Insha za Methali

Methali huwa na pande mbili na ni lazima insha ya methali izipe sehemu zote mbili uzito sawa. Upande mmoja hutoa wazo au pendekezo; na upande wa pili hutoa jibu, suluhisho au matokeo.

Chukua kwa mfano, "Mpanda ngazi hushuka". Katika insha yako ni lazima utoe hoja za kutosha kuonyesha kwamba mhusika fulani kweli alipanda ngazi (k.v alipata cheo kikubwa, alijisifu n.k). Mwandishi pia anapaswa kutoa hoja za kutosha kuonyesha namna mhusika huyo aliposhuka (k.v akafutwa kazi,n.k) . Kwa mara nyingi, wanafunzi huzingatia tu sehemu ya kwanza ya methali katika insha yote huku sehemu ya pili ikijitokeza katika aya ya mwisho pekee.

Kumbuka kwamba ni muhimu kuelewa maana ya methali vizuri kabla ya kuchagua insha ya methali.

Mifano ya Insha za Methali:

Andika inayoonyesha ukweli wa methali ifuatayo. Ifanye insha yako iwe ya kupendeza.

  1. "Usiache mbachao kwa msala upitao"
  2. "Chururu si ndo ndo ndo"
  3. "Siku za Mwizi ni arobaini"