Jukwaa La Kiswahili

Karibu kwenye jukwaa letu la Kiswahili

SWALI

Posted by Oso Oliver - Jul 29, 2015


Onyesha kishazi huru na tegemezi katika sentesi hii:
Anamolala mna viroboto wengi

PENDEKEZO

Posted by Oso Oliver - Jul 29, 2015


Ningependa kuwa na jinsi ya kuuliza maswali na kupata majibu kwa urahisi. Ahsante

Pendekezo

Posted by Maulid - Jul 26, 2015


Ninapendeke kuweko na uwezekano wa kuhariri(to edit) au kufuta (to delete) maoni ambayo tunayaandika katika sehemu ya maoni baada ya kuyatuma kwani unaweza unataka kubadilisha sehemu katika maoni yako lakini haiwezekani. Ahsanteni

riwaya

Posted by GEOFFREY - Jul 24, 2015


NGURUWE HUCHAGUA ALIYENONA. Kauli hii inadhihirika
hivi: Wakoloni
walikuja afrika na kustakimu nchi ya Tomoko ambako
waliendeleza ubepari.
Aidha, eneo la Sokomoko lilitengwa kuwa lao 'wazungu'.
Walinyakua
vipande vikubwa vya ardhi na kujiendeleza kiuchumi kwa
kupanda mimea
ambayo iliwafaidi wao. Aidha, waliishi katika majumba ya
kifahari yenye
kuezekwa vigae. Mtemi Nasaba Bora pia anarithi
mizungu ya kunyakua
mashamba. Analinyakua shamba la ekari 270 la Chichiri
Hamadi. Aidha
analinyakua shamba la akina Imani. Pia, analirithi kasri
la Majununi.
Aidha, anawateua watu wa nasaba yake na kuwapa kazi.
Anamringa Lowela na
kuendeleza mapenzi. Anampeleka Madhubuti kusoma
urusi. Aidha,
anamtafutia kazi nzuri jeshini. Balozi ni kibaraka wa
Mtemi. Anamsifu
ili ajinufaishe. Fao anamnyemelea mwanafunzi wake na
kumpachika mimba.
Amani na Imani wanaelekea Sokomoko kutafuta ajira.

kidagaa

Posted by GEOFFREY - Jul 24, 2015


\"BAADA YA DHIKI FARAJA\"
Imani-baada ya kuteseka mikononi mwa askari mwishowe
anarejeshewa mali yake na ya nduguze.
Amani-anaregeshewa hadhi yake kama mwandishi wa
kidagaa kimemwozea.
Dj-anapona baada ya kuumwa na mbwa.
Dora-ndoa yake inahuika baada ya Majisifu kubadilika.
Zuhura-anapata amani baada ya kuondokewa na Nasaba
Bora.
Wanasokomoko-wanapata amani baada ya viongozi
wabaya k.v Nasaba Bora kuondoka.
Amani-anapata nafuu baada ya kupigwa na Nasaba
Bora.
Wanawe Majisifu-wanapata mjakazi anayewajali(Imani)
japo kwa muda mfupi, na mwishowe jamii inaanza
kuwakubali.
Madhubuti-anakubaliwa na wanasokomoko baada ya dhiki
ya aibu na vitendo vya babake.
Majisifu-dhiki ya ulevi inaondoka na jamii inampa
heshima tena.