Jukwaa La Kiswahili

Karibu kwenye jukwaa letu la Kiswahili

usemi halisi, usemi wa taarifa.

Posted by GEOFFREY - Jul 23, 2015


USEMI HALISI NA USEMI WA TAARIFA
HOMABAY 2013
Andika katika usemi halisi
Wanzare alimwambia shangazi yake kuwa angekuwa
akienda kumtembelea kwake kila mwezi. (alama 3)
“Nitakuwa nikija kukutembelea kwako kila wiki,”
Wanzare alimwambia shangazi yake (4x ½ =3)
KHWISERO 2013
Geuza sentensi zifuatazo katika usemi wa taarifa (al.4)
(i) “Mabasi hayapiti hapa siku hizi , kuna nini” Mazrui
aliuliza
(ii) Karen: Tafadhali usiukanyage mguu wangu
Kadzo: Ah! Mbona niukanyage?
i) Mazrui alitaka kujua ni kwa nini mabasi yalikuwa
hayapiti hapo siku hizi.
ii) Karen alimsihi Kadzo asiukanyage mguu wake, naye
kadzo alishangaa ikiwa angemkanyaga.
LAIKIPIA-LECONET 2013
Andika katika usemi halisi. (alama 3)
Mama alinionya kuwa nilimokuwa nikichezea mlikuwa na
hatari.
Mama alimionya, “Unamochezea mna hatari.” (1/2 x 6 =
3)
“Unamochezea mna hatari,” mama alinionya.
KIBWEZI 2013
Andika sentensi ifuatayo kwa usemi wa taarifa. (alama
4 )
“Nataka ufikirie sana juu ya maisha yako ya ndoa.
Sitaki uishi maisha yasiyo na
mwelekeo.” Baba alinishauri.
Baba alinishauri nifikirie sana juu ya maisha yangu ya
ndoa kwa vile hangetaka niishi maisha
yasiyokuwa na mwelekeo.
MAKUENI 2013
Andika katika usemi halisi. (alama 3)
Mama alituarifu kuwa ingetupasa kwenda Nairobi baada
ya siku moja.
“ Itawapasa kwenda Nairobi kesho.” Mama alituarifu.
“ Kesho kutwa itawapasa kwenda Nairobi. ” Mama
alituarifu.
Mama alituarifu, “Itawapasa kwenda Nairobi kesho.”
Zozote 6 x ½ = alama 3
RABAI 2013
Andika sentensi ifuatayo katika usemi halisi
Mwalimu Mkuu alisema kwamba wote waliorudi shuleni
kuchelewa wangefanya mtihani mwingine kwa kuwa
wenzao walikuwa wamemaliza kufanya mtihani siku mbili
zilizopita.. (alama 2)
. Mwalimu mkuu alsema, “Nyote mliorudi shuleni
kuchelewa mtafanya mtihani mwingine maana wenzenu
walimaliza kufanya mtihani tangu juzi.” (Alama 3)
MATUNGULU 2013
Andika katika usemi halisi.
Mwalimu aliwaita wanafunzi na kuwaagiza wajitayarishe
kwani safari yao ingeng’oa
nanga alfajiri siku ambayo ingefuata. ( alama 2 )
“Wanafunzi nataka mjitayarishe kwani safari yenu
itang’oa nanga alfajiri ya kesho.”
Mwalimu akawaagiza wanafunzi. 2 x 1 = 2
NDHIWA 2013
Andika kwa usemi halisi: (al. 3)
“Lo! Uliweza kuubeba mzigo huu jana peke yako!’’ Tajiri
alishangaa
Tajiri alishangaa kuwa niliweza kubeba mzigo huo pekee
yangu.
KIHARU 2013
Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa.
(alama 3)
“Mimi nitawakaribisha wageni leo jioni. Kisha nitaondoka
kwenda kwangu kesho.”
Fatuma alimwambia Juma.
Fatuma alimwambia Juma kuwa yeye angewakaribisha
wageni siku hiyo
jioni kisha angeondoka kwenda kwake siku iliyofuata. (6
x ½) = 3
NANDI YA KATI 2013
Andika sentensi hii iwe katika usemi halisi. (alama 2)
Mwashigadi alimwambia shangazi yake kuwa angempokea
mjomba iwapo angempata.
“Nitampokea mjomba iwapo nitampata,” Mwashigadi
alimwambia shangazi yake. (alama 2)
SUBUKIA 2013
Andika kwa usemi wa taarifa. (alama 2)
Madima alimwambia, \"Uasi unaotuonyesha ndio
utakaokuponza\".
Madima alimwambia kuwa uasi aliokuwa akiwaonyesha
ndio utakaomponza. Al 2
NANDI KASKAZINI 2013
Andika katika msemo wa taarifa. (alama 2)
“Naapa ya kwamba nitatumikia wananchi wa Kenya na
nitakuwa mwaminifu,” Rais Mteule alisema
Rais mteule aliapa√ / alisema ya kwamba / kuwa√
angetumikia√ wananchi wa Kenya na angekuwa√
mwaminifu. ( ½ x 4 = alama 2)
NANDI KUSINI – TINDIRET 2013
Andika kwa msemo wa taarifa, “Sitathubutu kumpa
kitabu changu.” Chesebe alisema. (alama2)
Chesebe alisema kuwa hangethubutu kumpa kitabu chake
(alama 2)
KASSU 2013
Andika katika usemi taarifa. (alama 4)
“ Mbona unamfanyia karaha mwenzako? Je, utaenda
kumwomba radhi?” Phanice aliuliza.
Phanice alimwuliza kwa nini alimfanyia karaha mwenzake
na akamwuliza kama angeenda kumwomba.
SUPAJET 2013
Andika katika msemo wa taarifa. (al 3)
“Nimeonewa,” mshtakiwa alilalamika, “sijashiriki ulevi
tangu mwaka jana!”
Mshtakiwa alilalamika kuwa alikuwa ameonewa na kuwa
hakuwa ameshiriki ulevi tangu mwaka uliotangulia. (al 3)
KCSE 2012
Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa.
“shughuli yetu itamalizika kesho,” mama alimwambia
Juma. (alama 2)
Mama alimwambia Juma kwamba(kuwa) √shughuli yao√
inge√malizika siku ambayo ingefuata√.

ELDORET MAGHARIBI 2012
Andika kwa usemi halisi. (alama 3)
Mwanamkuu alisema kuwa yeye alikuwa mfanyibiashara
maarufu katika mji huo.
Mwanamkuu alisema, “Mimi ni mfanyibiashara maarufu
katika mji huu”(6 x ½ = 3)
ELDORET MASHARIKI 2012
Andika kwa usemi halisi. (alama 3)
Njoroge alisema alikuwa amepata alama zoe katika
mjarabu wa siku ikiyotagulia.
“Nilipata ala zote katika mjaribu wa jana”
“Nilipata alama zote katika mjaribu wa jana! Njoroge
alisema. (al. 3)
KEIYO 2012
Geuza sentensi ifuatayo iwe katika msemo wa taarifa.
(alama 2)
“Nimepita kwake nyumbani lakini sikumwona ingawa
ameniahidi kwamba hataondoka.”
Ali alituarifu.
Ali alituarifu kuwa alipita kwake nyumbani lakini
hakumwona ingawa alikuwa amemwahidi kuwa
asingeondoka.
Kila kitahiniwa nusu alama) (al. 2)
TRANS-NZOIA 2012
Andika katika usemi taarifa. (Alama 2)
“Tutawatembelea wazazi wetu leo jioni” Leo alimwambia
Asha.
Leo alimwambia Asha kuwa wangewatembelea wazazi wao
siku hiyo jioni.
½ x4=Alama 2
KIPKELION 2012
Andika kwa usemi wa taarifa. (alama 3)
Mamboleo alilia, “Marafiki zangu, majambazi wamenipiga
na kunipora pesa zangu zote.
Hali yangu sasa ni mbaya.
Usemi wa taarifa.
- Mamboleo aliwalilia marafiki zake kuwa majambazi
walikuwa wamempiga na kumpora pesa zake zote na hali
yake wakati huo ilikuwa mbaya. ( ½ x 6 =3)
MBITA – SUBA 2012
Andika katika usemi wa taarifa. (alm2)
Je, tutazuru Mombasa lini? Aboi aliwauliza wanafunzi.
Aboi alitaka kujua kutoka kwa wanafunzi siku ambayo
wangezuru Mombasa.
KWANZA 2012
Andika katika usemi wa taarifa. (Alama 2)
“Nitakuja kesho asubuhi. Inshallah!” Bakari alisema.
Bakari alisema kuwa angekuja siku ambayo ingefuata.
Inshallah. ½ x4=2
BORABU MASABA 2012
Kangumu alisema “Masomo yetu yatakuwa rahisi mwaka
huu hivyo hatutaumia sana.” Geuza kwa usemi wa
taarifa. (Alama 3)
Kangumu alisema kuwa masomo yao yangekuwa rahisi
mwaka huo hivyo hawangeumia sana. 6x ½ =Alama 3
BUNGOMA 2012
Andika katika usemi halisi
Waziri alisema kuwa wangepata tiba ya bure kama bunge
lingepitisha msuada huo.
(alama 2)
“Tutapata tiba ya bure ikiwa bunge litapitisha msuada
huu’’ Waziri alisema (AL 2)
KISUMU MASHARIKI NA KASKAZINI 2012
Andika kwa usemi halisi: (alama 3)
Yule mshukiwa aliyekamatwa na polisi alisema kuwa papo
hapo ndipo alipoficha ule mkufu.
Yule mshukiwa aliyekamatwa na polisi alisema, “papa
hapa ndipo nilipoficha huo mkufu.”
“papa hapa ndipo nilipoficha huo mkufu,” Yule mshukiwa
aliyekamatwa na polisi alisema.
(al.3)
KISUMU MASHARIKI NA KASKAZINI 2012
Andika katika usemi wa taarifa. (Alama 2)
“Karibu Bakari, tafadhali kaa”, Maimuna alisema.
“Asante, je, habari za nyumbani?” Bakari aliuliza.
Maimuna alimkaribisha Bakari na kumuomba/sihi akae
(naye) Bakari akamshukuru na
kumuuliza/kutaka kujua habari za nyumbani. (al.2)
OLOITOKITOK 2012
Andika katika usemi wa taarifa. (alama 4)
(i) “Njooni hapa!” baba akaamuru.
(ii) “Twende kwetu leo jioni”. Msichana alimwambia
mpenzi wake.
Baba alimwamuru aende hapo /pale/ alipokuwa 1X2
Msichana alimwambia mpenzi wake waende kwao siku hiyo
jioni. 1X2
TESO KUSINI 2012
Andika kwa usemi wa taarifa. (ala. 2)
‘‘’’Lo ! kumbe wazuri hawajazaliwa. ’’ Omari alisema
baada ya kumwona kisura huyo.
Omari alishangaa baada ya kuona kisura yule kuwa
wazuri hawakuwa wamezaliwa .
AU
Baada ya kumwona kisura Yule, Omari alishangaa kuwa
wazuri hawakuwa
wamezaliwa ( 1 x 2=2)
NANDI KASKAZINI 2012
Badilisha sentensi hii iwe katika usemi wa taarifa.
(alama 3)
“Juma njoo hapa, kesho utaenda kwake umwambie aje
huku kwetu Jumapili” baba alimwambia.
Baba alimwita Juma na kumtuma aende kwake siku
iliyofuatia ili amwarifu afike kwao siku ya Jumapili.
BURETI 2012
Andika sentensi ifuatayo katika usemi halisi;
Mtoto alisema kuwa angewatembelea kwao mwezi ambao
ungefuata. (ala.3)
``Nitawatembelea kwenu mwevi ujao,``mtoto alisema.
(1x2=.al.2)
NANDI KATI 2012
Andika sentensi hii kwa usemi wa taarifa. (alama 2)
“Sofia aliniletea nguo yake jana na nitaivaa kesho
nikienda Nairobi,” Fatuma alisema.
Fatuma alisema√ kuwa Sofia alikuwa amemletea√ nguo
yake siku√ iliyotangulia na angeivaa√ siku ambayo
ingefuata√ akienda √Nairobi. (6 x ½ = alama 3)
BUTULA 2012
Geuza katka usemi wa taarifa
“ Kwa nini unamrudi mtoto mdogo?” afisa wa maslahi ya
mototo aliuliza.
Afisa wa masilahi ya watoto alitaka kujua kilichomfanya
kurudi mototo mdogo
au
Afisa wa masilahi ya watoto aliuliza kilichomfanya
kumrudi mototo mdogo. 1 x 3 = Alama 3
Nakuru 2012
Geuza sentensi ifuatayo katika usemi halisi. (alama 3)
Mtoto alimwambia mwalimu kuwa hakuwa na kitabu cha
kusoma. Alimweleza kuwa kakake
angemnunulia kitabu hicho asubuhi ya siku iliyofuata.
Mtoto alimwambia mwalimu, “ Sina kitabu cha kusoma.
Kakangu ataninunulia kesho
asubuhi. “ ½ X 6 = (alama 3)
BUSIA 2012
Geuza sentesnsi hizi ziwe katika usemi halisi ( ala. 4)
i) Mwenye hoteli alitaka kujua jumla ya vikombe vya chai
tulivyohitaji.
ii) Mtoto alisema kuwa angewatembelea kwao mwezi
amabo ungefuata.
(i) “Mtahitaji vikombe vingapi vya chai?” √√ Mwenye
hoteli alituuliza. (1x2=al.2)
(ii) √ √ “Nitawatembelea kwenu√ mwezi ujao√,”
√mtoto alisema. (1x2=al. 2)
Muungano 2012
Andika kwa msemo halisi (alama 3)
Ng’oa kisiki hiki haraka askari akaamrisha mahabusu
Ngoa kisiki hiki haraka!”Askari akaamrisha mahabusu
Meru kati 2012
Andika katika usemi wa taarifa. (alama 4)
‘Nitakuja kwenu kesho na nitaandamana na rafiki
yangu.” alisema
Alisema kuwakwamba ageenda kwao siku iliyofuata na
ageandamana na rafiki yake
(8 x ½ = 4)
Mbooni magharibi 2012
Andika katika usemi halisi
Mshauri aliwasisitizia watoto kuwa kulikuwa na umuhimu
kuwatii wazazi wao kwani hili linaongeza siku zao
duniani. (alama2)
“Kuna umuhimu kuwatii wazazi wenu”,Mshauri
aliwasisitizia watoto”.Hili litaongeza siku zenu duniani”.
Alama 2
Mbooni mashariki 2012
Andika katika msemo wa taarifa.
Mzazi: Kesho nataka ufike nyumbani mapema,unasikia?
Mtoto: Nitajaribu,lakini mwalimu alisema tutafanya
mtihani jioni. (alama 4)
Mzazi alitaka mtoto afike nyumbani mapema siku
iliyofuata, kasha akamwuliza kama alikuwa amyasikia
hayo aliyoambiwa.Mtoto akajibu kuwa angejaribu
kufanya hivyo lakini mwalimu alikuwa amesema wao
wangefanya mtihani jioni ya siku hiyo. (4 x 1 = 4)
Yatta 2012
Andika kwa msemo wa taarifa. (alama. 3)
“Lo! Umeweza kuubeba mzigo huu pekeyo?” Mama
Alishangaa.
Mama alishangaa kuwa aliweza kuubeba mzigo huo peke
yake. (al.3)
Kitui kati 2012
Andika kwa usemi wa taarifa. (Alama 2)
“Lo! Kumekucha mara moja hii?” Alisema mgeni.
Mgeni alishangaa kuwa / kwamba kulikuwa kumekucha
mara moja hiyo (jumla =2)
Kilungu 2012
“Sitaki na sitataka mwanafunzi mkaidi kama wewe.”
Mwalimu mkuu alisema.Andika usemi wa taarifa.
Mwalimu mkuu alisema kuwa hakutaka na hangetaka
mwanafunzi mkaidi kama yeye.
(4 x1/2 = alama 2)
Embu 2012
Andika katika usemi wataarifa.
\"Mimi nitawakaribisha wageni leo jioni kisha nitaondoka
kwenda kwangu kesho.\" Fatuma alimwambia Juma .
(alama 3)
Fatuma alimwambia Juma kuwa yeye angewakabirisha
wageni siku hiyo jioni kisha angeondoka kwenda kwake
siku iliyofuata. (alama6 x ½= 3)
Kathiani 2013
Geuza sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa ( alama
3)
Katune: Tafadhali usiukanyange mguu wangu.
Muti: Ah! Mbona niukanyange?
Katune alimshawishi Muti asiukanyange mguu wake naye
Muti akashangaa kwa nini aukanyange. (alama 3)
Kassu 2012
Andika katika usemi wa taarifa: (al 2)
“Leo ni Leo,” mchezaji mmoja akasema, “Aliyesema
atafanya kesho ni mwongo”.
Mchezaji mmoja alikariri kuwa siku hiyo ilikuwa ni iyo
hiyo na aliyesema angefanya siku
iliyofuata alikuwa mwongo. (al 2)
Kakamega kati 2012
Andika katika usemi wa taarifa. (alama 4)
(i) “Njooni hapa!” baba akaamuru.
(ii) “Twende kwetu leo jioni”. Msichana alimwambia
mpenzi wake.
Baba aliwaamuru waende hapo /pale/ alipokuwa 1X2
Msichana alimwambia mpenzi wake waende kwao siku hiyo
jioni.1X2
Baringo 2012
Andika katika usemi halisi
Katibu alitangaza kuwa kungekuwa na mkutano wa
wanachama wote ambao walikuwa wamesajiliwa mwezi
huo Jumanne iliyofuata. (alama 3)
“ Kutakuwa na mkutano wa wanachama wote ambao
wamesajiliwa mwezi huu
Jumanne inayofuata”, katiba alitangaza (6 X ½ = 3)
Thika 2011
Andika katika usemi wa taarifa. (alama3)
“Ahh! Unadhani atakupenda nani ikiwa mawazo uliyo
nayo ni haya ya karne nyingi zilizopita”, alisema samiji.
Samiji alishangaa nani ambaye angempenda ikiwa mawazo
aliyokuwa nayo yalikuwa kama hayo ya karne nyingi
zilizopita. (alama3)
Busia 2011
Geuza sentesni hizi ziwe katika usemi halisi ( ala. 4)
i) Mwenye hoteli alitaka kujua jumla ya vikombe vya chai
tulivyohitaji.
ii) Mtoto alisema kuwa angewatembelea kwao mwezi
amabo ungefuata.
(i) “Mtahitaji vikombe vingapi vya chai?” √√ Mwenye
hoteli alituuliza. (1x2=al.2)
(ii) √ √ “Nitawatembelea kwenu√ mwezi ujao√,”
√mtoto alisema. (1x2=al. 2)
Kakamega Mashariki 2011
Andika kwa usemi wa taarifa. (al.3)
Mamboleo alilia, “Marafiki zangu, majambazi wamenipiga
na kunipora pesa zangu zote. Hali yangu sasa ni mbaya”.
- mamboleo aliwalilia marafiki zake kuwa majambazi
walikuwa wamemupiga na
kumpora pesa zake zote na hali yake wakati huo ilikuwa
mbaya. ( ½ x 6 = 3 )
Kisumu Magharibi 2011
Andika senetesni hii kwa mseno wa taarifa.
“ Mtaweza kuubeba mtungi huu peke yenu?” Maile
alishangaa. ( ala. 3)
Miale alishangaa kama tungeweza kuubeba mtungi pekee
yetu. (al. 3)
Kitui Magharibi 2011
Andika katika usemi wa taarifa.
“Tutakwenda kanisani kesho kutwa.” Zawadi alisema.
(Alama 2)
Zawadi alisema kuwa wangeenda kanisani siku mbili
zilizofuata (al. 2 )
Machakos 2011
Andika sentensi hii katika usemi halisi
Mjomba alisema angesafiri kwenda Dubai alasiri hiyo.
( alama 3 )
“ Nitasafiri kwenda Dubai leo alasiri.” Mjomba alisema.
Alama 3
Mumias 2011
Andika katika usemi wa taaarifa.
“Mkiendelea na tabia hiyo yenu, huenda msifanye vizuri
katika mtihani” Mwalimu aliwaonya watahiniwa.
Mwalimu aliwaonya watahiniwa kuwa wangendelea na
tabia hiyo yao huenda hawangefanya
vizuri katika mtihani.
Mutomo 2011
Andika sentensi hii kwa usemi wa taarifa (alama 2)
“Lo! Kube wazuri hawajazaliwa,” Omari alisema baada ya
kumwona kisura huyo.
Omari alishangaa baada ya kuona kisura yule kuwa
wazuri hawakuwa wamezaliwa
Baada ya kumwona kisura yule, Omari alishangaa kuwa
wazuri hawakuwa
wamezaliwa
Ndhiwa 2011
Andika kwa usemi wa taarifa.
“Hivi vibanda vilivyo kando ya shule yetu vinatumiwa
kulanguzia dawa za kulevya” Mwalimu mkuu alilalamika.
(Alama 3)
Mwalimumkuu alilalamika kuwa hivyo vibanda vilivyoiuwa
kando ya shule yao vilikiwa viatumike kulanguzia dawa
za kulevya. Alama 3
Nyamira 2011
Andika kwa msemo wa taarifa: (ala. 4)
“Rudi darasani,” mwalimu aliamuru mwanafunzi kisha
mwanafunzi akamjibu “ nitarudi tu ikiwa utanihakikishia
usalama wangu”
Mwalimu aliamuru mwanafunzi kurudi darasani kisha
mwanafunzi akamjibu kuwa angerudi Ikiwa
angehakikishiwa usalama wake (al. 4)
Rachuonyo 2011
Andika kwa msemo wa taarifa. (ala. 3)
“Lo! Umeweza kuubeba mzigo huu pekeyo?” Mama
Alishangaa.
Mama alishangaa kuwa aliweza kuubeba mzigo huo peke
yake.
Sotik 2011
Andika kwa msemo wa taarifa (al. 3)
“Mimi nitawakaribisha wageni leo jioni kisha nitaondoka
kwenda kwangu kesho” Fatuma alimwambia Juma.
Fatuma alimwambia Juma kuwa yeye angemakaribisha
wageni siku hiyo jioni kisha
angeondoka kwenda kwa ke siku iliyofuata. (6 x ½ = al.
3)
Baringo 2011
(d) Andika katika usemi halisi.
Kiptoo alimwambia shangazi yake kuwa angekuwa
akienda kumtembelea kwake kila wiki. (alama 3)
“Nitakuwa nikija kukutembelea kwako kila wiki,” Kiptoo
alimwambia shangazi yake.
(Vitahiniwa 6 x ½ = alama 3)
Kakamega 2010
Andika katika usemi wa taarifa : (al. 2)
“Karibu Rahma, tafadhali kaa,” Musa akasema . Ahsante,
je, habari za hapa?’ Rahma aliuliza
Musa alimkaribisha Rahma na kumsihi akae,Rahma
alishukuru na kumuuliza habari za pale.
Bondo 2008
Andika sentensi ifuatayo katika usemi halisi
Wakili alimtahadharisha mshukiwa kwamba asingemwarifu
ukweli wote kuhusu kesi hiyo asingemwakilisha (alama 2)
“ Usiponiarifu ukweli wote kuhusu kesi hii sitakuwakilisha
,“ wakili alimtahadharisha mshukiwa (8x ¼ =2
SIAYA UGENYA 2009
Andika upya katika usemi wa taarifa. (alama 2)
Achieng: Mbona umekuja kunitembelea leo?
Otieno: Nina nia ya kukuletea posa kutoka kwa Owino.
-Achieng alitaka kujua sababu ya Otieno kumtembelea
siku hiyo, naye akajibu kuwa alikuwa na nia ya
kumpelekelea posa kutoka kwa Owino.
MSURURU WA TOP STUDENT 2009
Badilisha sentensi hizi hadi usemi wa taarifa
(i) “Nitarudi tu ikiwa mtakubali kuomba msamaha.” Juma
alisema. (alama 2)
(ii) “Elezeni vile mlivyokuja hapa na namna
mtakavyokwenda.” Mwalimu mkuu
alisema (alama 3)
(i) Juma alisema ya kuwa / kuwa / ya kwamba / kwamba
angerudi tu ikiwa / kama
wangekubali kuomba msamaha. (Alama 2)
(ii) Mwalimu Mkuu aliwataka / aliwaambia waeleze vile
walivyoenda hapo na namna
wangeenda / watakavyoenda.
KCSE 2006
Andika katika msemo wa taarifa.
“Sitathubutu kumpa pesa zangu” Mkolwe alisema. (alama
2)
Mkolwe alisema yakwamba hangethubutu kumpa pesa zake
Mkolwe alisema ya kwamba ya kwamba/ kuwa
asingethubutu kumpa pesa
KCSE 2004
(a) Andika kifungu hiki kutoka usemi wa taarifa hadi
usemi halisi
( alama 4)
Watoto waliambiwa na mama yao watakaporudi nyumbani
waoge. Wale, halafu waanse kusoma moja kwa moja
badala ya kuharibu wakati wao kwa kutazama vipindi vya
runinga. Aliwakumbusha kuwa wanaofanya maonyesho
kwenye runinga tayari wamefuzu shuleni na wameajiriwa
kazi
Mama aliwaambia watoto wake “ mtakaporudi nyumbani
muoge, mle halafu muanze kusoma moja kwa moja badala
ya kuharibu wakati wenu kwa kutazama vipindi vya
runinga. Aliendelea kuwakumbusha wanaofanya
maonyesho kwenye runinga tayari wamefuzu shuleni na
wameajiriwa kazi. (Ijisehemu 14 anaweaz kuanzia
mtakaporudi muoge, mle….. (alama 4)

kinyume

Posted by GEOFFREY - Jul 21, 2015


KINYUME
BUNYORE MARANDA 2013
Andika kinyume:
Adui yake anameza chakula kwa pupa.
Adui yake anathema chakula taratibu/halahala/asteaste/
polepole
Akibadili nomino atuzwe 0
MAKUENI 2013
Andika sentensi ifuatayo katika hali ya kinyume. (alama
2)
Wanafunzi waliombwa watawanye punje zote.
Waliombwa - walilazimishwa / walishurutishwa
Watawanye – wakusanye
RABAI 2013
Andika kinyume cha neno lililopigwa mstari.
Kamau amehama mjini. (alama 1)
Hamia Amelowea/ Ameselea 1x1 = alama 1
KIHARU 2013
Andika kinyume cha sentensi hii. (alama 1)
Babu alikashifiwa kwa vitendo vyake.
Babu alisifiwa kwa vitendo vyake. (1 x 1) = 1
NANDI ya KATI 2013
Andika kinyume cha sentensi ifuatayo. (alama 1)
Aliangika bendera baada ya kifo cha mfalme wao.
Aliangua bendera baada ya kifo cha mfalme wao. (alama
1)
SUBUKIA 2013
Andika kinyume. (alama 1)
Msichana huyu anapendeza kwa tabia yake nzuri
Msichana huyu hapendezi kwa tabia yake mbaya ½ x 2 =
1
NANDI KATI 2012
Andika kinyume cha sentensi hii. (alama 1)
Mvulana mmoja ameoa.
Mvulana mmoja ametalikiwa. (alama 1)
Iwapo ataandika msichana anyimwe ½ alama
MUUNGANO 2012
Andika kinyume cha sentensi ifuatayo. (alama 2)
Juma ameinjika chungu mekoni.
Ameepua/ Amedeua/Ametegua chungu mekoni
MBOONI MAGHARIBI 2012
Andika kinyume cha maneno yaliyopigiwa mstari (alama2)
Nyanya alikusanya kuni
(i) Nyanya
(ii) Tawanya Alama 2
KWANZA 2012
Andika kwa kinyume (Alama 1)
Kijakazi aliangika vyombo vya tajiri wake.
Kitwana aliangua vyombo vya tajiri wake 1x2=2
MBOONI MASHARIKI 2012
(a) Geuza sentensi zifuatazo ziwe katika hali ya kinyume
.
(i) Nyanya alisema baba alipoingia. (alama2)
(ii) Kitinda mimba ameaga dunia. (alama 2)
(i) Nyanya alinyamaza baba alipotoka.
(ii) Kitinda mimba amezaliwa. (2 x 2 = 4)
KIISUMU MASHARIKI NA KASKAZINI 2012
Andika sentensi ifuatayo ukitumia kinyume cha neno
lililoandikwa kwa herufi ya mlazo: (alama 1)
Binadamu hawezi kumuumba mwenzake.
Binadamu hawezi kumuumba mwenzake (alama 1)
(akipata kitahiniwa bila kutunga sentensi – al.½)
KIPKELION 2012
Andika kinyume cha kitenzi kilichopigiwa mstari. (alama
1)
Alikashifiwa kwa kazi aliyofanya.
- Alisifiwa kwa kazi aliyofanya. (1)
OLIOTOKITOK 2012
Andika kunyume cha: (alama 2)
Baba alimbariki mwanawe mtiifu.
Baba alimlaani mwanawe muasi
MBITA-SUBA 2012
Tumia vinyume vya maneno yaliyopigiwa mistari katika
sentensi ifuatayo. (alm2)
Fundi alishona surupwenye aliyouza sokoni.
Fundi alishonoa surupwenye aliyonunua sokoni.
KITUI KATI 2012
Andika kwa kinyume. (Alama 2)
Kulia huku kwa mtoto kunakasirisha sana.
Kucheka1 huku kwa mtoto kunafurahisha 1 sana
Kilungu 2012
Andika kinyume
Chakula hiki kitamu nitakimeza. (alama1)
Chakula hiki kichungu nitakitema. (alama 1)
Kathiani 2012
Andika kinyume cha sentensi (alama 2)
Walipakia vyombo jahazini walipolewa.
Walipakua vyombo jahazini walipolevuka. (alama 2)
Kakamega kati 2012
Andika kunyume cha: (alama 2)
Baba alimbariki mwanawe mtiifu.
Baba alimlaani mwanawe muasi
Baringo 2012
Andika kinyume cha sentensi hii.
Wavuvi walizama walipoenda kukusanya majani mabichi.
(alama 2)
Wavuvi walielea walipoenda kutawanya majani mabichi
(alama 2)
Kakamega Kati 2011
Tunga sentensi ukitumia kinyume cha kitenzi: ‘umba’ (al.
2)
Mungu ndiye aliye na uwezo wa kuumba na kuumbua
Kakamega Mashariki 2011
Andika kinyume cha kitenzi kilichopigiwa mstari. (al.1)
Alikashifiwa kwa kazi aliyofanya.
Kinyume
Alisifiwa kwa kazi aliyofanya. (1)
Machakos 2011
Kamilisha sentensi hii kwa neno lililo kinyume na
lililopigiwa mstari.
(i) Maji yameganda huwezi ( alama 1 )
Kuyayeyusha 1 x 1 = 1
Ndhiwa 2011
Andika kwa kinyume (Alama 1)
Hii ni njia nyembamba
Hii ni njia pana Alama 1
THIKA 2011
Andika upya sentensi ifuatayo ukitumia vinyume vya
maneno yaliyopigiwa mstari.(alama2)
Msichana aliyevaa nguo tawili, alitwezwa na wenzake.
Tawili - Fupi (alama2)
Tweza - Heshimu
MSURURU WA TOP STUDENT 2009
Andika kwa kinyume:
(i) Nje kulikuwa kweupe. (alama 1)
(ii) Mzizimo (alama 1)
i) Ndani kulikuwa kweusi. (alama 1)
(ii) Mzizimo - ari au fukuto. (alama 1)
KCSE 2006
Andika kinyume cha:
Mwise alikunja nguo alizokuwa ameanika (alama 2)
Mwise alikunjua nguo alizokuwa ameanua

Ngeli

Posted by GEOFFREY - Jul 21, 2015


NGELI ZA NOMINO
HOMABAY 2013
Nomino hizi ziko katika ngeli gani (alama 2)
Ushuru
Maktaba
i) U-U
ii) U-I
BOMET 2013
Nomino zilizopigiwa mstari ni za ngeli gani? (al.2)
(i) Nyumba ya rafiki imeanguka.
(ii) Nipatie kiatu cha mama na ubwabwa wa mtoto.
(i) Nyumba (Ngeli ya I – ZI); rafiki (Ngeli ya A – WA) (½
x 4 = 2)
(ii) Kiatu (Ngeli ya KI-VI), Ubwabwa (U-U)
KIBWEZI 2013
Tunga sentensi ukitumia nomino ya ngeli ya I – I pamoja
na kionyeshi cha mbali. (alama 2 )
Sentensi zote zizingatie upatanisho wa kisarufi wa ngeli
ya I – I. k.m
Chumvi ile itatumiwa kesho.
KIBWEZI 2013
Tumia shina la kimilikishi cha nafsi ya tatu wingi pamoja
na ngeli ya LI – YA
kutunga sentensi.
Mf. meno yao yanauma n.k
MAKUENI 2013
Tumia maneno yafuatayo kutungia sentensi ili
kudhihirisha ngeli zake. (alama 4
(i) Marashi
(ii) Sabuni
(i) Marashi – YA - YA
(ii) Sabuni – I – ZI
Sentensi zidhihirishe matumizi ya ngeli hizo.
Kutambua na kutoa mfano – alama 2 x 2 = 4
KIKUYU 2013
Tunga sentensi inayodhihirisha matumizi ya ngeli ya U -
U. (alama 1)
atunge sentensi akitumia nomino za ngeli hii kama vile
ujeuri, uroho, usafi, ujana, ulaghai,
udhia, mchanga, ujinga, uchawi, uji, ugoro, uadilifu.
n.k.
Mfano; ujeuri wake ulimfanya aadhibiwe.
uvivu unarudisha maendeleo nyuma. (alama 1)
KHWISERO 2013
Andika nomino mbili katika ngeli ua U-YA (al.2)
i) ugonjwa
ii) ulezi n.k
MARANDA- BUNYORE 2013
Weka nomino shingo katika ngell yake mwafaka
I-ZI
KIRINYAGA 2013
Nomino hizi hupatikana katika ngeli zipi? (alama 2)
(i) Vita
(ii) Dunia
Vita – VI
Dunia - 1 – 1 (2 x 1)
NANDI KUSINI TINDERET 2013
Onyesha umoja au wingi wa ngeli za nomino zifuatazo.
(alama 2)
(i) Bawabu
(ii) Nyasi:
(i) bawabu – mabawabu A – WA (alama ½ wingi, ½ ngeli).
(ii) Nyasi – unyasi U – ZI (alama ½ umoja, ½ ngeli)
SUBUKIA 2013
1. Yaweke maneno haya katika ngeli zake. (alama 2)
i) Uyoga
ii) Majeruhi
iii) Chango
iv) Mali
. uyoga- U- U
Majeruhi – A-WA ( ½ X 4 = 2)
Chango- U-ZI
Mali- YA- YA
SUPAJET 2013
Neno muundi liko katika ngeli gani? (al1)
Ngeli ya U – I (al 1)
KASSU 2013
Tunga sentensi moja ukitumia kirejeshi kisisitizi cha
karibu katika ngeli ya LI – YA
umoja.
mfano: Lili hili litatupwa alama 2
KIKUYU 2013
Tunga sentensi inayodhihirisha matumizi ya ngeli ya U -
U. (alama 1)
Mwanafunzi atunge sentensi akitumia nomino za ngeli hii
kama vile ujeuri, uroho, usafi, ujana, ulaghai,
udhia, mchanga, ujinga, uchawi, uji, ugoro, uadilifu.
n.k.
Mfano; ujeuri wake ulimfanya aadhibiwe.
uvivu unarudisha maendeleo nyuma. (alama 1)
ELDORET MAGHARIBI 2012
Nomino hizi ziko katika ngeli zipi? (alama 2)
i) Sisimizi
ii) Marashi
A - WA
YA – YA
ELDORET MASHARIKI 2012
Maneno yafuatayo yanapatikana katika ngeli gani.
(alama 2)
i) Karakana
ii) Mamluki
i) Karakana – I-ZI
ii) mamluki – A - WA (al. 2)
LOITOKTOK 2012
Maneno haya yako katika ngeli gani? (alama 2)
(i) Karatasi
(ii) Nyasi
Karatasi - I – ZI
Nyasi - ZI (U – ZI)
KERICHO 2012
Andika mifano mitatu tofauti ya Nomino katika ngeli ya
U-ZI. (al.3)
Umoja Wingi
Ulimi ndimi
Ukuta kuta
Unywele nywele
Ubeleko mbeleko (zozote 3 ½ x6=3)
KERICHO 2012
Tunga sentensi ukitumia viambishi ngeli vya maneno
haya. (al.2)
(i) Mjusi
(ii) Mali
Ngeli
Mjusi – A – WA
Mali – YA – YA
KIPKELION 2012
Andika viwakilishi vya ngeli vya nomino zifuatazo; (alama
2)
i) Amri (umoja)
ii)Kwetu
Viambishi vya ngeli.
Amri (umoja) 1 (al. 1)
Kwetu KU (al. 1)
BORABU MASABA 2012
Weka nomino katika ngeli zao. (Alama 2)
i) Kitwana
ii) Maradhi
i) A-WA
ii) YA-YA
2x1=Alama 2
BORABU MASABA 2012
Nomino katika ngeli ya U-ZI huchukua maumbo tofauti
katika umoja na wingi. Tetea
kauli hii kwa mifano yoyote minne. (Alama 4)
i) Baadhi ya Nomino huanza na u ambayo hutoweka kwa
wingi k.m
ukuta-kuta
ii) Mengine huanza na U-Ny k.m
Uta-Nyuta
iii) Mengine huanza na U-Nd k.m
Ulimi-Ndimi
iv) Mengiine huanza na U-Mb k.m
Ubao-Mbao
v) Mengine huanza na U k.m
Wembe, wimbo n.k
Zozote 4x1=alama 4
(Maelezo= ½ , Mfano= ½ )
KCSE 2012
Tumia kivumishi kionyeshi kisisitizi cha karibu pamoja na
nomino katikka ngeli ya
YA-YA (alama 2)
Mafuta yaya haya yameuzwa
Marashi yaya haya ndiyo yanayonukia
Yaya haya ndiyo maji ya uzima
KISII KUSINI 2012
Nomino ‘huruma’ i katika ngeli gani? ala 1
Ngeli ya I—I 1 × 1
MERU KATI 2012
Tumia nomino zifuarazo kutungia sentensi ili kudhihirisha
ngeli ya kila mojawapo. (alama 4)
i) Kusoma ii) Udhalimu
i) kitezi jina (Ngeliya ku) mf. kusoma
kwake kulimletea mafanikio
ii) Ngeli ya U-U mf- Udhalimu wa viongozi
haufai katika nchi huru (alama 2 x 2= 4)
BUTULA 2012
Tunga sentensi kubainisha ngeli ya jina hili chetezo.
(al.2)
Chetezo kimepotea Ngeli ya Ki – VI 2 x 1 = Alama 2
KWANZA 2012
Taja ngeli za majina yafuatayo (Alama 2)
Uga
Kiroboto
Unga-U-ZI
Kiroboto -A-WA
1x2=2
MBOONI MAGHARIBI
Tunga sentensi itakayobainisha matumizi ya ngeli ya I-
ZI (alama1)
Mifano ya maneno katika ngeli
I - ZI
Meli
Mbari
Bahasha n.k.
M.f Meli imezama 1/2

santensi

Posted by GEOFFREY - Jul 21, 2015


SENTENSI YA KISWAHILI NA AINA ZAKE ( KIRAI , KIIMA
(KN),KIARIFA(KT),SHAMIRISHO, VISHAZI, NA CHAGIZO)
HOMABAY 2013
Tambua shamirisho na chagizo katika sentensi ifuatayo
(alama 2)
Mama alipika chakula kitamu
Shamirisho - chakula.
Chagizo - kitamu
HOMABAY 2013
Onyesha vishazi tegemezi na vishazi vikuu katika
sentensi ifuatayo. (alama 2)
Nilimwona Agwambo nilipofika Mombasa
Nilimwona Agwambo - kishazi huru.
Nilipofika Mombasa - kishazi tegemezi.
MATUNGULU 2013
Ainisha vishazi.
Mjapo kwangu mtanikuta. (alama 2 )
Mjapo kwangu – kishazi tegemezi.
Mtanikuta – Kishazi huru. 2 x 1 = 2
BOMET 2013
Tunga sentensi tatu ili kuonyesha ‘chagizo’ (al. 3)
(a) (i) Wanafunzi hawa watasafiri ng’ambo wiki tatu
zijazo.
(ii) Kina mama watanunua mifugo wengi kwelikweli.
(iii) Sote tuliamka asubuhi na mapema. (1 x 3)
BOMET 2013
Onyesha shamirisho kwenye sentensi zifuatazo: (al.2)
(i) Mkulima alivuna mahindi mengi
(ii) Nataka maji moto
(i) Mkulima alivuna mahindi mengi.
(ii) Nataka maji moto.
BOMET 2013
Huku ukitoa mfano mmoja mmoja, eleza maana ya virai
vifuatavyo. (al.4)
(i) Kirai – nomino
(ii) (ii) Kirai – vumishi
(a) Kirai ambacho neno kuu ni nomino. Kwa mfano:
(i) Wanafunzi wa shule yetu wana bidii sana.
(ii) Kirai ambacho neon kuu ni kivumishi. Kwa mfano:
Baiskeli ishirini za rangi ya kijani kibichi zitatumiwa
kwenye mashindano hayo.(2 x 2)
RABAI 2013
Bainisha shamirisho katika sentensi hii
Nilimnunulia mwanangu kitabu kwa marupurupu
niliyopata. (alama 3)
Mwanangu – kitondo
Kitabu- kipozi
Marupurupu- ala Alama 3
MATUNGULU 2013
Fafanua sifa mbili kuu za sentensi ambatano. (alama 2 )
(i) Huundwa kwa muungano wa sentensi mbili sahihi.
(ii) Huundwa kwa matumizi ya viunganishi / alama
mbalimbali za kuakifisha.
2 x 1 = 2
MARANDA BUNYORE 2013
Huku ukitoa mifano,taja miundo yoyote mitatuya kiima.
N - Omari anakula/N + U+ N -baba na babu ni wakalu
N+ V -Kuku yule anataga/ W- Yeye ni Omari.
N+H+N — Watoto wa Ziari ni wakorofi.
N + S - Mtoto aiiyekuja jana ni huyu.
MATUNGULU 2013
Bainisha aina za virai.
Walimshangilia kwa shangwe. (alama 2 )
Walimshangilia – Kirai tenzi; Kwa shangwe – Kirai elezi 2
x 1 = 2
KIBWEZI 2013
Onyesha shamirisho kipozi katika sentensi zifuatazo.
(alama 2 )
(i) Kijana amenunua baiskeli.
(ii) Ruth ameandika kitabu.
- Baiskeli
- Kitabu
KIBWEZI 2013
Andika sentensi ambatano kutokana na sentensi sahihi
zifuatazo. (alama 2 )
- Rehema ni mtoto mchangamfu.
- Rehema huwa nadhifu kila mara.
- Rita ni msichana mchafu.
Rehema ni mtoto mchangamfu na huwa nadhifu kila mara
ilhali / lakini Rita ni msichana mchafu.
MAKUENI 2013
Onyesha shamirisho kitondo, kipozi na ala katika sentensi
ifuatayo. (alama 3 )
Kamau alimbebea mzazi mzigo kwa gari.
Kipozi - mzigo
Kitondo – mzazi
Ala – kwa gari Kila moja alama 1 alama 3
KIHARU 2013
Fafanua maana ya kirai, kisha utunge sentensi sahihi
ambayo haina nomino kuonyesha
kirai nomino.
Kirai – Kundi la maneno ambalo halina muundo wa kiima –
kiarifu.
K.m. Sisi/yeye/wao hutembea usiku.
Tanbihi: Sehemu ya KN isiwe na nomino bali iwe na
kiwahilishi (2 x 1) = 2
KIHARU 2013
Bainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
Mwita alimtumia babake barua kwa posta.
(i) Barua - Kipozi
(ii) Babake - Kitondo
Posta - Ala (3 x 1) = 3
LIKIPIA – LENOCET 2013
Bainisha aina za vishazi katika sentensi. (alama 2)
Wakilipa deni la mkopo watarejeshewa mali yao.
Wakilipa deni la mkopo - kishazi tegemezi (2 x 1 = 2)
Watarejeshewa mali yao - kishazi huru.
LIKIPIA – LENOCET 2013
Ainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
Mwalimu alisoma barua aliyoandikiwa mwanafunzi.
Kipozi - barua (1 x 1 = 1)
Kitondo - mwanafunzi (1 x 1 = 1)
NDHIWA 2013
Bainisha aina za shamirisho katika sentensi hii:- (al. 3)
Mwanariadha ameandikiwa cheti kwa wino na
mwenyekiti:-
Mwanariadga ___ Shamirisho kitondo
Cheti_____ Shamirisho kipozi
Wino ____ Shamirisho ala / kitumizi 3x 1 3
NDHIWA 2013
Onyesha vishazi katika sentensi:- (al. 2)
Ijapokuwa alifafanua hakuelewa alichomaanisha.
Hakuelewa alichoanisha ____ kishazi huru (alama 1)
Ijapokuwa alitafafanua ____ kishazi tegemezi (alama1)
NYANDO 2013
Tunga sentensi moja na uonyeshe sehemu zifuatazo kwa
kupiga mstari (alama3)
a. shamirisho kipozi
b. shamirisho kitondo
c. shamirisho ala
mama alimpikia baba chakula kwa gesi
kitondo kipozi ala (1x3=alama 3)
NYANDO 2013
Onyesha aina za vishazi katika sentensi ifuatayo
(alama2)
Mkulima alipoenda shambani, alivuna mazao.
Mkulima alipoenda shambani-tegemezi (1x1=alama1)
alivua mazao - huru (1x1=alama 1)
NANDI YA KATI 2013
Bainisha yambwa katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
Mgeni aliandaliwa chakula kitamu na mwenyeji wake kwa
sinia
Mgeni – yambwa tendewa
Chakula – yambwa tendwa.
Sinia – yambwa (alama 3)
NANDI KATI 2013
(i) Kishazi ni nini? (alama 1)
(ii) Kwa kutumia mfano mmoja wa sentensi, onyesha aina
za vishazi. (alama 2)
(i) Kishazi ni fungu la maneno lililo na kitenzi, huweza
kutoa maana kamilifu au lisitoe.
(ii) Mtoto aliyekuwa mgonjwa amepona.
tegemezi huru
NANDI KATI 2013
Onyesha kundi nomino na kundi tenzi katika sentensi
ifuatayo. (alama 2)
Mtoto aliyezaliwa jana jioni akilia ametushangaza mno.
KN KT
Mtoto aliyezaliwa jana jioni akilia ametushangaza.
(alama 2)
NANDI KASKAZINI 2013
Onyesha vishazi katika sentensi ifuatayo. (alama2)
Uchaguzi uliofanywa nchini Kenya ulikuwa wa amani.
a. Uchaguzi uliofanywa nchini Kenya – kishazi tegemezi.
b. Ulikuwa wa amani – kishazi huru.
(1 x 2 = alama 2)
NANDI KASKAZINI 2013
Bainisha aina za shamirisho katika sentensi: (alama 3)
Shule nzuri ilijengewa wanafunzi kwa matofali.
Shule nzuri ilijengewa wanafunzi kwa matofali.
1 2 3
1) Shamirisho kipozi – shule.
2) Shamirisho kitondo – wanafunzi.
3) Shamirisho ala – matofali. (1 x 3 = alama 3)
NANDI KASKAZINI 2013
Eleza sifa mbili za sentensi ambatano na utoe mfano
mmoja. (alama 3)
(i) Huwa na mawazo mawili au zaidi (vitenzi viwili).
(ii) Huwa na kiunganishi.
Mama anasoma kitabu lakini baba analala. (1 x 3 = alama
3)
NANDI KASKAZINI 2013
Eleza maana ya chagizo na utunge sentensi moja
kuonyesha maana yake.
(alama 2)
– Chagizo ni kielezi.
- Walienda ufuani mwa bahari au Wanafunzi walisoma
kwa makini.
NANDI KUSINI- TINDIRET 2013
Bainisha shamirisho kipozi, kitondo na ala katika sentesi
ifuatayo:
Mjakazi aliwapelekea wageni chakula kwa sinia. (alama
3)
Chakula – kipozi (alama 1)
Wageni – kitondo (alama 1)
Sinia – ala / kitumizi (alama 1)
NANDI KUSINI- TINDIRET 2013
Onyesha kishazi huru na kishazi tegemezi katika sentensi
ifuatayo.
Tulibeba maji ya kutosha tulipoenda safari Turkana.
(alama 2)
Tulibeba maji ya kutosha tulipoenda safari Turkana.
Huru tegemezi (al.1 tegemezi, al. 1 huru)
KIHARU 2013
Eleza maana ya dhana ya chagizo kisha uonyeshe kwa
kupigia mstari chagizo katika
sentensi ifuatayo: (alama 2)
Mtoto alitembea asteaste.
(i) Huelezea zaidi kuhusu kitendo (1 x 1) = 1
(ii) Mtoto alitembea asteaste (1 x 1) = 1
SUPA JET 2013
(i) Fafanua maana ya kishazi tegemezi. (al 1)
(ii) Huku ukitoa mifano, eleza sifa mbili za vishazi
tegemezi. (al 2)
(i) Ni sehemu ya sentensi kuu ambayo haitoi taarifa
iliyokamilika. Taarifa Fulani huhitajika ili pawepo na
maana kamili; hajitegemei. (al 1)
(ii) Sifa za vishazi tegemezi
a) Havitoi taarifa kamili mf. Malinda akija
b) Huwa na virejeshi kama O-rejeshi
c) Kishazi tegemezi huweza kuondolewa kwenye sentensi
bila ya kupoteza maana kuu.
d) Kishazi tegemezi kiondolewapo kwenye sentensi kuu,
hakiwezi kujisimamia.
(zozote 2 x 1)
SUPA JET 2013
Virai vilivyopigiwa mstari ni vya aina gani? (al 2)
(i) Shujaa Nelson Mandela ni mgonjwa.
(ii) Hivi karibuni shule iliyofungwa itafunguliwa.
(i) Kirai – tenzi (al 1)
(ii) Kirai – elezi (al 1)
SUPA JET 2013
Badilisha shamirisho kipozi katika sentensi ifuatayo iwe
shamirisho kitondo. (al 2)
Rispa alipigwa na mama.
Rispa alipigiwa na mama. (al 2)
SUPA JET 2013
Tunga sentensi moja yenye chagizo ya idadi. (al 1)
Kitoto huimba daima. (al 1)
LARI 2013
Onyesha kishazi huru na kishazi tegemezi katika sentensi
ifuatayo. (alama 2)
Pindi kipenga kilipopulizwa wanafunzi walipiga foleni.
Pindi kipenga kilipopulizwa – tegemezi. (1x2)
wanafunzi walipiga foleni – huru.
LARI 2013
Tambua aina za virai katika sentensi hizi. (alama 3)
i) Ilipandwa yote kando ya mto
ii) Kuimba huko kunaudhi
Ilipandwa yote– kirai kitenzi.
Kando ya—kirai kihusishi (1x3)
Kuimba huko kunaudhi – kirai nomino.
KIRINYAGA 2013
Tunga sentensi moja yenye kirai vumishi chenye muundo
wa V + E. (alama 2)
Kivumishi kifuatwe na kielezi,
Mfano, mtoto mzuri sana analia. 2 x 1 = 2
KIRINYAGA 2013
Bainisha kiima na kiarifa katika sentensi ifuatayo:
Mhadhiri huyo alifutwa jana jioni. (alama 2)
Mhadhiri huyu/alifutwa jana jioni
kiima kiarifa 2 x 1 = 2
KIRINYAGA 2013
Tambua kishazi na kipozi katika sentensi hii. (alama 3)
Ijapokuwa ameolewa tutamwandalia karamu leo.
Ijapokuwa ameolewa – Tegemezi
Tutamwandalia karamu leo – huru
Karamu – kipozi 3 x 1 = 3
SUBUKIA 2013
a) Eleza maana ya kishazi. (alama 1)
b) Onyesha vishazi huru na tegemezi katika sentensi hii.
(alama 1)
Mpira uliotoboka sana ulitengenezwa haraka
Kifungu cha maneno chenye muundo wa kiima kiarifa
- Kundi nomino + kundi tenzi
- Haswa kinapotokea katika sentensi al 1
- Tungo yenye kiima na kiarifa ambayo imo katika tungo
kuu
b) Mpira uliotoboka jana- kishazi tegemezi al ½
Ulitengenezwa haraka- kishazi huru al ½
SUBUKIA 2013
Onyesha shamirisho kipozi, kitondo na ala katika sentensi
ifuatayo. (alama 3)
Mwindaji haramu alilimulia mhindi ndovu kwa mkuki
Ndovu- kipozi- al 1
Muhindi- kitondo- al 1
Mkuki- ala- al 1
KASSU 2013
Onyesha chagizo katika tungo hili. (alama 1)
Mwalimu mnene zaidi anamiliki shamba lile kubwa.
chagizo – zaidi
KASSU 2013
Tambua aina ya virai katika sentensi zifuatazo: (alama
2)
(i) Uzembe ni adui wa maendeleo.
(ii) Paka alikuwa amejificha chini ya kitanda.
(i) Adui wa maendeleo – kirai nomino
(ii) Chini ya kitanda – Kirai elezi
(iii) Ni adui wa maendeleo – Kirai tenzi
TESO KUSINI 2012
Ainisha vishazi katika tungo hizi. (ala. 3)
a) Mwalimu anafunza vizuri . (ala 1)
b) Kiti kilichovunjika kilitengenezwa na seremala. (ala.
2)
a) Mwalimu anafunza vizuri .(kishazi Huru( 2
b) Kiti kilichovunjika (kishazi tegemezi) 1
c) Kiti kilitengenezwa na seremala ( Kishazi Huru) 1 (2 x2
= 4)
TESO KUSINI 2012
Onyesha aina za shamirisho katika ifuatayo . (ala. 3)
Mama alimakatia mgeni muwa kwa panga.
Mgeni : Shamirisho kitondo
Muwa :- Shamirisho kipozi
Panga : Shamirisho ala / kitumiza ( 3 x 1 = 3)
TESO KUSINI 2012
Pigia mstari kirai kihusishi katika sentensi ifuatayo.
(ala.1)
Bakari alikuwa miongoni mwa wanahewa.
Miongoni mwa wanahewa ( kirai kihusishi) (1 x 1 = 1)
ELDORET MAGHARIBI 2012
Bainisha vishazi katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
Farida anaaminiwa na watu wengi ijapokuwa ni mjanja.
Farida anaaminiwa na watu wengi kishazi huru. (1 x 2 =
2)
Ijapokuwa ni mjanja – kishazi tegemezi.
ELDORET MAGHARIBI 2012
Bainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
Nilimwandikia mwanangu barua kwa kalamu.
Kitondo - mwanangu
Kipozi - barua
Ala (kitumizi) - kalamu
ELDORET MASHARIKI 2012
Bainisha aina za shamirisho katika sentensi ifuatayo.
(alama 3)
Ali alimletea Yohana chai kwa chupa.
SH. Kipozi - chai
SH. Kitondo – Yohana
SH. Ala – chupa (3 x 1 = al. 3)
ELDORET MASHARIKI 2012
Bainisha vishazi katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
Kisima ambacho kimejaa maji kitajengwa.
Kisima kitajengwa – kishazi huru.
Kisima ambacho kimejaa maji – kishazi tegemezi. (ala. 2)
KWANZA 2012
Tambua shamirisho na chagizo katika sentensi hii. (Alama
2)
Alipiga teke mpira ukaruka juu juu zaidi.
Shamirisho-mpira
Chagizo-juu juu/zaidi 1x2=2
KWANZA 2012
Tambua aina za vishazi katika sentensi ifuatayo: (Alama
2)
Mtoto mwenye bidii hufanya vyema.
Aina za vishazi
Mtoto hufanya vyema-kishazi huru
Mwenye bidii-Kishazi tegemezi 1x2=2
OLOITOKITOK 2012
Tambua aina ya vishazi vilivyo katika sentensi ifuatayo.
(alama 2)
Mwanafunzi aliyesoma amefuzu mtihani.
Mwanafunzi aliyesoma (Kishazi tegemezi)
Amefuzu mtihani (Kishazi huru) 2X1
OLOITOKITOK 2012
Onyesha virai vilivyo katika sentensi hii. (alama 2)
Yule mwanabiashara amepata hasara kubwa.
Yule mwanabiashara (Kirai kiwakilishi)
Amepata hasara kubwa(Kirai kitenzi)
Hasara kubwa(kirai nomino) (2X1) = 2 (Zozote 2)
KIPKELION 2012
Tambua aina za sentensi zifuatazo (alama 2)
i) Kondoo aliyekata kamba ni wa mkulima yule.
ii) Alikuja jioni lakini hakunipata.
Aina za sentensi
i) Kondoo aliyekata kamba ni wa mkulima yule -
Changamano. (al. 1)
ii) Alikuja jioni lakini hakunipata – ambatano (al. 1)
KIPKELION 2012
Onyesha kirai katika sentensi ifuatayo na ueleze ni cha
aina gani. (alama 2)
Watoto wa kike hudunishwa katika jamii nyingi.
Kirai: Kuonyesha na kueleza.
- Watoto wa kike hudunishwa katika jamii nyingi.
- Watoto wa kike - KN (N+ V + N)
(1) (1)
KIPKELION 2012
Tambua yambwa katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
Wazazi wanawalipia karo watoto kwa hundi.
Yambwa
- Wazazi wanawalipia karo watoto kwa hundi.
- Kipozi → karo (al. 1)
- Kitondo / kitendewa → watoto (al. 1)
- ala – kwa hundi (al. 1)
KISUMU KASKAZINI 2012
Kwa kutoa mfano katika sentensi, onyesha angalau
miundo miwili ya sentensi sahihi.(alama 2)
- Sahili
- Changamano
- Ambatano (al. 2)
KEIYO 2012
Pigia mistari virai katika sentensi zifuatazo na utaje ni
vya aina gani? (alama 4)
i) Mboga zilipandwa kando ya mto.
ii) Wanafunzi wote wazembe wataadhibiwa.
Virai
i) Mboga zilipandwa kando ya mto
ii) Wanafunzi wote wazembe wataadhibiwa.
Mboga – kirai nomino
Kando ya mto – kirai kihusishi
Wote wazembe – kirai kivumishi
Wanafunzi – kirai nomino (al. 4)
Al. 2 kutaja, al. 2 kueleza
KEIYO 2012
Tabulisha aina za shamirisho katika sentensi ifuatayo.
(alama 2)
Kimtai alimsomea Kipruto barua.
Bana – shamirio kipozi (al. 1)
Kipruto – shamirisho kitondo (al. 1)
KISUMU MASHARIKI NA KASKAZINI 2012
Onyesha chagizo katika sentensi ifuatayo: (alama 1)
Watu wanne walipeperushwa juu kwa juu na upepo mkali.
Chagizo : juu kwa juu na upepo mkali (al.1)
KISUMU MASHARIKI NA KASKAZINI 2012
Tumia sentensi moja moja kubainisha tofauti kati ya
sentensi sahili na sentensi ambatano (alama 2)
Sahili : sentensi yoyote sahihi yenye kitenzi kikuu
kimoja/wazo moja kuu. (al.1)
Ambatano: sentensi sahili mbili zilizounganishwa (al.1)
KISUMU MASHARIKI NA KASKAZINI 2012
Taja aina ya yambwa iliyopigiwa mstari katika sentensi
uliyopewa: (alama 1)
mpishi amempikia mgeni wali vizuri.
Mgeni – yambwa tendewa (al.1)
KERICHO 2012
Onyesha kishazi huru na kishazi tegemezi katika sentensi
hii (al.2)
Mvua iliyonyesha jana ilisababisha madhara makubwa.
Iliyonyesha jana – kishazi tegemezi
Iliyosababisha madhara makubwa – kishazi huru. (2x1=2)
KERICHO 2012
Tambua yambwa tenda na yambwa tendewa katika
sentesi ifuatayo.
Maria alimnywesha mtoto maziwa jana asubuhi. (al.2)
Yamwa tenda – maziwa
Yambwa tendewa – mtoto ( ½ x4=2)
KISII KUSINI 2012
Onyesha virai katika sentensi ifuatayo na ueleze ni vya
aina gani? (ala 2)
Anapenda kusomka, gazeti lenye masuala ya kijamii.
Anapenda kusoma — Kirai tenzi. Gazeti lenye masuala ya
kijamii — Kirai nomino.
(Jibu)
KISII KUSINI 2012
Onyesha kishazi huru na kishazi tegemezi katika sentensi
ifuatayo (ala 2)
Mwanasiasa shupavu aliyewachochea wananchi
amekamatwa.
Mwanasiasa shupavu amekamatwa-kishazi huru.
Aliyechochea wananchi- kishazi tegemezi. (1×2)
KISII KUSINI 2012
Bainisha aina za shamirisho katika tungo hili. (ala 3)
Mgeni aliandaliwa chakula kitamu na mwenyeji wake kwa
sinia
Mgeni — shamirisho kitondo.
Chakula kitamu — kipozi
Kwa sinia - shamirisho ala 3×1= 4
BURETI 2012
Onyesha kishazi huru na tegemezi katika sentensi hii
Ijapokuwa kulikuwa na baridi kali niliondoka kwenda
sokoni. (ala.2)
Ijapokuwa kulikuwa na baridi kali- kishazi tegemezi.
Niliondoka kwenda sokoni - kishazi huru
KISUMU KASKAZINI 2012
Kwa kutolea mfano, onyesha miundo miwili tofauti ya
kirai nomino. (alama 2)
- Nomino na kivumishi - Mtoto mzuri anakula
- Kiwakilishi na kivumishi – Wewe pekee
- Kitenzi / jina na kivumishi – kusoma kwake
kunapendeza.
- Kivumishi na nomino – Yule mkulima ni hodari.
KISUMU KASKAZINI 2012
Onyesha shamirisho kipozi na kitondo katika sentensi
zifuatazo. (alama 2)
i) Shule nzuri imefunguliwa mayatima.
ii) Wanafunzi wamenunuliwa matunda na mwalimu wao.
(alama 2)
i) Shule nzuri imefunguliwa mayatima.
- Shule – Kipozi
- Mayatima - kitondo
ii) Wanafunzi wamenunuliwa matunda na mwalimu wao.
(alama 2)
- Wanafunzi – kitondo
- Matunda – kipozi
BORABU MASABA 2012
Mama alisema kuwa atamlimia afurahi ndipo amlipe
vizuri. (Tambua sentensi sahihi zilizoko
katika sentensi hii) (Alama 2)
i) Mama alisema.
ii) Mama atamlimia.
iii) Atafurahi(Yeye).
iv) Atamlipa vizuri.
4x ½ =Alama 2
BUTERE 2012
Tambua vishazi katika sentensi ifuatayo (alama 2)
Mwanafunzi aliyesoma kwa bidii alipita mtihani
Mwanafunzi aliyesoma kwa bidii –kishazi tegemezi
Alipita mtihani – kishazi huru
Kutambulisha ½ al
Kuainisha ½ al jumla alama 2
Ama
Mwanafunzi alipita mtihani
( Kishazi huru)
- aliyesoma kwa bidii
( kishazi tagesi)
BUTERE 2012
Tambua aina ya shamirisho katika sentensi ifuatayo
(alama 2)
Mama alimpikia chakula
yeye(m) kitondo (a 1)
Chakula kipozi (al 1)
BUTERE 2012
Tambua kirai kihusishi katika sentensi ifuatayo (alama 1)
Tulimkuta akiwa katika uchungu mwingi
Katika uchungu mwingi
BORABU MASABA 2012
Tunga sentensi yenye :
i) Chagizo ya mahali
ii) Kiunganishi wala (Alama 2)
i) Atumie vielezi/zaidi vinavyofuatana k.m Mjini
Mombasa,
ii) M.f Halii wala kucheka
KCSE 2012
Bainisha kiima na chagizo katika sentensi ifuatayo:
Watahiniwa hao walisoma maswali yote kwa makini
(alama 2)
Kiima-watahiniwa hao
Chagizo-kwa makini 2x1=2
KCSE 2012
Bainisha aina za virai vilivyopigiwa mstari :
Ubaguzi wa kijinsia umekashifiwa na viongoziwenye
misimamo thabiti mno. (alama 2)
-Wa kijinsia-kirai kihisishi
- uongozi wenye msimamo- kirai nomino
- thabiti mno- kirai kivumishi 3x1=3
KCSE 2012
Unda sentensi yenye muundo ufuato: KN(N)+KT(T+E)+U
+KN(N)+KT(T+E) (alama 2)
Baba anatembea haraka ilhali musa anatembea polepole.
Hemedi huandika vyema alkini zuhura huandika vibaya
4x1/2=2
KCSE 2012
Huku ukitoa mfano,eleza maana ya sentensi changamano
. (alama2)
Ni sentensi yenye kishazi huru na kingine tegemezi.
Iliyo na vishazi viwili tegemezi.
mf.angalisoma kwa bidii angalipita mtihani.
TRANS-NZOIA 2012
Bainisha yambwa tendwa na yambwa tendewa katika
sentensi hii.(Alama 2)
Mbunge wa Mtondo Kaskazini atawajengea wanakijiji
josho kisha aghurie mjini.
- Yambwa tendwa-josho
- Yambwa tendewa-wanakijiji 2x1=Alama 2
TRANS-NZOIA 2012
Bainisha kirai nomino na kirai kivumishi katika sentensi
hizi. (Alama 2)
i) Nguo aliyonunua mzazi ni mpya.
ii) Kondoo mwenye manyoya mengi hupendeza.
i) Kirai nomino
Nguo aliyonunua mzazi Alama1
ii) Kirai kivumishi
Mwenye manyoya mengi. Alama 1
BUSIA 2012
Ainisha shamirisho na chagizo katika sentensi (ala. 2)
Wachimba migodi wanafanya kazi haraka ipasavyo
kazi – shamirisho Haraka – chagizo (1x2=al.2)
NANDI KATI 2012
Onyesha sentensi zifuatazo ni za aina gani. (alama 2)
(i) Aliyetoroka in yule:
(iii) Sisi ndisi wezi ilhali wale ni watundu:
(i) Sentensi changamano
(ii) Sentensi ambatano (2 x 1 = alama 2)
NANDI KATI 2012
Onyesha aina ya kirai kilichopigwa mstari katika sentensi
ifuatayo. (alama 1)
Walimu wa kigeni watawasihi leo.
Walimu wa kigeni watawasili leo.
Kirai nomino (alama 1)
BUNGOMA 2012
Virai vilivyopigiwa mstari katika sentensi ni vya aina
gani. (alama2)
Mwanafunzi stadi ndiye akayetuzwa.
Mwanafunzi stadi – kirai nomino
Ndiye atakayetuzwa – kirai tenzi (AL 2)
NANDI KATI 2012
Bainisha aina za shamirisho katika sentensi ifuatayo:
(alama 3)
Baba alitumiwa pesa na kakangu kwa rununu.
Baba – kitondo
Pesa – kipozi
Rununu – ala / kitumizi (3 x 1 = alama 3)
NAKURU 2012
Bainisha vishazi katika sentensi ifuatayo. (alama 1)
Mkifanya kazi kwa bidii mtafaulu maishani.
Mkifanya kazi kwa bidii - kishazi tegemezi
Mtafaulu maishani – kishazi huru. (alama 1)
BUTULA 2012
Tunga sentensi ukitumia kirai kihusishi. (al.2)
Matumizi ya maneno kama,
- Kosa
- Na
- Katika
- Kwenye
- Maneno haya yafuatayo na nomino au kikundi nomino.
Mfano: Katika shule yao. 1 x 2 = Alama 2
BUTULA 2012
Bainsha matumizi ya yambwa na chagizo katika sentensi
(al.2)
Alimtupia kalamu jioni kwa mkono
- Kalamu
- Mkono Alama 2 x 1 = Alama 2
MERU KATI 2012
Bainisha vishazi. (Alama 2)
Mtoto akilishwa vizuri atakuwa na afya njema (alama 2)
Tegemezi – mtoto akilishwa vizuri
Huru – atakuwa na afya njema
MERU KATI 2012
Onyesha Yambwa. Yambiwa, kitumizi na chagizo katika
sentensi ifuatayo: (alama 4
Gathari amekatiwa kitamhaa kwa makasi makali sana.
Yambwa – Kitambaa
Yambiwa – Gacheri
Kitumizi –Makasi
Chagizo – sana (4x1=4)
MACHAKOS 2012
Bainisha sentensi sahili zilizo katika sentensi ifuatayo.
Meza yangu ilivunjika matendeguu yaliyoliwa na mchwa.
( alama 2 )
(i) Meza yangu ilivunjika matendeguu. (alama 1 )
(ii) Matendeguu yaliliwa na mchwa. (alama 1 )
YATTA 2012
Bainisha shamirisho tofauti katika sentensi ifuatayo:
(alama. 4)
Ali alimnunulia simu mpenzi wake.
SHAMIRISHO; Simu — kipozi
Mpenzi - kitondo (al.4)
YATTA 2012
Onyesha kishazi huru na tegemezi katika sentensi hii.
(alama. 2)
Ijapokuwa kulikuwa na baridi kali niliondoka kwenda
sokoni.
Ijapokuwa kulikuwa na baridi kali- kishazi tegemezi.
Niliondoka kwenda sokoni — kishazi huru
Kuria mashariki 2012
Tambua aina za sentensi zifuatazo kwa kuzingatia
muundo. (alama 2)
(i) Kitabu nilichomnunulia kitamsaidia kupita mtihani.
(ii) Somo la muhtasari na Isimu Jamii husisimua sana.
i) Changamano1
(ii) Sahihi1
KURIA MASHARIKI 2012
Huku ukitoa mifano, eleza miundo yoyote mitatu ya
kikundi Tenzi (KT).(alama 3)
(i) Kitenzi pekee – Amebadilika.
(ii) Kitenzi na nomino – Askofu atahudhuria mahafala.
(iii) Kitenzi na kitenzi – Wanapenda kucheza.
(iv) Kitenzi, nomino na kitenzi – Wazazi walipendekeza
shule ipanuliwe.
(v) Kitenzi na nomino mbili – Bunge limeirudishia tume
katiba.
(vi) Kitenzi na kivumishi – Amekuwa mrefu.
(vii) Kitenzi na kielezi – Mama alipika vizuri.
(viii) Kitenzi, kielezi na kitenzi – itakuwa vyema nje.
KURIA MASHARIKI 2012
Tambua na uainishe kirai katika sentensi hii. (alama 1)
Walimsaidia yatima kwa hali na mali.
Kwa hali na mali – kirai kielezi ( ½ x 2)
Kuria mashariki 2012
Bainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo.
Mwita alimtumia babake barua kwa posta. (alama 3)
Babake – Kitondo.
Barua – kipozi
Posta – ala / kifumizi (3 x 1 = 3)
(Akiandika kwa hundi – sufuri)
KITUI KATI 2012
Tambulisha shamirisho kipozi, kitondo na kitenzi katika
sentensi uliyopewa.(Alama 3)
Mzee Saidi alimwangushia mwanawe mti jana.
Kipozi – mti 1
Kitondo – mwanawe 1
Kitenzi – alimwangushia 1
KITUI KATI 2012
Tambua na ueleze aina za vishazi katika sentensi
uliyopewa. (Alama 2)
Ingawa ni mjanja hataki kutia bidii masomoni.
Ingawa ni mjanja½ – kishazi tegemezi ½
Hataki kutia bidii½ masomoni ½– kishazi huru ½
KILUNGU 2012
Tambua na ueleze aina ya virai: Mwanafunzi mzee
alikuwa akisoma. (alama2)
Mwanafunzi mzee – Kirai nomino (alama 2)
Alikuwa akisoma – Kirai kitenzi.
KILUNGU 2012
Onyesha shamirisho kipozi na kitondo katika sentensi
ifuatayo. (alama2)
Mwanafunzi aliwakariria wageni shairi kwa ustadi.
Shairi – Kipozi
Wageni – Kitondo (alama 2)
KILUNGU 2012
Bainisha kishazi huru na kishazi tegemezi katika
sentensi hii. (alama2)
Nitasafiri kesho jioni ingawa sina nauli.
Nitasafiri kesho njioni – Kishazi huru (alama 2)
Igawa sina nauli – Kishazi tegemezi.
KATHIANI 2012
Onyesha kishazi huru na tegemezi katika sentensi
ifuatayo. (alama 2)
Mateka wote waliokamatwa leo watafikishwa
mahakamani.
Mateka wote waliokamatwa – kishazi Tegemezi
Watafikishwa mahakamani – Kishazi Huru (alama 2)
KATHIANI 2012
Onyesha shamirisho kipozi na kitondo katika sentensi
ifuatayo (alama 2)
Mwalimu alimpa mwanafunzi kitabu.
Kitabu – kipozi
Mwanafunzi – kitondo (alama 2)
KASSU 2012
Onyesha virai nomino na virai elezi katika utungo
ufuatao. (al 2)
Mtoto mtukutu ameadhibiwa leo vikali sana.
Mtoto mtukutu – kirai nomino
Leo vikali sana – kirai kielezi (al 2)
KASSU 2012
Onyesha chagizo katika sentensi ifuatayo. (al 1)
Musyimi alishinda mara tatu leo asubuhi.
Mara tatu leo asubuhi
CH (al 1)
KASSU 2012
Tunga sentensi moja, kisha ubainishe kishazi huru na
kishazi tegemezi. (al 2)
Vitabu vilivyonunuliwa leo vimeibiwa.
Vitabu vimeibiwa al 1
Ulivyonunuliwa leo al 1 (al 2)
KASSU 2012
Onyesha yambwa kwa sentensi uliyopewa. (al 2)
Kasavuli alinadikiwa barua na Amina kwa kalamu.
Kasavuli – Yambwa tendewa (al 2)
Barua – Yambwa tendwa
KAKAMEGA KATI 2012
Tambua aina ya vishazi vilivyo katika sentensi ifuatayo.
(alama 2)
Mwanafunzi aliyesoma amefuzu mtihani.
Mwanafunzi aliyesoma (Kishazi tegemezi)
Amefuzu mtihani (Kishazi huru) 2X1
KAKAMEGA KATI 2012
Onyesha virai vilivyo katika sentensi hii. (alama 2)
Yule mwanabiashara amepata hasara kubwa.
Yule mwanabiashara (Kirai kiwakilishi)
Amepata hasara kubwa (Kirai kitenzi)
Hasara kubwa (kirai nomino)(2X1) = 2(Zozote 2)
EMBU 2012
Tunga sentensi changamano kutokana na sentensisahihi
zifuatazo.
Jumaamelala /Juma angekwenda shule jana / Juma
alisema
BARINGO 2012
Bainisha kiima na yambwa tendewa katika sentensi hii.
Zubeda alitungiwa wimbo mtamu na Hemedi. (alama 2)
Hemedi – Kiima
Zudeda – Yambwa tendewa/kitondo (2 X 1 = 2)
MSURURU WA UTABIRI 2012
Tambua kishazi tegemezi katika kirai nomino ulichopewa.
(alama 2)
Wanafunzi waliofanya mtihani wao mwaka jana walifika
shuleni leo.
Waliofanya mtihani wao mwaka jana 1 x 2 = 2
MSURURU WA UTABIRI 2012
Tenganisha kitenzi ulichopewa ili kuonyesha kirejeshi na
shamirisho yambwa.(alama 2)
Wanaokuletea
a) Wa – na – o – ku – let – e – a
O – Kirejeshi1
Ku – shamirisho yambwa1
Makosa
Ondoa H = 6 x ½ = 3
S = isizidi nusu ya tuzo kwa kila kitengo cha swali
Kwa mfano, swali la kwanza: (a) limetengewa alama 1,
kosa la sarufi (s) hadi nusu ya 1 = ½
BARINGO 2011
Fafanua tofauti kati ya kirai na kishazi. (alama 2)
Kirai hakina uhusiano wa kiima – kiarifu ilhali kishazi
kina uhusiano wa kiima kiarifu
(sharti kiwe na kiaritu/kitenzi). (Maelezo kamili – dama
2)
BUSIA 2011
Ainisha shamirisho na chagizo katika sentensi (ala. 2)
Wachimba migodi wanafanya kazi haraka ipasavyo
kazi – shamirisho
Haraka – chagizo (1x2=al.2)
KAKAMEGA MASHARIKI 2011
Tambua aina za sentensi zifuatazo. (al.2)
(i) Kondoo aliyekata kamba ni wa mkulima yule.
(ii) Alikuja jioni lakini hakunipata.
i) Kondoo aliyekata kamba ni wa mkukima yule –
Changamano. (alam 1)
ii) Alikuja jioni lakini hakunipata – ambatano (alama 1)
KAKAMEGA MASHARIKI 2011
Tambua yambwa katika sentensi ifuatayo: (al. 3)
Wazazi wanawalipia karo watoto kwa hundi.
Yambwa
Wazazi wanawalipia karo watoto kwa hundi.
- Kipozi karo (alama 1)
- Kitendo/Kitendea watoto (alama 1)
- ala – kwa hundi (alama 1)
KAKAMEGA MASHARIKI 2011
Onyesha kirai katika sentensi ifuatayo na ueleze ni cha
aina gani. (al.2)
Watoto wa kike hudunishwa katika jamii nyingi
Kirai: Kuonyesha na kucheza.
Watoto wa kike hudunishwa katika jamii nyingi.
Watoto wa kike – KN (N+ V + N)
(1) (1)
KAKAMEGA KATI 2011
Onyesha aina za shamirisho katika sentensi ifuatayo:
(ALAMA 2)
Seremala alimtengenezea baba kiti kizuri.
Baba – shamirisho kitondo
Kiti – shamirisho kipozi
KISUMU MAGHARIBI 2011
Onyesha aina mablimbali za shamirisho katika sentensi
hii. (ala. 3)
Mama aliwa fungulia wageni malngo kwa ufunguo.
(i) Wageni – kitondo
Mlango – kipozi
Kwa ufunguo – ala/kitumizi (al. 3)
KISUMU MAGHARIBI 2011
Bainisha aina ya vishazi katika sentensi ifuatayo. (ala.
2)
Tarakilishi hurahisihsa kazi tena hufanya kazi haraka.
Tarakilishi hurahisisha kazi – huru.
Hufanya kazi haraka – huru (al.2)
NDHIWA 2011
Bainisha aina za virai kwenye sentensi ifuatayo (Alama
1)
Leo asubuhi nilichelewa kuja kazini
Leo asubuhi – kirai kielezi Alama 1

kinyume

Posted by GEOFFREY - Jul 21, 2015


KINYUME
BUNYORE MARANDA 2013
Andika kinyume:
Adui yake anameza chakula kwa pupa.
Adui yake anathema chakula taratibu/halahala/asteaste/
polepole
Akibadili nomino atuzwe 0
MAKUENI 2013
Andika sentensi ifuatayo katika hali ya kinyume. (alama
2)
Wanafunzi waliombwa watawanye punje zote.
Waliombwa - walilazimishwa / walishurutishwa
Watawanye – wakusanye
RABAI 2013
Andika kinyume cha neno lililopigwa mstari.
Kamau amehama mjini. (alama 1)
Hamia Amelowea/ Ameselea 1x1 = alama 1
KIHARU 2013
Andika kinyume cha sentensi hii. (alama 1)
Babu alikashifiwa kwa vitendo vyake.
Babu alisifiwa kwa vitendo vyake. (1 x 1) = 1
NANDI ya KATI 2013
Andika kinyume cha sentensi ifuatayo. (alama 1)
Aliangika bendera baada ya kifo cha mfalme wao.
Aliangua bendera baada ya kifo cha mfalme wao. (alama
1)
SUBUKIA 2013
Andika kinyume. (alama 1)
Msichana huyu anapendeza kwa tabia yake nzuri
Msichana huyu hapendezi kwa tabia yake mbaya ½ x 2 =
1
NANDI KATI 2012
Andika kinyume cha sentensi hii. (alama 1)
Mvulana mmoja ameoa.
Mvulana mmoja ametalikiwa. (alama 1)
Iwapo ataandika msichana anyimwe ½ alama
MUUNGANO 2012
Andika kinyume cha sentensi ifuatayo. (alama 2)
Juma ameinjika chungu mekoni.
Ameepua/ Amedeua/Ametegua chungu mekoni
MBOONI MAGHARIBI 2012
Andika kinyume cha maneno yaliyopigiwa mstari (alama2)
Nyanya alikusanya kuni
(i) Nyanya
(ii) Tawanya Alama 2
KWANZA 2012
Andika kwa kinyume (Alama 1)
Kijakazi aliangika vyombo vya tajiri wake.
Kitwana aliangua vyombo vya tajiri wake 1x2=2
MBOONI MASHARIKI 2012
(a) Geuza sentensi zifuatazo ziwe katika hali ya kinyume
.
(i) Nyanya alisema baba alipoingia. (alama2)
(ii) Kitinda mimba ameaga dunia. (alama 2)
(i) Nyanya alinyamaza baba alipotoka.
(ii) Kitinda mimba amezaliwa. (2 x 2 = 4)
KIISUMU MASHARIKI NA KASKAZINI 2012
Andika sentensi ifuatayo ukitumia kinyume cha neno
lililoandikwa kwa herufi ya mlazo: (alama 1)
Binadamu hawezi kumuumba mwenzake.
Binadamu hawezi kumuumba mwenzake (alama 1)
(akipata kitahiniwa bila kutunga sentensi – al.½)
KIPKELION 2012
Andika kinyume cha kitenzi kilichopigiwa mstari. (alama
1)
Alikashifiwa kwa kazi aliyofanya.
- Alisifiwa kwa kazi aliyofanya. (1)
OLIOTOKITOK 2012
Andika kunyume cha: (alama 2)
Baba alimbariki mwanawe mtiifu.
Baba alimlaani mwanawe muasi
MBITA-SUBA 2012
Tumia vinyume vya maneno yaliyopigiwa mistari katika
sentensi ifuatayo. (alm2)
Fundi alishona surupwenye aliyouza sokoni.
Fundi alishonoa surupwenye aliyonunua sokoni.
KITUI KATI 2012
Andika kwa kinyume. (Alama 2)
Kulia huku kwa mtoto kunakasirisha sana.
Kucheka1 huku kwa mtoto kunafurahisha 1 sana
Kilungu 2012
Andika kinyume
Chakula hiki kitamu nitakimeza. (alama1)
Chakula hiki kichungu nitakitema. (alama 1)
Kathiani 2012
Andika kinyume cha sentensi (alama 2)
Walipakia vyombo jahazini walipolewa.
Walipakua vyombo jahazini walipolevuka. (alama 2)
Kakamega kati 2012
Andika kunyume cha: (alama 2)
Baba alimbariki mwanawe mtiifu.
Baba alimlaani mwanawe muasi
Baringo 2012
Andika kinyume cha sentensi hii.
Wavuvi walizama walipoenda kukusanya majani mabichi.
(alama 2)
Wavuvi walielea walipoenda kutawanya majani mabichi
(alama 2)
Kakamega Kati 2011
Tunga sentensi ukitumia kinyume cha kitenzi: ‘umba’ (al.
2)
Mungu ndiye aliye na uwezo wa kuumba na kuumbua
Kakamega Mashariki 2011
Andika kinyume cha kitenzi kilichopigiwa mstari. (al.1)
Alikashifiwa kwa kazi aliyofanya.
Kinyume
Alisifiwa kwa kazi aliyofanya. (1)
Machakos 2011
Kamilisha sentensi hii kwa neno lililo kinyume na
lililopigiwa mstari.
(i) Maji yameganda huwezi ( alama 1 )
Kuyayeyusha 1 x 1 = 1
Ndhiwa 2011
Andika kwa kinyume (Alama 1)
Hii ni njia nyembamba
Hii ni njia pana Alama 1
THIKA 2011
Andika upya sentensi ifuatayo ukitumia vinyume vya
maneno yaliyopigiwa mstari.(alama2)
Msichana aliyevaa nguo tawili, alitwezwa na wenzake.
Tawili - Fupi (alama2)
Tweza - Heshimu
MSURURU WA TOP STUDENT 2009
Andika kwa kinyume:
(i) Nje kulikuwa kweupe. (alama 1)
(ii) Mzizimo (alama 1)
i) Ndani kulikuwa kweusi. (alama 1)
(ii) Mzizimo - ari au fukuto. (alama 1)
KCSE 2006
Andika kinyume cha:
Mwise alikunja nguo alizokuwa ameanika (alama 2)
Mwise alikunjua nguo alizokuwa ameanua