wamebuniwa kwa kuzingatia matendo na sifa walizopewa. Baadhi ya wahusika wajenzi katika Kidagaa Kimemwozea ni pamoja na Ben Bella, Bwana Maozi, Chirchir Hamadi, Oscar Kambona, Lowela, Bi. Maozi, Chwechwe Makweche, Michelle, Yusufu, Fao, Uhuru, Mwinyitabu Mutembezi na wengineo. 4.3.2 BEN BELLA Ben Bella ni mtoto wa kiume wa Bi na Bw. Maozi. Ni kaka yake Lowela ambaye walipendana sana na hawakufichana siri. Alikuwa na hulka ya uhalifu na alizoea kufungwa gerezani. Alikuwa amekamilisha kifungo cha miaka miwili kwa tuhuma ya kubaka mtoto mdogo. Baadaye walikutana na kufahamiana na Mashaka. Ni mraibu wa bangi na sifa hii inasisitiza mwenendo wake wa kihalifu. Namna alivyokuwa akivaa ilikuwa ishara ya mwenendo wa kichepe wa kutojali na wa uhalifu. Pamoja na kuwa mhalifu, pia ni mpotevu; hakusuluhia maishani. Mwenendo wake ulisigana vibaya na kaida na kanuni za maisha ya jamii. Vitendo vyake kama vile mavazi ya kichepe, uraibu wa kuvuta bangi, ubakaji na visa vingine vya jinai ni vitendo vya upotovu. Ben Bella alipenda raha. Mavazi yake, mapenzi yake ya muziki wa kufokafoka, uraibu wake wa bangi, umahiri wake wa kucheza densi ni ishara ya kupenda raha. Kupenda raha kwake 61 ndiko kulikomfanya ajiingize katika njia potovu ili ajipatie uwezo wa kuendeleza raha. Yeye pia ni mnyanganyi na muuaji. Alikuwa na maneno matamu ya kuwavutia wasichana wadogo wa shule kama Mashaka. Aidha, Ben alipewa taji kwa ubingwa wa kucheza densi baada ya kuibuka mshindi jimboni mwao (uk 80). Ingawaje anadhihirisha udhaifu huu hatua yake ya kusitisha urafiki wake na Mashaka alipogundua kuwa Mtemi alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na dadake Lowela inamtambulisha kama mhusika mwenye ujasiri. 4.3.3 BWANA MAOZI Huyu ndiye baba wa Lowela na Ben Bella. Alikuwa jirani wa Mtemi Nasaba Bora. Alikuwa mwajiri wake DJ bob. Hakuwa mtu mzuri maanake alishindwa kuwapa wanawe malezi bora. Aidha, DJ alipong’atwa na mbwa hakujali kumpeleka hospitali nzuri. Bwana Maozi ni kati ya watu wachache waliohudhuria mazishi ya Mtemi. Ni kielelezo cha ujirani mwema, alihudhuria mazishi ya Mtemi japo alimharibu binti yao Lowela. Anaendeleza wazo la unyanyasaji wa matajiri kwa watoto. Alimwajiri Bob DJ, mtoto wa miaka kumi achunge ngombe wake. 4.3.4. OSCAR KAMBONA (GADDAFI) Huyu ni mwanawe Mwinyitabu Mutembezi. Alikuwa kaka wa Imani na Chwechwe. Alikuwa na jina la kupanga la ‘Gaddafi.’ Alijihusisha na biashara ya kuuza bangi na ndiposa alifungwa jela. Akiwa gerezani aliwahi kutana na Amani na wakajuana. Alishuhudia manyanyaso mengi na mateso aliyofanyiwa mama yake na askari wa Nasaba Bora. Ni kutokana na hayo ndipo aliamua kulipiza kisasi kwa Nasaba Bora baada ya kifo cha mamaye. Alikuwa mmoja wa waathirika wa kuporwa mashamba na Mtemi. Alipotoka gerezani aliungana na majambazi wengine kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa Mtemi Nasaba. Kutokana na nasaha za 62 Amani aliahirisha nia yake ya kutaka kumuua Nasaba Bora. Aidha, alishauriwa na Imani aache azma yake ya kulipiza kisasi na badala yake arudi nyumbani akamtunze ndugu yao Chwechwe aliyekuwa kilema kutokana na ajali ya soka. Kambona ni kielelezo cha athari mbaya za vijana zinazotokana na watu wazima waliopotoka. (Nasaba Bora ndiye chanzo cha utovu wake wa nidhamu). Anawakilisha kundi la vijana wenye tabia ya kujihusisha na madawa ya kulevya. Pia, anaghadhabishwa na Nasaba Bora kutokana na maovu aliyoyafanyia familia yake na kuapa kulipiza kisasi. 4.3.5 LOWELA Ni bintiye Bwana na Bi. Maozi. Ni dadake Ben Bella ambaye walipendana sana na hawakufichana siri. Aliacha shule kidato cha tatu ili aponde maisha. Alikuwa mpenzi wa Mtemi. Alipata mimba akaificha kwa kuifunga mkanda hadi akajifungua kitoto kilichotupwa mlangoni mwa Amani. Hakuwa na huruma na kitoto chake na ndiposa akaweza kukitupa. Alikuwa akimtuma DJ Bob kupeleka barua kwa Mtemi Nasaba Bora. Ni mpotovu kinidhamu kwani alimkashifu Bi. Zuhura katika barua yake kwa Mtemi ingawa yeye ndiye aliyeingilia ndoa yake. Ni kielelezo cha vijana wanaoshindwa kudhibiti tamaa za ujana. Ni mfano mbaya kwa vijana kwa vile anavuruga ndoa ya Bi. Zuhura. Ni vyema msichana angojee aposwe akiwa bado kwa wazazi wake na asijihusishe na mapenzi mapema. 4.3.6 CHICHIRI HAMADI Huyu ndiye babaye Yusufu na babu yake Amani. Alikuwa mhadhiri huko London. Aliweza kununua makao ya Majununi iliyokuwa katika maeneo yakifahari kwa mkopo. Alinunua makao hayo kutoka kwa mzungu aliyekuwa mwanzilishi wa makao hayo. Pindi tu alipofika kutoka ngambo Mtemi aliwatuma majambazi wamuue ili aweze kuchukua mashamba yake kwa urahisi. Kifo chake kilizingiziwa mwanawe Yusufu ambaye alifungwa kifungo cha maisha. Chichiri ni 63 kielelezo cha wamiliki wa mali walioipata kwa jasho lao halali. Ana wakilisha watu wanaouawa bila hatia kutokana na hila za viongozi za kutaka kupokonya raia mali. 4.3.7 BI MAOZI Huyu ndiye mke wa Bw. Maozi. Ni mamayao Ben Bella na Lowela. Alishindwa kuwalea wanawe kwa njia inayofaa. Hakuwapa mawaidha ya kuwafaa maishani na ndiposa wakawa na mielekeo inayoaibisha. Hakujali, masilahi ya DJ Bob ambaye alikuwa akimchungia ng’ombe. DJ alikua na kaptula moja tu na hivyo hakuwa akipata msaada wowote kutoka kwake. Aliyapuuza mambo yote yaliyokuwa yakitendeka nyumbani kwake na hakuweza kutoa ushauri wowote. Ni kielelezo cha wanawake ambao hawajui haki zao na wanaona kila kitu kama ni maajaliwa. 4.3.8 MWINYI HATIBU MUTEMBEZI Alikuwa baba yao Amani, Chwechwe Makweche na Oscar Kambona. Alikuwa miongoni mwa Waafrika waliokwenda nchini Burma kumpigania mkoloni. Aliporudi nchini mwake aliendeleza harakati za ukombozi. Alikuwa ameapa kuwaunganisha Waafrika wenzake ili wamng’oe mkoloni. Kutokana na kupinga serikali ya ukoloni aliweza kufutwa kazi. Alikufa katika mapambano ya ukombozi na vilevile shamba lake alilopokonywa na Mtemi. Alikuwa akijali maslahi ya familia yake na ndiposa aliwaachia urithi wa shamba lake. Ni kielelzo cha watu waliokwenda kupigana katika vita vya dunia na baada ya kurudi hawakukumbukwa na serikali ya kikoloni licha ya madhara waliyoyapata huko. Ni kiwakilishi cha wapigania ukombozi ambao hawathaminiwi baada ya kifo. 4.3.9 MICHELLE Ni mwanamke Mfaransa aliyependana na Majununi (Major Noon). Alidhamini mapenzi ya mali, yaani alimpenda Majununi kwa masharti mazuri, nyumba nzuri ya kifahari na kadhalika. Baada 64 ya Majununi kushindwa kumtekelezea matakwa yake alivunja uchumba wao. Ni mnafiki kwa sababu alipogundua hisia zake za mapenzi zilikuwa zimeisha alitafuta visingizio vya kuuvunja uhusiano huo. Alimkataa majununi kwa kushindwa kumtekelezea mahitaji finyu yasiyo na mashiko. 4.3.10 YUSUFU Ni mwanawe Chichiri Hamadi na ni amu yake Amani. Alisingiziwa kuwa alimuua babaye Hamadi na hivyo alifungwa jela kifungo cha maisha. Alikuwa amepangiwa kuuawa pamoja na baba yake ila Majambazi walikosea wakamuacha. Alifidiwa mamillioni ya pesa baada ya kushinda kesi. Amani ndiye aliwakilisha malalamishi kumhusu kortini na akaweza kuachiliwa huru. Ni kielelezo cha watu ambao wanateseka gerezani kutokana na makosa ya kuzingiziwa. 4.3.11 FAO Alikuwa rafiki yake Amani enzi ya utoto wao hasa walipokuwa shule ya msingi, huko ulitima. Alikuwa amehitimu kama mwalimu. Hakuwa mfano mzuri kwa sababu alijiingiza kwenye mapenzi na mwanafunzi wake. Kimasomo alikuwa mfano mbaya kwa sababu alifanyiwa mitihani ya kitaifa na mtu mwingine. Anawakilisha watu wenye tabia mbaya ya kufaulu kwa kuiba au kufanyiwa mtihani. Ni kielelezo cha picha potovu kuhusu mwalimu ambaye anatakikana kuwa na maadili mema. 4.3.12 UHURU Huyu ni mtoto aliyepewa jina hilo na Amani baada ya kutelekezwa mlangoni kwake Amani. Amani alimpeleka kwa Bi. Zuhura ili aweze kusaidiwa lakini Mtemi Nasaba alimkataza kumshungulikia. Amani alirudi naye kibandani chake na akamuita Imani aje kumsaidia kumlea. Walimtunza vyema kama mtoto wao lakini alifariki kwa kukosa huduma za kiafia kufuatia 65 uzembe wa wauguzi katika hospitali ya Nasaba Bora. Kupitia kwake tunaona ukosefu wa utu na anawakilisha watoto wanaoathirika kutokana na maovu ya wanajamii. 4.3 .13 CHWECHWE MAKWECHE (HORSE POWER) Ni mwanawe Bwana na Bi. Mutembezi Mwinyihatibu. Ni kaka yao Imani na Oscar kambona. Alikuwa mwanasoka maarufu na hodari katika timu ya Songoa FC. Aghalabu aliliinua jina la Taifa lake baada ya kuongoza timu yao katika ushindi katika nchi za nje. Alikuwa akiishi kwao Baraka alipochukuliwa ili ajiunge na timu ya Taifa, alipogunduliwa ana kipawa. Kisha akakikuza hakuwahi wasiliana na familia yake tangu atoke kwao. Alivunjwa fupa la mguu na ikawa ndio hatima ya uchezaji wake. Baada ya kuumia, hakuna aliyemjali ila mwandishi mmoja mwenye huruma aliyemtembelea na kuchapisha habari yake kwenye gazeti. Ni mhusika ambaye aliathirika pia kwa matendo ya Nasaba Bora. Baada ya mama yake kupokonywa ardhi naye aliathirika sana na hakuweza kuwasiliana na nduguze 4.3 .14 BALOZI Huyu alikuwa rafiki na Msiri wa Mtemi. Alimwakilisha Mtemi kwa kila jambo kama lilivyo jina lake. Aliongoza sikukuu za wazalendo. Alikuwa mcheshi mno na aliweza kuwachekesha wanahadhira, waliohudhuria sikukuu ya Wazalendo. Aliwafumba wanasokomo macho kwa kumpa Mtemi sifa kubwa alizokuwa hastahili. Kumhusu Mtemi alidai: “Kiongozi aliyeteuliwa na Mwenyezi Mungu. Yeyote aliyempinga alipingana na Mwenyezi Mungu.” (uk 68). Ni kielelezo cha vibaraka wanaosaidia kuendeleza utawala mbaya kwa kutumia propaganda ili kuwafunga raia macho wasione wanavyonyanyaswa. 66 4.3.15 MAMA IMANI Ni bibiye Mwinyihatibu Mutembezi. Ni mama yao Chwechwe, Kambona na Imani. Alikuwa mjane aliyedhulumiwa na Nasaba Bora. Ni mtetezi wa haki zake maana alikataa katakata kuachilia shamba lake la Baraka. Alichapwa na Askari wa Mtemi mpaka akafa. Ni kielelezo cha jinsi walio uongozini huwaumiza raia wao wanyonge. Jamii haina mikakati ya kutetea wajane, hasa wajane wa waliopigania ukombozi. 4.3.16 MAC ARTHUR KUTO Huyu ni mkuu wa Idara ya Isimu na Lugha Chuo cha Mkokotoni (nchi ya Wangwani). Ndiye aliyemwalika Mwalimu Majisifu kwa njia ya barua. Alizitambua sifa za Mwalimu za kuwa gwiji wa fasihi na ubunifu. Alimpa Mwalimu Majisifu fursa ya kutoa mhadhara ukumbini lakini Mwalimu Majisifu hakuweza. Ni Mhadhiri ambaye anapenda kubadilisha mawaidha na vyuo vingine na sio mchoyo. Kupitia kwake tunajifunza kwamba ni vyema kushirikiana na vyuo vya nchi zingine kitaaluma. 4.3.17 KIMALIZIO Wahusika wajenzi wameweza kufikia lengo lao la kukamilisha dhamira na maudhui ya mwandishi. Wameweza kutuangazia zaidi juu ya wahusika wasaidizi na wakuu. Hili kundi ndilo lililowakilisha watu wengi katika jamii. Wengi wao ni wazuri, waovu, wavivu na kadhalika, kama tulivyoelezea. Walinyonywa ma kukandamizwa vibaya na Mtemi Nasaba na walilazimishwa kumpa sifa za kinafiki badala ya kulalamika. Walipozinduliwa na vijana walizinduka na matokeo yake tumeyaona. 67 SURA YA TANO HITIMISHO NA MAPENDEKEZO 5.0 UTANGULIZI Katika tasnifu hii, tumewasilisha hitimisho la utafiti wetu. Tumetoa muhtasari na mchango wetu ambao tunaona tumeudokeza kwa uwazi, pia tumeyajibu kimamilifu maswali ya kiutafiti tuliyoyatumia kama dira ya kuongoza kazi hii. Pamoja na hayo tumetoa mapendekezo kwa wasomi na watafiti wa siku za usoni. 5.1 MUHTASARI Katika tasnifu hii, tuliazimia kuchunguza jinsi mtunzi wa Kidagaa Kimemwozea (2012). Alivyoshughulikia maudhui na suala la wahusika. Katika kuchunguza usawiri wao, mbinu zilizotumika kuwasawiri, umuhimu na majukumu yao tumegundua kwamba mfumo wa ubabedume bado upo. Wahusika kama vile Nasaba Bora na nduguye Majisifu ni bingwa wa kuwatesa na kuwadunisha wanawake. Lakini kuna wanaume kama Imani na Madhubuti ambao wamejitolea kutetea watu wa jinsia zote. Wahusika wa kike wamesawiriwa kama walezi, wategemezi wa wenzao wa kiume, viumbe dhaifu na duni, wenye laana, na ambao kazi yao ni kuzaa tu. Wamedhihirishiwa haya kwa kubakwa, kutalakiwa, kuachiwa upweke, kunyang’anywa watoto, kuchapwa, kutusiwa na kuaibishwa kwa aina yote. Ni kama kwamba mwandishi anaihukumu jamii kwa ukatili na unyama unaoendelezwa dhidi ya wanyonge Wanaume kwa upande wao wamechorwa kama wenye nguvu, amri zote na uwezo mkubwa wa kuamrisha wanawake. Jamii inawadekeza zaidi na inawachukulia kama watu wasio na kosa hata moja. 68 Hatuwezi kuwalaumu wahusika wote wa kike na wa kiume kwani kuna baadhi yao ambao wamechukua mwelekeo mwingine. Amani anaamua kushirikiana na Imani kwa kila jambo. Naye Bi. Maozi anaiona hali ya kunyanyaswa na mwanaume kama ni majaliwa tu. Pia tumegundua kwamba makosa mengi yanatokana na utamaduni wa jamii husika, kwa mfano Mtemi alichaguliwa kuwa kiongozi kutokana na uhusiano wake na Mudir wa Wilaya kwa sababu walikuwa wa ukoo mmoja. Ushirikiano ni jambo la maana sana katika jamii na ndio ulioweza kunusuru jamii husika kutokana na utawala mbovu wa Mtemi. Ushirikiano wa vijana kama vile Madhubuti, Imani, Amani na wengine unapelekea kuufichua upotovu wa Mtemi na kumuumbua vibaya. Mabaya aliyoyatenda yanawekwa wazi naye anajingatua uongozini na kujinyonga. Huku kujinyonga kwake kunaiondolea jamii mzigo mkubwa wa hiana na dhuluma. Kwa hivyo uzalendo wa nchi ili ufufuliwe lazima watu waungane na kuvunja mipaka ya kinasaba, kikabila, kitabaka na kadhalika kama walivyofanya wanasokomoko. Kuhusu umuundo ni kwamba Riwaya imejitokeza kama zao linalojitosheleza. Tumepata kwamba hakuna namna kipengele kimoja cha sanaa kinaweza tumika katika upekee wake ni lazima kihusiane na kukamilishana na kingine kwa mfano, huwezi kutaja maudhui bila kuhusisha wahusika na lugha inayotumika na kadhalika. 5.2 HITIMISHO Utafiti huu uliongozwa na maswali ya utafiti mawili. Kwanza, ni mbinu zipi zilitumiwa kuwaumba wahusika? Wahusika wameumbwa kwa ukamilifu mzuri na wamechangia katika 69 kufanikisha ujumbe kwa njia inayoeleweka na ya kuvutia. Wameweza kutekeleza majukumu waliopewa na jamii ya kuipindua na kubadilisha hali yao ya maisha. Swali la pili lilikuwa, ni vipi mwandishi ameshughulikia maswala anuwai katika kazi yake? Ni dhahiri kwamba juhudi za mwandishi zimefanikiwa katika kushughulikia suala la ukombozi. Mapambano ya kishujaa ya kupinga utawala dhalimu yaliendeshwa na vijana ambao walishirikiana ili kuboresha maisha yao naya wanajamii wenzao. Baadhi ya mambo waliyokuwa wakipinga ni uozo wa viongozi, ukosefu wa haki, ukatili, tama, udhalimu na maovu mengine. Kupitia kwa wahusika tofauti msomaji ameweza kujifunza mambo kadha wa kadha. Kwa mfano kupitia kwa Mtemi Nasaba ni dhahiri ya kwamba hatima ya kuwatendea wanyonge maovu ni maafa. Na kutokana na vijana ni bayana ya kwamba wanyonge wakishirikiana wanaweza kuondoa vizingiti vinavyovuruga maisha yao. Kwa hivyo ni dhahiri ya kwamba mwandishi Ken Walibora amefaulu katika azimio lake la kuelimisha wasomaji wake kupitia riwaya yake ya Kidagaa Kimemwozea. 5.3 MAPENDEKEZO Riwaya hii imefanyiwa uhakiki kadha wa kadha lakini bado sehemu nyingi ambazo kwa sababu ya wakati na mada tuliyojikita kwayo haingewezekana kuzijadili zote. Utafiti huu umeshughulikia maudhui na fani katika fasihi andishi kwa kurejelea Kidagaa Kimemwozea. Hata hivyo hatuwezi kudai kwamba uchunguzi huu umekamilika na kwamba Kidagaa Kimemwozea haiwezi kufanyiwa uchunguzi mwingine wowote. Mapendekezo yetu ni kwamba vipengele vingine vya fani kama vile msuko, matumizi ya lugha na vinginevyo vifanyiwe uchambuzi ili kubainisha ikiwa vinaweza kuwasilishwa kwa mtazamo wa nadharia ya umuundo. 70 Riwaya hii pia inaweza kuhakikiwa kwa kutumia nadharia zingine tofauti kama vile Ufeministi wa Kiafrika na nadharia ya Baada ya Ukoloni ili wasomaji waweze kudurusu yaliomo kutokana na mitazamo mingine tofauti. Pia nadharia ya Baada-Ukoloni inaweza tumiwa kuchambua maudhui. Utafiti huu ni muhimu katika fasihi ya Kiswahili kwa sababu umetoa mchango mkubwa katika kuziba pengo lililokuwepo la uhakiki wa matini za kifasihi za Kiswahili katika misingi ya nadharia za umuundo na uhalisia, hasa uhalisia wa kijamaa. 71 MAREJELEO Barry, P.(1995) Beginning Theory. An Introduction to Cultural Theory. Culler, J (2003) Structuralism and Literature London: May field publishing company Escarpit, R. (1971) Sociology of Literature Frank and Cass: London Forster, E. M (1927) Aspects of the Novel. London: Penguin Books Gikandi, S. (1986) Reading the African Novel, Nairobi: Heinemann Gorky, M (1921) Though Russia. London: CJ Hoogarth. Hawkes, T. (1997) Structuring and semiotics, London: Methuen Hawthorn, T. (1997) Studying the Novel: An introduction 3rd Edition London: Edward Arnold. Hegel, G (1971) Introduction to Aesthetics: Oxford: Clerendon. Hochman, B. (1985) Characters in Literature Ithaca: Cornell University press. Hough, G (1966) Essay on Criticism London: Duckworth. Katola, E (2006) Usawiri wa Mhusika wa Kike. Tasnifu ya MA Chuo Kikuu Cha Nairobi. Kundera, M (1986) The Art of the Novel; London : Faber and Faber. Leech, G. (1969) A linguistic Guide to English Poetry. London ; Longman Leech & Short (1981) Style in fiction. Essex: Longman. Lugano, R. (1989) Usawiri wa wanawake katika riwaya za Euphrase Kezilahabi. Tasnifu ya MA Chuo Kikuu Cha Nairobi (Haijachapishwa) Lukacs, G. (1979) The Meaning of Contemporary Realism: London: Merlin Mbatia, A. M. (2002) Kamusi ya Fasihi, Nairobi: Standard Textbooks Mlacha na Madumulla (1991) Riwaya ya Kiswahili Dar-es-Salaam Dar-es-salaam University Press Mohamed, A. S (1972) Kiu, Nairobi: Longman (1980) Utengano, Nairobi: Longman (1989) Asali Chungu Nairobi: EAEP (2001) Babu Alipofufuka Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation 72 (2010) Nyuso za Mwanamke Nairobi: Longman Publishers. Msokile, M. (1992) Misingi ya Hadithi Fupi. Dar-es-salaam University Press. Muindi, A (1990) Usawiri wa wahusika makahaba katika vitabu vya Said A. Mohamed. Tasnifu ya MA Chuo Kikuu cha Nairobi. Mulila, A. K. (2005) Muala na mshikamano katika Kiswahili: umuhimu wake katika uchanganuzi wa riwaya ya Vipuli Vya Figo. Tasnifu ya MA Chuo Kikuu cha Nairobi. Murray, P( 1978) Literary Criticism: A Glossary of major Terms: Longman. Ndungu, N. (1996) Uhakiki wa fani katika Riwaya za Katama Mkangi. Tasnifu ya MA Chuo Kikuu cha Nairobi. Njogu, K. na R, Chimerah (1999), Ufundishaji wa Fasihi na Mbinu, Nairobi: JKF Otieno, O.N (2005) Matilaba na utendi wa Malengo na wahusika. Tasnifu ya MA Chuo Kikuu cha Nairobi. Scholes, R. (1974) Structuralism in Literature New Haven: Yale University Press. Shifa, A. N (1971) In Topan F. M (Mh) Uchambuzi wa Maandishi ya Kiswahili Dar-es-salaam: OUP. Syambo, B. n.w (1992) Uchambuzi wa Fasihi, Nairobi: EAEP. Traore, (2008) Suala la familia na jamii katika riwaya sita za Said Ahmed. Tasnifu ya MA Chuo Kikuu cha Nairobi. Trotsky, L (1971) Literature and Revolution. USA: University of Michagan press. Vladimir, P (1999) The structure of Russian Fairy Tales. Boston: Rowman & Litle field Publishers. Wafula, R. M na K. Njogu (2007), Nadharia za uhakiki wa fasihi, Nairobi JKF. Walibora, K, (2012), Kidagaa Kimemwozea, Nairobi: Target Publications Limited Wamitila, K. W (2002) Uhakiki wa Fasihi, Misingi na Vipengele vyake, Nairobi: Phoenix Publishers. 73 (2003) Kichocheo cha Fasihi Simulizi na Andishi, Nairobi: Focus publications Ltd. (2008) Kanzi ya Fasihi: Msingi ya Uchanganuzi wa Fasihi, Nairobi: Vide-muwa Publishers Ltd. Wanyonyi, C. M (2011) Uhakiki wa riwaya ya Nyuso za Mwanamke na Said Ahmed: Tasnifu ya MA Chuo Kikuu Cha Nairobi. Welleck, R. Warren (1986) Theory of Literature, Harmondsworth: Penguin

TAHAKIKI YA TAMTHILIA KIGOGO

Posted by DUNCAN WERE LUTOMIA - Sep 20, 2017


Kwa wadau wa fasihi, hii hapa ni tahakiki yangu ya tamthilia ya Kigogo, maoni yanakubalika KIGOGO: TAMTHILIA INAYOANGAZIA UOZO ULIOTAMAKANI KATIKA JAMII NA JINSI YA KUUKOMESHA Anwani: Kigogo Mwandishi: Pauline Kea Mchapishaji: Storymoja Mhakiki: Duncan Were Lutomia Kitabu: Tamthilia Kurasa: 94 Bei: KES 377 Uandishi wa tamthilia kama Sanaa ya maonyesho umefikia upeo wa juu. Kwa muda mrefu, hapajawahi teuliwa kitabu kinachotahiniwa katika shule za sekondari ambacho mwandishi wake ni wa kike! Waandishi wengi waliobobea wameibuka huku kila mmoja akidhihirisha umahiri wake katika taaluma hii. Uteuzi wa Kigogo kama kitabu seti kwa kiwango kubwa kimewapa hadhi waandishi wa kike humu nchini na kuleta usawa katika Sanaa ya uandishi. Kigogo ni tamthilia iliyogawika katika maonyesho saba(7), na maonyesho hayo yamegawanywa katika matendo kadhaa. Huu ni mtindo sahili na wa kipekee ambao mwandishi ameutumia kuwasilisha kazi yake. Mwandishi ameangazia na kusawiri mandhari ya jimbo la Sagamoyo ambako mamlaka yote ya nchi yako chini ya Kigogo Majoka na vikaragosi wanaomuunga mkono. Maandhari haya yanaakisi mandhari kamili ya mataifa ya bara la Afrika, panaposhuhudiwa migongano na harakati za ukombozi zinazoendelezwa na wazalendo halisi ili kuleta haki na usawa katika jamii. Kigogo ni tamthilia inayoelezea kwa ustadi mkuu uozo katika jamii, uongozi mbaya, ukoloni mamboleo na harakati za kuzitetea haki. Mwandishi anaukosoa uongozi mbaya uliopo katika baadhi ya nchi zilizotawaliwa na wakoloni enzi zile. Mengi ya mataifa haya yameeathiriwa na mfumo wa ukoloni mamboleo unaoendelezwa na watawala wenyeji. Huku wakazi wa Sagamoyo wakijiandaa kuadhimisha siku ya uhuru utakaosherehekewa kwa mwezi mmoja na kujivunia maendeleo makuu, soko la Chapakazi, ambalo ndilo tegemeo la wengi linafungwa. Swali ni je, linafungwa kwa nia ipi? Mwandishi pia anatujuza mbinu wanazotumia watawala kuhakikisha kuwa wanasalia madarakani. Kwa mfano utawala wa Majoka- Kigogo, unatumia vitisho, ukandamizaji na hata mbinu ya tenga tawala. Utawala wa nchi nyingi zinazostawi unaonekana ni wa kurithishwa kutoka kwa familia tajika. Majoka anataka kumrithisha mwanawe Ngao Junior utawala pindi tu atakapostaafu. Utawala unakiuka haki za wananchi kwa kuwakandamiza, kwa mfano kulifunga soko la Chapakazi, linalotegemewa na wakazi na wachuuzi kwa riziki yao ya kila siku. Mchango wa vijana ni muhimu sana katika harakati za ukombozi wan chi kutokana na uongozi dhalimu. Ndivyo anavyodhihirisha Pauline Kea. Vijana ndio viongozi wa kesho hivyo basi wanafaa kupigania haki zao kwa vyovyote vile. Bila shaka Sudi na Tunu wanaajibikia hili. Mwandishi amewajenga wahusika wake kwa njia halisi inayoakisi jamii za nchi zinazoendelea. Viongozi wanasawiriwa kama wanyanyasaji. Kuna wahusika ambao ni wafuasi kindakindaki wa utawala wa Majoka kwa mfano Ngurumo na walevi wenzake. Kuna wale wanaoupinga utawala wa Majoka kama vile Sudi na Tunu. Wanaoupinga utawala wa Majoka wanajikuta pabaya kwa kuvamiwa (Tunu) na kuumizwa. Hivyo basi baadhi ya wahusika wamezinduka ilhali wengine ni “vipofu’. Kifani, mwandishi amefaulu sana katika kutumia mbinu za sanaa na tamathali za usemi. Pana matumizi mengi ya jazanda kwa mfano keki ya uhuru, taswira, taharuki, na mbinu rejeshi. Tamathali za usemi ni pamoja na methali, tashbihi, misemo, kuchanganya ndimi n.k. Pia kuna mbinu za uandishi kama vile mdokezo, nidaa, litifati na kuhamisha msimbo. Hili linaongeza ladhaa lugha licha ya kumsisimua msomaji na kurembesha sanaa yake. Aidha mwandishi ametumia mtindo wa kinudhumu ambapo amehusisha nyimbo na mashairi. Hata hivyo mwandishi ameegemea sana matumizi ya mbinu za uandishi hasa nidaa/kihisishi na mdokezo. Mbinu hizi zinajitokeza kwa wingi hivyo kufinya maudhui. Licha ya hayo, tamthilia hii imetungwa kwa ustadi mkubwa unaonata msomaji. Bila shaka tamthilia hii ni tunu kwa wanafunzi na wadau wote wa lugha ya Kiswahili!!

Barua kwa mhariri

Posted by Erick - Mar 24, 2017


wadau eeh naombeni usaidizi,nisaidieni na jinsi ya kuandika barua kwa mhariri jameni