Fasihi

Fasihi ni sanaa ya lugha. Fasihi hutumia lugha kutoa sanaa mbalimbali katika jamii.

Tanzu za Fasihi

Kuna tanzu mbili kuu za fasihi, na kila utanzu una vipera vyake: Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi:

Fasihi Simulizi

  1. Hadithi (Ngano) - hekaya, mighani, visasili n.k
  2. Nyimbo - za jandoni, za ndoa, za kazi n.k
  3. Maigizo - michezo ya kuigiza, ngomezi n.k
  4. Tungo Fupi - methali, vitendawili n.k

Fasihi Andishi

  1. Hadithi Fupi - hadithi isiyokuwa ndefu iliyochapishwa katika mkusanyiko wa hadithi nyingine
  2. Riwaya - hadithi ndefu iliyochapishwa katika kitabu chake pekee
  3. Tamthilia - mchezo wa kuigiza uliowekwa kwa maandishi
  4. Ushairi* - mashairi yaliyoandikwa

Tofauti kuu kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi ni kwamba Fasihi Simulizi huwasilishwa kwa njia ya mdomo au matendo ilhali Fasihi Andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishi.

Tanbihi:Ushairi ni kipera cha nyimbo lakini pia mashairi yanaweza kuwa chini ya Fasihi Andishi, ikiwa yamechapishwa.

Tofauti kati ya Fasihi Andishi na Fasihi Simulizi

FASIHI SIMULIZIFASIHI ANDISHI
1. Huwasilishwa kwa njia ya mdomo na/au matendo. Huwasilishwa kwa njia ya maandishi
2. Ni mali ya jamii. Kazi andishi ni mali ya mwandishi (na mchapishaji)
3. Msimulizi anaweza kubadilisha sehemu fulani Kitabu kilichoandikwa hakiwezi kubadilishwa
4. Huhifadhiwa akilini Huhifadhiwa vitabuni
5. Kazi simulizi hubadilika na wakati Kazi andishi haibadiliki na wakati
6. Huhitaji msimulizi na hadhira yake wawe mahali pamoja wakati wa masimulizi Msomaji anaweza kusoma kitabu cha hadithi peke yake, mahali popote, wakati wowote
7. Mtu yeyote anaweza kutunga na kusimulia Ni lazima mwandishi na msomaji wawe na uwezo wa kusoma
8. Hutumia wahusika changamano (wanyama, watu, mazimwi n.k) Hutumia wahusika wanadamu.

Umuhimu wa Fasihi Katika Jamii