Hadithi Fupi

Hadithi Fupi ni aina ya kazi andishi ambayo huwa fupi; na huangazia wazo moja kwa kurejelea kisa kimoja. Hadithi huwa na wahusika wachache na huchukua muda mfupi. Aghalabu hadithi fupi huchapishwa katika mkusanyiko wa hadithi nyingine fupi.

Mifano ya Hadithi Fupi

Hadithi Fupi kutoka kwenye mkusanyiko wa hadithi katika Mayai Waziri Wa Maradhi na Hadithi Nyinginezo

Tofauti kati ya Hadithi Fupi na Riwaya

HADITHI FUPIRIWAYA
1. Huwa fupi - hadithi fupi nyingi huhitaji kuunganishwa pamoja kuunda kitabu kimoja.Huwa ndefu - huunda kitabu kizima
2. Huwa na wahusika wachache.Huwa na wahusika wengi
3. Hurejelea wazo au kisa kimoja tuHuwa na visa vingi na mawazo mengi yanayojenga wazo kuu
4. Husimuliwa kwa lugha ya moja kwa mojaMasimulizi yake yanaweza kuchanganya visengere nyuma na visengere mbele.
5. Huwa na muundo rahisi kuelewekaAghalabu huwa vigumu kueleweka
6. Hufanyika katika mandhari/mazingira moja tu au chache.Visa mbalimbali hufanyika katika mandhari mbalimbali