Jukwaa La Kiswahili

Karibu kwenye jukwaa letu la Kiswahili

silabi

Posted by GEOFFREY - Jul 21, 2015


SHADDA/MKAZO, KIIMBO, VIPASHIO VYA LUGHA NA SILABI
ZA KISWAHILI
MARANDA- BUNYORE 2013
Ukitolea mfano,eleza maana ya silabi wazi.
-Silabi inayoisha kwa irabu/vokali mfano ka-ka
RABAI 2013
i)Taja vipashio vya lugha ya kiswahili. (alama 2)
ii) Toamifano miwili ya vipashio ulivyotoa hapo juu
i)Sauti ----------- silabi------------ neno--------
sentensi (alama 2)
/a/ - sauti
ta-ka-ta-ka – silabi
matoto anacheza mpira – sentensi
zozote mbili ( alama 2)
RABAI 2013
Tunga sentensi katika wingi ukitumia maneno yaliyo
katika mabano ili yalete dhana zifuatazo. (alama 2)
i) Amri (pa)
ii) Swali (ja)
Mpe mwenzako kitabu !Mpe!/Wale!
Mpeni mwalimu kitabu Mpeni!/wapeni!
Yoyote moja alama 1
ii) Je mtakuja?
Tena mwaja?
Mwaja?
Mtakuja?
Yeyote moja alama 1
LAIKIPIA 2013
Eleza maana ya kiimbo. (alama 1)
Onyesha kiimbo kiwezavyo kutokea katika neno hili.
(alama 1)
‘amekusamehe’
(i) Hali ya kushuka na kupanda kwa sauti
unapozungumza. (1 x 1 = 1)
(ii) amekusamehe! au amekusamehe? au amekusamehe.
(lolote 1 x 1 = 1)
NYAMIRA 2013
Andika sentensi moja ya Kiswahili itakayoonyesha hali
hizi: (alama 2)
(i) Swali
(ii) Taarifa
(i) Kamau ameenda sokoni?
(ii) Kamau ameenda sokoni
- hakiki kazi ya mwanafunzi 2x1=2.
MAKUENI 2013
Tumia shadda panapofaa na ueleze maana mbili tofauti
za neno walakini. (alama 2)
Wa’lakini – hata hivyo
Wal’akini – kasoro / doa / dosari ( alama 2 )
MATUNGULU 2013
Eleza tofauti kati ya sauti: (alama 2 )
(i) /d /
(ii) /t/
d – kipasuo ghuna (GH)
t – kipasuo sighuna (H) 2 x 1 = 2
RABAI 2013’
Huku ukitoa mifano eleza maana ya kiimbo. (alama 2)
Kupanda na kushuka kwa sauti katika uzungumzaji.
Mfano : Watoto wamelala. (maelezo)
Watoto wamelala? (swali)
Maelezo sahihi alama 1
Mfano sahihi alama 1.2 kwa kila mfano
SUBUKIA 2013
Kwa kutoa mfano onyesha miundo miwili ya silabi za
kiswahili. (alama 2)
i) Silabi za irabu moja- oa, au, ua
ii) Konsonanti za irabu- ki, ka, - ku – ta
iii) Konsonanti moja- M+tu, n+chi
iv) Konsonanti mbili na irabu- ndi+mu
v)Konsonanti tatu na irabu- Le+ngwa
[(muundo ½ mfano ½ ) x2]=2
NDHIWA 2013
Toa mfano wa neno lenye muundo wa silabi ya konsonanti
tatu mwambatano (al. 1)
mf. Mbeha / nywele /kunywa n.k. (a1ama 1)
NDHIWA 2013
Onyesha utakapoweka shadda katika maneno haya ili
kutoa maana katika mabano.
(al. 2)
Barabara (sawasawa) …
Niletee (Rai)
(i) ba’rabara (alama 1)
(ii) Nilet‘ee (alama 1)
NYANDO 2013
Toa mfano wa neno lenye muundo wa silabi ya konsonanti
tatu mwambatano pamoja na irabu (Alama1)
kkkI
mbwa/mbweha/(1x1=alama 1)
KIHARU 2013
Onyesha mahali panapowekwa Shadda kwenye kitenzi
katika sentensi ifuatayo:(alama 1)
Kiberiti ki juu ya meza.
Shadda – ‘Ki’ (1 x 1) = 1
NANDI YA KATI 2013
(i) Kiimbo ni nini? (alama 1)
(ii) Eleza matumizi ya kiimbo. (alama 2)
(i) Kiimbo ni hali ya kupanda na kushuka kwa sauti
wakati mtu anapozungumza.
(ii) Kiimbo hutekeleza majukumu yafuatayo: kuonyesha
kuwa sentensi ni swali.
Mama anakuja?
Kuonyesha kuwa sentensi ni kauli.
Mama amekuja.
Kuonyesha kuwa sentensi ina ujumbe unaoshangaza.
Mama amekuja. (yoyote 2x1 = alama 2)
NANDI KASKAZINI 2013
Badilisha sentensi ifuatayo iwe katika hali ya kuamuru
katika wingi. (alama 2)
Njoo hapa.
Njooni√ hapa! √ (1 x 2 = alama 2)
NANDI KUSINI- TINDIRET 2013
Andika neno lenye muundo ufuatao wa silabi. (alama 1)
KKKI
KKKI – mchwa,mbwa, n.k
KIRINYAGA 2013
Andika maneno matatu yenye miundo tofauti ya silabi.
(alama 3)
(i) Irabu pekee – au, ua
(ii) KIKI – baba
(iii) KKI - ndoa, kwao
(iv) KKKI - mbwa, nywea 3 x 1 = 3
KIRINYAGA 2013
Amrisha vitenzi vifuatavyo katika umoja na wingi.
(alama 2)
(i) fa
iii) Imba
Fa – Kufa!
- Kufeni! Feni!
Imba - Imba!
- Imbeni! 4 x ½ = 2
KASSU 2013
Pigia mstari silabi inayowekwa shadda katika tungo
lifuatalo. (alama 1)
Alituchochea
Alituchochea alama 1
KASSU 2013
Eleza matumizi ya kiimbo. (alama 2)
Kuonyesha swali kuonyesha ombi
Kuonyesha amri
Kuonyesha taarifa
Kuonyesha mshangao, hasira n.k. zozote 2 alama 2
KASSU 2013
Tunga sentensi yenye silabi mwambatano. (alama 1)
Konsonanti mbili au tatu zifuatane k.m njoo, mbweha
n.k
SUPAJET
Eleza miundo ya silabi za neno lifuatalo. (al 3)
Dhaifu
Dhaifu
Dha – i – fu
Dh/a – Konsonanti + Irabu
i – Irabu
f/u – Konsonanti + Irabu (al 3)
SUPAJET 2013
Huku ukidhihirisha maana mbili tofauti, tia shadda katika
neno lifuatalo. (al 2)
Walakini
Wal’akini – dosari / ila (al 1)
Wala’kini – lakini (al 1)
KCSE 2012
i) Eleza maana ya shadda. (alama1)
Mkazo unaotiwa katika ‘neno’ au ‘silabi’ wakati wa
kutamka ili kubaini maana
ii) Onyesha panapotokea shadda katika neno:
‘mteremko’ (alama 1)
Mtere’mko mteremko mterem’ko
ELDORET MAGHARIBI 2012
Taja vipashio vikuu vya lugha. (alama 2)
Sauti
Silabi
Neno
Sentensi (4 x ½ = 2)

Sauti

Posted by GEOFFREY - Jul 21, 2015


MATAMSHI BORA
BOMET 2013
Ainisha sauti zifuatazo (al.3)
(i) /r/
(ii) /P/
(iii) /m/
(iv) /w/
(i) ‘r’ – kimadende
(ii) ‘p’ – kipasuo halifu cha midomo
(iii) ‘m’ – nazali ya midomo (1 x 3)
Iiv) w - kiyeyusho/nusu irabi
MATUNGULU 2013
Eleza vigezo vichunguzwapo kutamka konsonanti. (alama
3 )
(i) Mahali hewa inavyozuiliwa.
(ii) Jinsi hewa inavyozuiliwa.
(iii) Hali ya mtetemeko katika nyuzi za sauti. 3 x 1 = 3
MARANDA –BUNYORE 2013
Eleza sifa mbiLi bainifu za konsonanti /h/ (alama 2)
-Ni sighuna/hafifu..Ni konsonanti ya glota/koo/
koromeo.
Ni kikwamizo
KIBWEZI 2013
Eleza tofauti baina ya irabu na konsonati. ( alama 2
Irabu hutamkwa kwa ulaini / hewa haizuiliwi / mdomo
huviringwa au hutandazwa.
Konsonati hutamkwa kwa kubana hewa kisha kuachilia
taratibu. Sehemu mbili za kutamkia
husongeleana au kugusana.
RABAI 2013
Eleza tofauti na mfanano uliopo baina ya sauti /f/ na /
v/ (alama 2)
i) Tofauti:
/f/ si ghuna alama ½
/v/ sauti ghuna alama ½ alama 1
ii) mfanano
Vikwamizo alama 1
HOMABAY 2013
(i) Taja sauti moja ya kaakaa laini. (alama 1)
(ii) Taja sauti moja ya ufizi (alama 1)
(i) g,k,gh,ng’,y (zozote 1x1=1)
(ii) t, d,s,z,n,l,r (zozote 1x1=1)
MAKUENI 2013
(a) Taja sauti mbili ambazo ni za (alama 2)
(a) Kikwamizo ghuna
(b) King’ong’o cha kaa kaa ngumu
(i) / v/ /dh/ /z/
(ii) /ny/ ( alama 2 )
KIKUYU 2013
Ni ala zipi za sauti zinazotumika kutamkia sauti
zifuatazo? (alama 3)
/I/
/ng’/
/ny/
/I/ - Ulimi ni ufizi
/ng/ - Ulimi / kaa kaa laini
/ny/ - Ulimi / kaakaa gumu (alama 3)
LAIKIPIA-LENOCET 2013
Andika vitamkwa vyenye sifa zifuatazo vinapotamkwa.
(alama 2)
(i) Midomo wazi
(ii) Midomo kuviringwa
(i) |e| |i| (1 x 1 = 1)
(ii) |a| |o| |u| (1 x 1 = 1)
KISUMU MAGHARIBI 2013
Eleza tofauti kati ya sauti za vipasuo na vikwamizo (al
2)
–Hewa huzuiwa kabisa na kuachiliwa kw ghafla kwa
mpasho k.m p& b
-Vikwamizo – Ala za kutamkia hukaribiana na kutoa
sauti ya mkwaruzo wa hewa au msuguano k.m.(f/v/lt
gh)
NDIWA 2013
Taja sauti ambazo ni konsonanti na wakati uo huo ni
irabu.
(al. 2)
(i) /y/
(ii) / w / (alama 2)
NYANDO 2013
(i) Toa mfano wa sauti nazali (alama 1)
(ii) Taja sauti mbili ambazo ni vikwamizo na hutamkiwa
kwenye ufizi (Alama 1)
i)/m/,/n/ /ny/ /ng‘/(1x1=alama 1)
(ii) /s/, /z/ (2x1/2= alama 1)
SUBUKIA 2013
Toa mfano wa sauti ambayo ni ; (al ama 2)
Kikwamizo ambacho ni ghuna
Kikwamizo ambacho si ghuna
a) v, dh z, gh, h, 1x1= al 1
b) f th s sh 1x1=al 1
KASSU 2013
Bainisha sifa zinazotofautisha sauti zifuatazo. (alama
2)
/e/ na /u/
/ e / - irabu ya mbele
- Midomo hutandazwa
- Irabu ya kati
/ u / - Irabu ya nyuma
- Irabu ya juu
- Midomo huviringwa (Tofauti zozote mbili = alama 2)
SUPA JET 2013
Eleza njia mbili za kuainisha konsonanti.
NJia za kuanisha konsonanti:-
(i) Mahali pa kutamkia (mf. Ufuzi, menu)
(ii) Utikisaji wa nyuzi za glota (ghuna na sighuna)
(iii) Ubanaji wa hewa
(zozote 2 x 1)
KIHARU 2013
Taja ala za kutamkia zinazotumiwa kuelezea sifa za
vokali yoyote ile. (alama 2)
(i) Midomo
(ii) Ulimi (2 x 1) = 2
KIRINYAGA 2013
Taja sifa mbili bainifu za konsonanti /ny/. (alama 1)
Ni sauti nazali.
Taja sauti mbili ambazo ni vikwamizo vya meno. (alama 1)
- th, dh
LARI 2013
Tofautisha sauti zifuatazo; (alama 2)
i) /g/
ii) /gh/
i) /g/ - kipasuo (1x2)
ii) /gh/- kikwamizo
NANDI YA KATI 2013
Toa mifano miwili miwili ya sauti zifuatazo. (alama 2)
(i) Sauti ghuna ambazo ni vipasuo.
(ii) Sauti sighuna ambazo ni vikwamizo
(i) /b/ /d/ /g/
(ii) /t/ /th/ /sh/ /h/
Kila moja nusu alama. Lazima atungie na fonimu
ziandikwe kwa herufi ndogo
NANDI KASKAZINI 2013
Taja sauti mbili za nazali. (alama 2)
/m/, /n/, /ny/, /ng/ - zozote mbili (1 x 2 = alama 2)
Atumie herufi ndogo. Akitumia herufi kubwa anapata
sufuri.
NANDI KUSINI- TINDERET 2013
Taja sauti yenye sifa zifuatazo: (alama 2)
(i) Mbele, juu, tandazwa:
(ii) Kikwamizo, sighuna cha ufizi:
(i) /i/
(ii) /s/
KIKUYU 2013
Ni ala zipi za sauti zinazotumika kutamkia sauti
zifuatazo? (alama 3)
/I/
/ng’/
/ny/
/I/ - Ulimi ni ufizi
/ng/ - Ulimi / kaa kaa laini
/ny/ - Ulimi / kaakaa gumu (alama 3)

Damu Nyeusi

Posted by Patrick Kimathi - Jul 14, 2015


Habari wanalugha,?Naomba mnisaidie na maudhui katika Hadithi ya Mizizi na Matawi.

Ombi Kushiriki

Posted by Okelo w'Esonga - Jul 12, 2015


Hamjambo wanalugha wenza. Naomba mnifafanulie madhumni hasa yatovuti hii kisha naomba mniambia iwapo naruhusiwa kushiriki utunzi wangu waq mashairi na wenzangu katika tovuti hii.

Maswali

Posted by Haggai Millo - Jul 07, 2015


Hamjambo wapenzi wa lugha teule ya Kiswahili? Naomba mnifafanulie kwa kina kuhusu nomino changamano na nomino huru. Aidha naomba kufahamu zaidi kuhusu a-unganifu yangu na wangu kwa kurejelea majina ya ukoo. Ahsanteni kwa kazi nzuri mnayofanya. Mungu awape nguvu na hekima zaidi katika nyanja hii.