Jukwaa La Kiswahili

Karibu kwenye jukwaa letu la Kiswahili

HAWATAKi...

Posted by Mstahiki zack - Dec 19, 2015


HAWATAKI... nasaha zishatolewa,ela wao hawataki. Tushapiga nazo duwa,ela kwao hazifiki. Wanajifanya kujuwa,kuchapo hawashikiki. Hawataki hawataki,hawa vijana watundu. Elimu hawathamini,wanajiona mahiri. Wanaupenda uhuni,kichwa chote ni kiburi. Washajiweka shidani,inawangoja kaburi. Hawataki hawataki,vijana hawa watundu. Leo natoa mfano,wamejaa kote nchini. Wanazithamini ngono,hawakomi danguroni. Hupenda na mapigano,wakiwapo ulevini. Hawataki hawataki,vijana hawa watundu. Sizidishi na kubuni,mwisho wangu nimefika. Dunia ipo mbioni,ninajuwa tawashika. Iwapee mitihani,walie kwayo mashaka. Hawataki hawataki,vijana hawa watundu. @mstahiki zack sauti ya babu.

Chemistry

Posted by Gideon Rono - Oct 24, 2015


notes

Heko Wallah Bin Wallah

Posted by Vianney Muli - Oct 19, 2015


Ni shairi lenye mtiririko mwafaka kabisa. Heko kwa mtunzi pia

kidagaa kimemwozea

Posted by Hassan Albannah - Oct 03, 2015


'asasi ya ndoa katika riwaya ya kidagaa kimemwozea inakabiliwa na changamoto nyingi' Jadili

UKAHABA JAMBO OVU.

Posted by Mstahiki zack - Oct 02, 2015


UKAHABA JAMBO OVU,MABINTI JISITIRINI.
nakipuliza kipenga,hadhirani sikizeni.
nimekuja kuyapinga,maovukwa ubishani.
mkono sitowaunga,mahawara wafitini.
ukahaba jambo ovu,mabinti jisitirini.

kujiuza mitaani,ni nini unafaidi.usiku wote mjini,wapigwa nayo baridi.
nusu uchi kimwilini,ati huo ni mradi.
ukahaba jambo ovu,mabinti jisitirini.

ngozi iliyokupwaya,waitembeza mjini.
usiku wawayawaya,kujitapa danguroni.
hauoni hata haya,ukimwi upo mbioni.
ukahaba jambo ovu,mabinti jisitirini.

mwajifanya hamjali,kujionyesha taswira.
magonjwa hayapo mbali,mtaanza na kuhara.
mjifiche viamboni,kwa sura ziloparara.
ukahaba jambo ovu,mabinti jisitirini.

sasa ni mitandaoni,utupu mwauanika.
munatukera juweni,kuwaona tumechoka.
hatupendezwi baini,fahamu pia mwanuka.
ukahaba jambo ovu,mabinti jisitirini.

zimekana Qur'an,nazo pia Bibilia.kuenda na vilabuni,kaburi mwajijengea.
mtaupata mtihani,mwishowe mtajutia.
ukahaba jambo ovu,mabinti jisitirini.

kazi zipo vijijini,zifwate mzifanyeni.
muondoke mitaani,umalayaukomeni.
msirushwe misibani,visonono vijuweni.
ukahaba jambo ovu,mabinti jisitirini.

munawaiga wazungu,kufanyaya hayawani.
na tabia za kizungu,mumezianza mijini.
juwa mwamuudhi Mungu,mwisho mwaenda motoni.
ukahaba jambo ovu,mabinti jisitirini.

kwa walioa jamaneni,msitoroke ndoani.
mkaenda mitaani,kujideka pabayani.
mkaja ugua ndani,na mkafa karibuni.
ukahaba jambo ovu,mabinti jisitirini.

wanafunzi msomeni,msiendevilabuni.
mkahepa mashuleni,kujiuza mitaani.
mboko zipo hadharani,shauri yenu wendani.
ukahaba jambo ovu,mabinti jisitirini.

nikizidi kuandika,nitawaudhi bwaini.heri mwisho kuufika,kwa kauli mtimani.
ukahaba kihakika,wanadamu tuacheni.
ukahaba jambo ovu,mabinti jisitirini.

kaditama najipunga,ashakum si matusi.
shairi nishalitunga,lisomeni kwayo kasi.
nami hapa najitwanga,nishatoa wasiwasi.
ukahaba jambo ovu,mabinti jisitirini.

UTUNZI WA.
SAUTI YA BABU.
MSTAHIKI ZACK