Mifano ya Methali

Ifuatayo ni mifano ya Methali, kipera cha tungo fupi katika Fasihi Simulizi.
1. Achekaye kovu hajaona jeraha.

2. Adhabu ya kaburi aijua maiti.

3. Adui aangukapo muinue.

4. Adui mpende

5. Adui ya mtu ni mtu.

6. Afadhali dooteni kama ambari kutanda

7. Afadhali mchawi kuliko mfitini.

8. Afya ni bora kuliko mali.

9. Aingiaye kichakani hurejea na kuni

10. Aisifuye mvua imemnyea

11. Ajabu ya shingo kukataa kulala kitandani.

12. Akiba haiozi

13. Akili ni mali

14. Akili ni nywele, kila mtu ana zake.

15. Akili nyingi huondoa maarifa.

16. Akufukuzaye hakwambii toka

17. Akumegeaye tonge humpiga mamako ukitazama

18. Akunyimaye mbazi kakupunguzia mashuzi.

19. Aliyekutweka ndiye atakayekutua.

20. Aliyeumwa na nyoka akiona jani hushtuka.

21. Anayekueleza ya wengine atawaeleza mengine ya kwako.

22. Asante ya punda ni mateke

23. Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu.

24. Asiyejua kufa na atazame kaburi.

25. Asiyejua maana haambiwi maana.

26. Asiyekubali kushindwa si mshindani

27. Asiyekunywa kwenye chemchemi hunywa kwenye mto.

28. Asiyekuwapo na lake halipo

29. Asiyekuwepo machoni na moyoni hayupo.

30. Asiyeogopa ng’ombe ni ng’ombe

31. Asiyeona aibu zake asione za mwenziwe.

32. Atangaye na jua hujuwa

33. Atekaye maji mtoni asitukane mamba.

34. Avumaye baharini papa kumbe wengine wapo.

35. Baada ya dhiki faraja

36. Badiliko kwa mjukuu uanze na babu.

37. Bahari haivukwi kwa kuogolea.

38. Bahari iliko ndiko mito iendako.

39. Bahati ikipiga hodi ni lazima ufungue mlango mwenyewe.

40. Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi

41. Banda likikushinda jenga kibanda.

42. Baniani mbaya kiatu chake dawa

43. Bata mtaga mayai usimchinje kwa tamaa ya wengi.

44. Bendera hufuata upepo

45. Bila silaha usiingie vitani.

46. Bilisi wa mtu ni mtu

47. Cha mkufuu mwanafuu ha, na akila hu; cha mwanafuu mkufuu hu na akila ha

48. Cha mlevi huliwa na mgema.

49. Chaka la simba halilali nguruwe.

50. Chanda chema huvikwa pete

51. Chema chajiuza kibaya chajitembeza

52. Chombo cha kuzama hakina usukani

53. Chombo hakiendi ikiwa kila mtu anapiga makasia yake.

54. Chovya chovya humaliza buyu ya asali.

55. Chui hakumbatiwi.

56. Chui naye ana mke.

57. Chura huweza kumwua tembo.

58. Dalili ya mvua ni mawingu.

59. Damu ni nzito kuliko maji

60. Daraja livuke ulifikiapo.

61. Daraja ukilibomoa ujue kuogolea.

62. Dau la mnyonge haliendi joshi

63. Dawa kubwa ya hasira ni kuchelea.

64. Dawa ya moto ni moto

65. Debe tupu haliachi kutika

66. Dua la kuku halimpati mwewe

67. Dudu liumalo usilipe kidole

68. Elimu maisha si vitabu.

69. Elimu ni mwangaza gizani hung’aa

70. Epuka wakusifuo siku zote.

71. Fadhila ya punda ni mashuzi

72. Farasi hamuwawezi, tembo mtawalishani?

73. Fimbo ya mbali haiuwi nyoka.

74. Fuata nyuki ufe mzingani

75. Fuata nyuki ule asali

76. Fumbo mfumbie mjinga, mwerevu huligangua

77. Ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno.

78. Gome la udi si la mnuka uvundo.

79. Haba na haba hujaza kibaba.

80. Hafriti hafichiki

81. hakuna marefu yasiyo na mwisho

82. Hakuna masika yasiyokuwa na mbu.

83. Hakuna siri ya watu wawili

84. Haraka haraka haina baraka.

85. Hasira hasara

86. Hatua ndefu hufupisha mwendo.

87. Heri kenda shika kuliko kumi nenda rudi

88. Heri kufa macho kuliko kufa moyo.

89. Heri kujikwaa kidole kuliko kujikwaa ulimi.

90. Heri nitakula na nini kuliko nitakula nini.

91. Heri ya mrama kuliko kuzama.

92. Hisani haiozi

93. Ila ya kikwapa kunuka pasipo kidonda.

94. Iliyopita si ndwele, ganga ijayo.

95. Imara ya jembe kaingoje shamba.

96. Ipunguzwayo ni iliyojaa.

97. Isipokuwasha hujairamba.

98. Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza.

99. Jicho halina pazia.

100. Jino la pembe si dawa ya pengo

101. Jitihada haiondoi kudura

102. Jogoo hulia "uta wangu u kule".

103. Jogoo la shamba haliwiki mjini.

104. Kafiri akupaye si Islamu asiyekupa

105. Kamba hukatika pabovu

106. Kanga hazai ugenini

107. Kawaida ni kama sheria

108. Kawia ufike

109. Kazi mbaya siyo mchezo mzuri.

110. Kazi mbi si mchezo mwema

111. Kelele za chura hazimkatazi ng'ombe kunywa maji.

112. Kelele za mlango haziniwasi usingizi

113. Kelele za mwenye nyumba hazimkatazi mgeni kulala.

114. Kenda karibu na kumi

115. Kibaya chako si kizuri cha mwenzio

116. Kiburi si maungwana

117. Kibuzi na kibuzi hununua jahazi.

118. Kichango kuchangizana

119. Kichwa cha kuku hakistahili kilemba

120. Kidole kimoja hakivunji chawa

121. Kiingiacho mjini si haramu

122. Kikulacho ki nguoni mwako

123. Kila chombo kwa wimbile

124. Kila lenye mwanzo lina mwisho

125. Kila mlango na ufunguo wake

126. Kila msiba una mwenzake

127. Kila mtoto na koja lake

128. Kila mwamba ngoma ngozi huivuta kwake

129. Kila ndege huruka na mbawa zake

130. Kilio huanza mfiwa ndipo wa mbali wakaingia.

131. Kimya kingi kina mshindo

132. Kinga kwa kinga ndipo moto uwakapo

133. Kinyozi hajinyoi na akijinyoa hujikata.

134. Kinywa ni jumba la maneno

135. Kipendacho moyo ni dawa

136. Kipya kinyemi ingawa kidonda

137. Kisebusebu na roho kipapo

138. Kisicholiwa na mlimwengu, sera nale

139. Kitanda usichokilalia hujui kunguni wake

140. Kivuli cha fimbo hakimfichi mtu jua.

141. Kiwi cha Yule ni chema chake hata ulimwengu umwishe

142. Konzo ya maji haifumbatiki.

143. Kosa moja haliachi mke.

144. Kozi mwandada, kulala na njaa kupenda

145. Kuagiza kufyekeza

146. Kuambizana kuko kusikilizana hapana

147. Kucha Mungu si kilemba cheupe.

148. Kuchamba kwingi kuondoka na mavi

149. Kufa kikondoo ndiko kufa kiungwana.

150. Kufa kufaana

151. Kufa kwa jamaa harusi

152. Kufa kwa mdomo mate hutawanyika.

153. Kuishi kwingi ni kuona mengi

154. Kukopa harusi kulipa matanga

155. Kuku havunji yai lake

156. Kuku hawekwi shahidi wala hajui sheria.

157. Kuku mgeni hakosi kamba mguuni

158. Kula ku tamu kulima mavune

159. Kulea mimba si kazi, kazi kulea mwana

160. Kumwashia taa kipofu ni kuharibu mafuta.

161. Kunako matanga kumekufa mtu

162. Kunguru mwoga hukimbiza mbawa zake

163. Kuni ya juu uchaga hucheka iliyo motoni.

164. Kupanda mchongoma, kushuka ngoma

165. Kupata si kwa werevu na kukosa si ujinga.

166. Kupotea njia ndiko kujua njia

167. Kusikia si kuona.

168. Kutaataa siyo dawa ya kufa.

169. Kutangulia si kufika

170. Kuteleza si kuanguka

171. Kutoa ni moyo usambe ni utajiri

172. Kutu kuu ni la mgeni

173. Kuuliza si ujinga

174. Kuvunjika kwa mwiko si mwisho wa kupika ugali

175. Kuzima koleo sio mwisho wa uhunzi

176. Kwa mwoga huenda kicheko na kwa shujaa huenda kilio

177. Kwenda mbio si kufika

178. La kuvunda halina ubani.

179. La kuvunja halina rubani

180. Lake mtu halimtapishi bali humchefusha.

181. Leo kwako, kesho kwa mwenzio.

182. Leo ni leo asemayo kesho ni mwongo.

183. Liandikwalo ndilo liwalo.

184. Lila na fila hazitangamani.

185. Lililo moyoni ulimi huiba.

186. Lipitalo hupishwa .

187. Lisemwalo lipo, ikiwa halipo laja.

188. Lisilokuwapo moyoni, halipo machoni.

189. Maafuu hapatilizwi.

190. Macho hayana pazia.

191. Mafahali wawili hawakai zizi moja

192. Maiti haulizwi sanda.

193. Maji hufuata mkondo.

194. Maji huteremka bondeni, hayapandi mlima.

195. Maji ukiyavulia nguo huna budi kuyaoga.

196. Maji usiyoyafika hujui wingi wake.

197. Maji ya kifuu bahari ya chungu.

198. Maji yakija hupwa.

199. Maji yakimwagika hayazoleki.

200. Majumba makubwa husitiri mambo.

201. Majuto ni mjukuu.

202. Manahodha wengi chombo huenda mrama

203. Maneno makali hayavunji mfupa

204. Maneno mema hutoa nyoka pangoni.

205. Mapenzi ni kikohozi, hayawezi kufichika.

206. Masikini akipata matako hulia mbwata

207. Masikini haokoti, akiokota huambiwa kaiba.

208. Masikini na mwanawe tajiri na mali yake.

209. Mavi usioyala,wayawingiani kuku?

210. Mavi ya kale hayaachi kunuka

211. Mavi ya kale hayanuki

212. Mbinu hufuata mwendo.

213. Mbio za sakafuni huishia ukingoni.

214. Mbiu za mgambo ikilia kuna jambo.

215. Mchagua jembe si mkulima

216. Mchagua nazi hupata koroma.

217. Mchakacho ujao,halulengwi na jiwe.

218. Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo.

219. Mcheka kilema hafi bila kumpata.

220. Mchele moja mapishi mengi

221. Mchelea mwana kulia hulia yeye..

222. Mcheza hawi kiwete, ngoma yataka matao

223. Mcheza kwao hutuzwa.

224. Mchezea matope humruka

225. Mchezea mavi hayaachi kumnuka.

226. Mchezea zuri baya humfika.

227. Mchimba kisima hungia mwenyewe.

228. Mchonga mwiko hukimbiza mkono wake.

229. Mchovya asali hachovi mara moja.

230. Mchuma janga hula na wakwao.

231. Mchuma juani hula kivulini.

232. Mdharau biu,hubiuka yeye..

233. Meno ya mbwa hayaumani.

234. Mfa maji haishi kutapatapa.

235. Mfa maji hukamata maji.

236. Mficha uchi hazai.

237. Mfinyazi hulia gaeni.

238. Mfukuzwa kwao hana pa kwenda.

239. Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.

240. Mganga hajigangui.

241. Mgema akisifiwa tembo hulitia maji.

242. Mgeni ni kuku mweupe.

243. Mgeni njoo mwenyeji apone.

244. Mgomba haushindwi na mkunguwe.

245. Mgonjwa haulizwi uji.

246. Miye nyumba ya udongo ,sihimili vishindo

247. Mjinga akierevuka mwerevu yupo mashakani.

248. Mjinga mpe kilemba utamwona mwendowe.

249. Mjumbe hauawi.

250. Mkamatwa na ngozi ndiye mwizi.

251. Mkamia maji hayanywi.

252. Mkata (masikini) hana kinyongo.

253. Mke ni nguo mgomba kupalilia.

254. Mkono mmoja hauchinji ngombe.

255. Mkono mmoja haulei mwana.

256. Mkono mtupu haulambwi.

257. Mkono usioweza kuukata, ubusu.

258. Mkosa kitoweo humangiria.

259. Mkuki kwa nguruwe mtamu, kwa mwanadamu uchungu.

260. Mkulima ni mmoja walaji ni wengi.

261. Mla cha mwenziwe na chake huliwa.

262. Mla cha uchungu na tamu hakosi..

263. Mla kuku wa mwenziwe miguu humwelekeya.

264. Mla mbuzi hulipa ng'ombe.

265. Mla mla leo mla jana kala nini?

266. Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.

267. Mlenga jiwe kundini hajui limpataye.

268. Mlimbua nchi ni mwananchi.

269. Mlinzi hulinda ndege, mke mzuri halindwi.

270. Mnyamaa kadumbu.

271. Mnywa maji kwa mkono mmoja, kiu yake i pale pale.

272. Moja shika, si kumi nenda urudi.

273. Moto hauzai moto, huzaa jivu.

274. Moto hauzai moto.

275. Mpanda farasi wawili hupasuka msamba.

276. Mpanda ngazi hushuka.

277. Mpanda ovyo hula ovyo.

278. Mpemba akipata gogo hanyii chini.

279. Mpemba hakimbii mvua ndogo.

280. Mpiga ngumi ukuta huumiza mkonowe.

281. Mpofu hasahau mkongojo wake.

282. Mpofuka ukongweni,hapotewi na njia.

283. Msafiri kafiri

284. Msafiri masikini ajapokuwa sultani.

285. Msasi haogopi mwiba.

286. Msema kweli hukimbiwa na rafiki zake.

287. Msema pweke hakosi.

288. Mshale kwenda msituni haukupotea.

289. Mshika mawili moja humponyoka

290. Mshoni hachagui nguo.

291. Msitukane wagema na ulevi ungalipo.

292. Msitukane wakunga na uzazi ungalipo.

293. Mstahimilivu hula mbivu.

294. Mtafunwa na nyoka akiona unyasi hushtuka.

295. Mtaka cha mvunguni sharti ainame.

296. Mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba.

297. Mtaka unda haneni.

298. Mtaka yote hukosa yote

299. Mtegemea nundu haachi kunona.

300. Mtego bila chambo hanasi.

301. Mtembezi hula miguu yake.

302. Mteuzi hashi tamaa.

303. Mti hauwendi ila kwa nyenzo.

304. Mti mkuu ukigwa wana wa nyuni huyumba

305. Mtondoo haufi maji.

306. Mtoto akililia wembe, mpe.

307. Mtoto umleyavyo ndivyo akuavyo.

308. Mtoto wa nyoka ni nyoka.

309. Mtu hakatai mwito, hukata aitwalo.

310. Mtu hujikuna ajipatiapo.

311. Mtu huulizwa amevaani , haulizwi amekulani.

312. Mtumai cha ndugu hufa masikini.

313. Mtumi wa kunga haambiwi maana.

314. Mtumikie kafiri upate mradi wako.

315. Mtupa jongoo hutupa na mti wake.

316. Mume wa mama ni baba.

317. Mungu hamfichi mnafiki.

318. Muungwana ni kitendo

319. Mvumbika changa hula mbovu.

320. Mvumilivu hula mbivu.

321. Mvungu mkeka.

322. Mvunja nchi ni mwananchi.

323. Mvuvi ndiye ajuaye pweza alipo.

324. Mwacha mila ni mtumwa.

325. Mwamba na wako hukutuma umwambiye.

326. Mwamini Mungu si mtovu.

327. Mwana maji wa kwale kufa maji mazowea.

328. Mwana mkaidi hafaidi mpaka siku ya idi.

329. Mwana mkuwa nawe ni mwenzio kama wewe.

330. Mwana simba ni simba.

331. Mwana wa kuku hafunzwi kuchakura.

332. Mwana wa nyoka ni nyoka

333. Mwanga mpe mtoto kulea.

334. Mwangaza mbili moja humponyoka.

335. Mwanzo kokochi mwisho nazi.

336. Mwanzo wa chanzo ni chane mbili.

337. Mwanzo wa ngoma ni lele.

338. Mwapiza la nje hupata la ndani.

339. Mwekaji kisasi haambiwi mwerevu.

340. Mwenda bure si mkaa bure,huenda akaokota..

341. Mwenda mbio hujikwaa kidole..

342. Mwenda pole hajikwai.

343. Mwenda tezi na omo marejeo ngamani..

344. Mwenye haja ndiye aendaye chooni.

345. Mwenye kelele hana neno.

346. Mwenye kovu usidhani kapowa..

347. Mwenye kubebwa hujikaza.

348. Mwenye kuchinja hachelei kuchuna

349. Mwenye macho haambiwi tazama.

350. Mwenye nguvu mpishe

351. Mwenye njaa hana miiko.

352. Mwenye pupa hadiriki kula tamu.

353. Mwenye shibe hamjui mwenye njaa

354. Mwenye shoka hakosi kuni.

355. Mwenye tumbo ni tumbole, angafunga mkaja.

356. Mwenzako akinyolewa wewe tia maji.

357. Mwibaji na watwana, mlifi ni mwungwana.

358. Mwili wa mwenzio ni kando ya mwilio.

359. Mwizi hushikwa na mwizi mwenziwe.

360. Mwomba chumvi huombea chunguche

361. Mwosha hadhuru maiti.

362. Mwosha huoshwa..

363. Mwosha husitiri maiti..

364. Mzaha,mzaha, hutumbuka usaha

365. Mzazi haachi ujusi.

366. Mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi

367. Mzika pembe ndiye mzua pembe.

368. Mzowea kunyonga, kuchinja hawezi.

369. Mzowea kutwaa, kutoa ni vita

370. Mzungu Wa kula hafundishwi mwana..

371. Nadhari njia ya peponi.

372. Nahodha wengi, chombo huenda mrama.

373. Natuone ndipo twambe, kusikia Si kuona

374. Nazi haishindani na jiwe.

375. Nazi mbovu harabu ya nzima.

376. Ndege mjanja hunaswa kwa tundu bovu.

377. Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu

378. Ndege mwigo hana mazoea.

379. Ndoto haihadithiwi.

380. Ndugu chungu, jirani mkungu.

381. Ndugu mwui afadhali kuwa naye

382. Ndugu wakigombana, chukua jembe ukalime,

383. Ngoja ngoja huumiza matumbo.

384. Ngoma ivumayo haidumu.

385. Ngoma ivumayo haikawii kupasuka.

386. Ng'ombe avunjikapo guu hurejea zizini

387. Ng'ombe haelemewi na nunduye.

388. Ng'ombe wa maskini hazai mapacha.

389. Ngozi ivute ili maji.

390. Nguo ya kuazima haisitiri matako.

391. Nia njema ni tabibu, nia mbaya huharibu

392. Nifae na mvua nikufae na jua.

393. Nilikuonyesha nyota, uliona kidoto tu.

394. Nimekula asali udogoni, utamu ungali gegoni.

395. Nimekupaka wanja, wewe wanipaka pilipili

396. Njia ya mwongo fupi.

397. Njia ya siku zote haina alama.

398. Nta si asali; nalikuwa nazo si uchunga.

399. Nyani haoni kundule, huliona la mwenziwe.

400. Nyimbo ya kufunzwa haikeshi ngoma.

401. Nyumba kubwa husitiri mambo makubwa.

402. Nyumba usiyolala ndani huijui ila yake

403. Nyumba ya udongo haihimili vishindo.

404. Nzi kufa juu ya kidonda Si haramu.

405. Ogopa ni ngao pia.

406. Ombaomba huleta unyonge.

407. Ondoa dari uezeke paa.

408. Pabaya pako si pema pa mwenzako

409. Padogo pako si pakubwa pa mwenzako. .

410. Painamapo ndipo painukapo.

411. Paka akiondoka, panya hutawala.

412. Paka akiwa hakimu panya hawezi kushinda kesi.

413. Paka hakubali kulala chali

414. Paka hashibi kwa wali, matilabaye ni panya.

415. Paka wa nyumba haingwa. .

416. Panapo wengi hapaharibiki neno

417. Papo kwa papo kamba hukata jiwe.

418. Pele hupewa msi kucha.

419. Pema usijapo pema; ukipema Si pema tena.

420. Penye kuku wengi hapamwagwi mtama

421. Penye mafundi, hapakosi wanafunzi

422. Penye mbaya wako, hapakosi mwema wako/na mwema wako hakosi.

423. Penye miti hakuna wajenzi .

424. Penye nia, pana njia.

425. Penye urembo ndipo penye urimbo. .

426. Penye wazee hapaharibiki neno

427. Penye wengi pana mengi.

428. Penye wengi pana Mungu.

429. Pilipili usiyoila yakuwashiani?

430. Pofu hasahau mkongoja wake.

431. Pwagu hupata pwaguzi.

432. Radhi ni bora kuliko mali.

433. Radhi ya wazee ni fimbo.

434. Sahani iliyofunikwa, kilichomo kimesitirika.

435. Sahau ni dawa ya waja.

436. Samaki mmoja akioza, huoza wote

437. Shida haina hodi.

438. Shika! Shika! na mwenyewe nyuma

439. Shimo Ia ulimi mkono haufutiki.

440. Shimo la ulimi mkono halifukiki.

441. Shoka la mgeni haliwezi kuimaliza kazi yako.

442. Shoka lisilo mpini halichanji kuni.

443. Si kila mwenye makucha huwa simba.

444. Sikio halilali na njaa.

445. Sikio halipwani kichwa. / Sikio halipiti kichwa. .

446. Sikio la kufa halisikii dawa

447. Siku njema huonekana asubuhi.

448. Siku utakayokwenda uchi ndiyo siku utakayokutana na mkweo.

449. Siku ya kufa nyani miti yote huteleza.

450. Siku za mwizi ni arubaini

451. Simba mwenda kimya(pole) ndiye mla nyama.

452. Simbiko haisimbuki ila kwa msukosuko

453. Siri ya mtungi mwulize kata

454. Sitaacha kula mkate kwa kuogopa kiungulia.

455. Sitafuga ndwele na waganga tele.

456. Sitapiki nyongo harudi haramba.

457. Subira ni ufunguo wa faraja.

458. Subira yavuta heri, huleta kilicho mbali.

459. Sumu ya neno ni neno.

460. Tabia ni mimba haifichiki

461. Tabia ni ngozi ya mwili.

462. Tamaa mbele, mauti nyuma.

463. Tamaa mbele, mauti nyuma.

464. Tamu likizidi tamu huwa si tamu tena

465. Tamu ya mua kifundo.

466. Taratibu ndiyo mwendo..

467. Tawi kavu kuanguka si ajabu.

468. Teke Ia kuku halimwumizi mwanawe

469. Tonga si tuwi

470. Tunda jema halikawii mtini.

471. Ucheshi wa mtoto ni anga Ia nyumba.

472. Uchungu wa mwana, aujua mzazi.

473. Udongo uwahi ungali maji

474. Udugu wa nazi hukutania chunguni

475. Ujana ni moshi.

476. Ukenda kwa wenye chongo, vunja lako jicho.

477. Ukimwiga tembo kunya utapasuka mkundu.

478. Uking'wafua mnofu ukumbuke kuguguna mfupa.

479. Ukiona kwako kunaungua kwa mwenzako kunateketea.

480. Ukiona neno, usiposema neno, hutapatikana na neno.

481. Ukiona vinaelea, vimeundwa.

482. Ukiona zinduna, ambari iko nyuma.

483. Ukipewa shibiri usichukue pima.

484. Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni

485. Ukistahi mke ndugu huzai naye.

486. Ukitaja nyoka, shika fimbo mkononi.

487. Ukitaka kula nguruwe chagua aliyenona

488. Ukitaka salama ya dunia zuia ulimi wako.

489. Ukitaka uzuri sharti udhurike.

490. Ukupigao ndio ukufunzao.

491. Ukuukuu wa kamba si upya wa ukambaa.

492. Ulimi hauna mfupa.

493. Ulimi unauma kuliko meno..

494. Ulipendalo hupati, hupata ujaliwalo.

495. Ulivyoligema utalinywa.

496. Umejigeuza pweza, unajipalia makaa?

497. Umekuwa bata akili kwa watoto?

498. Umekuwa jeta hubanduki?

499. Umekuwa nguva, huhimili kishindo?

500. Unamlaumu mwewe, kipanga yuwesha kuku.

501. Ungalijua alacho nyuki, usingalionja asali.

502. Ushikwapo shikamana.

503. Usiache kunanua kwa kutega

504. Usiache mbachao kwa msala upitao.

505. Usicheze na simba, ukamtia mkono kinywani.

506. Usigombe na mkwezi, nazi imeliwa na mwezi.

507. Usijifanye kuku mweupe.

508. Usikaange mbuyu ukawaachia wenye meno watafune.

509. Usile na kipofu ukamgusa rnkono.

510. Usimwage mtama kwenye kuku wengi

511. Usimwamshe aliyelala, ukimwamsha utalala wewe.

512. Usinivishe kilemba cha ukoka.

513. Usione kwenda mbele kurudi si kazi

514. Usione simba kapigwa na mvua.

515. Usipoziba ufa utajenga ukuta.

516. Usisafiriye na nyota ya mwenzio.

517. Usisahau ubaharia kwa sababu ya unahodha.

518. Usishindane na Kari; Kari ni mja wa Mungu

519. Usitukane wagema na ulevi ungalipo.

520. Usitukane wakunga na uzazi 'ungalipo.

521. Usiyavuke maji usiyoweza kuyaoga.

522. Vita havina macho.

523. Wapiganapo tembo wawili ziumiazo nyasi.

524. Watetea ndizi mgomba si wao.

525. Wengi wape, usipowapa watajichukulia wenyewe

526. Yote yang'aayo si dhahabu.

527. Zana za vita ni silaha.

528. Ziba mwanya usipite panya.

529. Zimwi likujualo halikuli likakwisha

530. Zunguo la mtukutu ni ufito.