Insha za Barua

Kuna aina mbili za barua:

Pia tutaangalia Barua Kwa Mhariri


Barua ya kirafiki

Barua ya kirafiki ni barua ambayo mtu huandika kwa mwenzake au mtu wa familia yake. Barua hii haichukui mtindo wowote maalum wa kuandikwa. Huwa na anuani moja tu: ya mpokeaji. Barua hii haitumii lugha rasmi na mwandishi anaweza kumrejelea mwandikiwa kwa kutumia jina lake la kwanza. Aidha barua za kirafiki haziitaji kutiwa saini.


Barua Rasmi

Barua rasmi au barua ya kiofisi/kibiashara huzingatia mtindo rasmi wa barua. Huwa na sehemu zifuatazo:

Muundo

  1. Anuwani ya mwaandishi huwekwa juu kabisa na huwa katika upande wa kulia wa kartasi.
  2. Tarehe ya barua hiyo - tarehe huandikwa chini ya anwani ya mwandishi
  3. Anuwani ya mpokeaji - Anwani ya anayeandikiwa huwa katika upande wa kushoto wa kartasi, na huwekwa msitari mmoja chini ya tarehe.
  4. Salamu-Chini ya anwani ya mpokeaji, barua huanza kwa kumrejelea mpokeaji kama bwana au bi. Ni makosa kumsalimia mpokeaji wa barua rasmi au kumwuliza hali yake.
    Kwa Bwana Menomakubwa, => taja jina lake ikiwa mnajuana na unayemwandikia.
    Kwa Bw/Bi, => Ikiwa humjui mpokeaji wa barua, tumia bw/bi
  5. Mada -Kichwa cha barua rasmi huja pindi tu baada ya salamu. Hutangulizwa na maneno kama vile KUH:(kuhusu), MINT:(mintarafu). Ni sharti kiachwe kiandikwe kwa herufi kubwa na kipigiwe mstari. Kichwa kinapaswa kuwa kifupi na kinachoelezea mada ya barua kiukamilifu.
  6. Ujumbe - Ujumbe wa barua rasmi lazima uwe mfupi na unaotumia lugha rasmi.
  7. Tamati – mwandishi humalizia kwa maneno ya hitimisho kama vile:
    Wako mwaminifu,

    [jina]

    Sahihi

Barua kwa Mhariri

Hii ni barua ya msomaji wa jarida kwa mhariri mkuu wa jarida/gazeti fulani akitoa maoni yake kuhusu jambo fulani kama vile uchumi, kisa, sera za serikali au habari zozote zinazoendelea kwa wakati huo.

k.m:

Kwa Mhariri Mkuu

Jarida la Mwenda Zake Leo

MINT : HATUA YA SERIKALI KUFADHILI SEKTA YA BODABODA



...ujumbe...

Na [jina]