Ngano Katika Fasihi Simulizi

Hadithi (ngano) ni utungo wenye visa vya kubuni unaosimuliwa kwa lugha nathari kwa kusudi la kuburudisha, kukuza maadili na kuunganisha jamii. Msimulizi wa hadithi huitwa Fanani au Mtambaji.

Vipera vya Ngano

Tunaweza kuainisha ngano kulingana na vipengele vifuatavyo:

Utanzu huu wa fasihi simulizi umegawanyika katika vipera (aina) kadhaa:

AINA MAELEZO KWA UFUPI
Khurafa hadithi ambazo wahusika ni wanyama.
Hekaya mhusika mmoja (k.v sungura) huwa mjanja kuliko wenzake
Usuli (Visaviini) huelezea chanzo cha jambo au hali fulani
Visasili huelezea asili au chimbuko la jamii au mambo ya kiada k.v mauti, ndoa, tohara n.k.
Mighani (Visakale) hadithi za mashujaa
Mazimwi huwa na wahusika majitu au mazimwi
Mtanziko humwacha mhusika katika hali ya kutojua chaguo linalofaa. Kila achagualo lina matukio mabaya.

Sifa za Ngano

  1. Huwa na mianzo maalumu
    • Paukwa! Pakawa!
    • "Hadithi! Hadithi!" - "Hadithi Njoo!"
    • Hapo zamani za kale...
  2. Huwa na miishio maalum
    • Hadithi yangu yaishia papo!
    • ...wakaishi kwa raha mustarehe.
  3. Huwa na funzo fulani ambalo aghalabu hutajwa mwishoni mwa hadithi.
  4. Masimulizi yake huwa kwa wakati uliopita
  5. Husimuliwa kwa lugha ya natharia
  6. Huwa na wahusika ambao wanaweza kuwa binadamu, wanyama, miungu, mashetani au vitu visivyo hai
  7. Huhusisha mbinu nyingine za fasihi simulizi kama vile
    • Nyimbo - kuburudisha, kuamsha hadhira, kupitisha ujumbe
    • Methali - kutoa funzo
    • Misemo - kupamba lugha
    • Vitendawili na mafumbo - kushirikisha hadhira katika masimulizi
  8. Hutumia mbinu ya takriri ili kusisitiza ujumbe kwa kurudiarudia maneno, matukio au nyimbo
  9. Hutumia tamathali za lugha kama vile tashbihi, tashihisi, chuku, tanakali za sauti ili kupamba masimulizi n.k
  10. Huwa na muundo rahisi wenye mwanzo, kati na mwisho.
  11. Ufanisi wake hutegemea mbinu za mtambaji k.v ishara-uso na ubunifu wake jukwaani.
  12. Sehemu fulani zinaweza kubadilishwa kulingana na hadhira

Umuhimu wa Ngano

Sifa za Mtambaji wa Hadithi

Msimulizi wa hadithi pia huitwa mtambaji, fanani au mganaji.