Jukwaa La Kiswahili

Karibu kwenye jukwaa letu la Kiswahili

HEKO WALLAH BIN WALLAH.

Posted by Mstahiki zack - Oct 02, 2015


HEKO WALLAH BIN WALLAH.

Rabbi Mola Msifika,nipe swiha ya kutunga.
nitunge pasi mashaka,mishororo kuipanga.
mengi nipate tamka,ya ukweli kubananga.
Heko Wallah Bin Wallah,Kiswahili kukikuza.

Nasaha zako ni bora,binadamu zatwongoa.
tanadhari za busara,gizani zinatutoa.
husemi kwa masihara,sheng yote ushang'oa.
Heko Wallah Bin Wallah,kiswahili kukikuza.

mlezi wa kiswahili,Guru Wallah bin Wallah.
asemayo ni halali,Guru Wallah Bin Wallah.
kwa lugha twamukubali,Guru Wallah Bin Wallah.
Heko Wallah Bin Wallah,Kiswahili Kukikuza.

vipindi meshachangia,redio na runingani.
vitabu metwandikia,vyatumika mashuleni.
hadithi zako murua,zatuweka furahani.
heko Wallah Bin Wallah,kiswahili kukikuza.

afrika mashariki,Gwiji tunakutambua.
katu wewe hushikiki,lugha yako ni halua.
vipaji mevimiliki,kote wewe meibua.
heko Wallah Bin Wallah,kiswahili kukikuza.

fani kote unatamba,si ngeli si mashairi.
jahazi haliwezi yumba,kiwa ndani wabashiri.
kiswahili wakipamba,kwa lugha isiyo shari.
Heko Wallah Bin Wallah,Kiswahili kukikuza.

kituo pia 'meunda,Wasta jina twajuwa.
huku sarufi walinda,lugha isiyo mawewa.
tuite tule matunda,kitujalia Moliwa.
Heko Wallah Bin Wallah,Kiswahili kukikuza.

mwalimu tunakujua,watajika jumuia.
ushambenga ushatoa,hekimani meingia.
twakuombea Jalia,siha kukuzidishia.
heko Wallah Bin Wallah,Kiswahili kukikuza.

Mshairi nasimama,haya machache yatosha.
Guru wetu Tumwandama,vichwa apate kuosha.
atujaze na hekima,Guru hawezi boesha.
Heko Wallah Bin Wallah,Kiswahili kukikuza.

Kaditamati shairi,kalamu chini natia.
isimu ndimi Omari,mwana zack maridhia.
wasomi namba kwaheri,Mstahiki hufwatia.
Heko Wallah Bin Wallah,Kiswahili kukikuza.

UTUNZI WA.
SAUTI YA BABU.
MSTAHIKI ZACK.
INSHAALLAH.

walimu

Posted by alex - Sep 25, 2015


Black tall about 5
34fts. I like kiswahili and I teach kiswahili kwa while za upili.

Kiswahili

Posted by Dennis yusuf - Sep 16, 2015


Jinsi ya kupita kiswahili

Eleza sera ya lugha nchini Kenya na nafasi ya Kiswahili.

Posted by andrew mathias - Sep 04, 2015


Eleza sera ya lugha nchini Kenya na nafasi ya Kiswahili.

serikali ya ugatuzi

Posted by julius - Aug 30, 2015


faida zake ni mingi