Vihusishi (H)

Vihusishi ni maneno yanayotuarifu zaidi kuhusu uhusiano wa nomino na mazingira yake.

Aina za Vihusishi

Vihusishi vya Mahali

mbele ya, nyuma ya Kuna mzoga '_'nyuma ya'_' jengo hilo.
chini ya, juu ya Joto lilipozidi, watoto waliketi '_'chini ya '_' mti ule.
kando ya '_'Kando ya '_' mito ya Babeli ndipo tulipoketi.
karibu na, mbali na Fisi aliambiwa asile mifupa '_'karibu na'_' mtoto yule.

Vihusishi vya Wakati

kabla ya Ni vizuri kusali '_'kabla ya'_' kula chakula.
baada ya Watoto safi hupiga meno mswaki '_'baada ya'_' kila mlo.