Msamiati wa Nyakati na Saa

Siku za Juma

Juma au wiki moja huwa na siku saba. Yafuatayo ni majina ya siku za juma. Kwa kuwa asili yake ni Kiarabu na Kiislamu, Jumamosi ndiyo siku ya kwanza ya wiki; nayo Ijumaa ndiyo siku ya saba.

SIKU YA JUMA KIINGEREZA
Jumatatu Monday
Jumanne Tuesday
Jumatano Wednesday
Alhamisi Thursday
Ijumaa Friday
Jumamosi Saturday
Jumapili Sunday

a id="siku"

Siku Zikilinganishwa na Leo

Haya ni majina tunayotumia kurejelea siku zinazokaribiana na leo.

SIKU MAELEZO MFANO
juzi siku iliyotangulia jana ikiwa leo ni Jumatano, juzi ilikuwa Jumatatu.
jana siku iliyotangulia leo ikiwa leo ni Jumatano, jana ilikuwa Jumanne.
leo siku ambayo tuko sasa hivi
kesho siku inayofuata Ikiwa leo ni Jumatano, kesho itakuwa Alhamisi.
kesho kutwa siku itakayokuja baada ya kesho ikiwa leo ni Jumatano, kesho kutwa itakuwa Ijumaa.
mtondogoo siku itakayokuja baada ya kesho kesho kutwa. siku tatu kutoka leo ikiwa leo ni Jumatano, kesho kutwa itakuwa Jumamosi.

Miezi ya Mwaka

Jedwali lifuatalo linaonyesha majina ya miezi katika mwaka, na idadi ya siku katika kila mwezi.

# JINA MWEZI WA: SIKU
1 Januari kwanza 31
2 Februari pili 28
3 Machi tatu 31
4 Aprili nne 30
5 Mei tano 31
6 Juni sita 30
7 Julai saba 31
8 Agosti nane 31
9 Septemba tisa 30
10 Oktoba kumi 31
11 Novemba kumi na moja 30
12 Disemba kumi na mbili 31

Masaa ya Siku

Yafuatayo ni mafungu ya masaa au nyakati mbalimbali za siku.

WAKATI MAELEZO MASAA
mchana wakati wa siku wenye jua. kutoka saa kumi na mbili asubuhi hadi saa moja jioni hivi 6am - 7pm
usiku wakati wa siku usiokuwa na jua. kutoka saa moja jioni hadi saa kumi na mbili siku inayofuatia 7pm - 6am
alfajiri kati ya saa tisa na saa kumi na moja asubuhi 3am - 5am
macheo saa kumi na moja hadi saa kumi na mbili hivi jua linapochomoza 3am - 5am
asubuhi kutoka saa kumi na mbili hadi saa sita za mchana 6am - 12pm
adhuhuri saa sita za mchana hadi saa nane 12pm - 2pm
alasiri saa nane hadi saa kumi na moja hivi 2pm - 5pm
jioni saa kumi na moja hadi saa moja jioni 5pm - 6pm
machweo/magharibi saa kumi na mbili hadi saa moja jioni; jua linapotua 6pm - 7pm
usiku mchanga kati ya saa moja jioni na saa sita za usiku 7pm - 12am
usiku wa manane kutoka saa sita za usiku hadi alfajiri 12am - 3am

Kusoma Saa

Tunaweza kusoma saa tukitumia:

Mfumo wa Kiswahili

katika mfumo wa Kiswahili/Kibantu, siku huanza saa kumi na mbili asubuhi. Kwa hivyo, saa moja ya asubuhi inakuwa ndiyo saa ya kwanza(1) ya siku.

Mfano:

Mfumo wa Kimataifa/Kiingereza

Huu ndio mfumo unaokubalika kirasmi katika mataifa na lugha mbalimbali. Kulingana na mfumo huu, siku huanza saa sita za usiku. Hivyo basi, saa saba ya usiku inakuwa saa ya kwanza(1) ya siku.

Mfano: