Khurafa

Hurafa au Khurafa ni hadithi ambazo wahusika wake huwa ni wanyama. Hadithi hizi hunuia kuangazia tabia za kibinadamu kupitia kwa wanyama. Hadithi nyingi huwa ni za khurafa ambapo wanyama hupewa uwezo wa kibinadamu wa kuongea, kufanya kazi, kufikiri na nyinginezo.

Kwa kuwa wahusika wote katika hadithi za aina hii ni wanyama kutoka mwanzo hadi mwisho, hatuwezi kusema kwamba mbinu ya uhuishaji/tashihisi imetumika.

Sifa za Khurafa

  1. Wahusika wake ni wanyama wenye uwezo wa kuongea na kufanya kama binadamu
  2. Hurejelea maswala yanayopatikana katika jamii zetu kama utendaji kazi, ukuzaji uchumi, uongozi, utangamano katika jamii, n.k
  3. Funzo lake huwa wazi kv tamaa, ujinga n.k


Umuhimu wa Khurafa

  1. Kuburudisha hadhira
  2. Kuelimisha watoto kuhusu wanyama mbalimbali na sifa zao
  3. Kukuza maadili katika jamii
  4. Kuelekeza na kunasihi
  5. Kupitisha muda


Mifano

MNYAMASIFA
Sunguratabia za ujanja - sungura huwakilisha watu wasiopenda kuchoka/kufanya kazi lakini hutumia ujanja wao kula jasho la wengine, au kuwaangamiza adui zao.
Simbakwa mara nyingi simba hutumika kama kiongozi/mfalme - huwakilisha watu wenye ukali katika jamii, ambao wakiongea husikika na huogopewa sana.
FisiNi mhusika mwenye tamaa na ulafi ambaye fikira zake zimetawaliwa na tamaa yake. Fisi hutumika kuwakilisha wanadamu wazembe na wajinga, wasiopenda kufikiria sana kwani mawazo yao yamejikita katika tamaa zao.
NyaniAnapotumika katika hadithi, hudhihirisha hekima na uwezo wa kufanya uamuzi wa busara. Nyani hutumika sana kama hakimu na huwakilisha viongozi wenye hekima katika jamii.
Nyokani mnyama mwenye hila na huwakilisha watu wenye hila katika jamii.
Kobe huwakilisha watu wanyamavu, ambao japo wanajua kufanya kitu, hawapendi kuchangia, lakini mwisho huibuka washindi; watu wasiokimbilia kufanya mambo
Ndovu huwakilisha watu wenye kimbelembele, ambao hujisifu na kujitafutia umaarufu. Watu wa aina hii hupenda kuwa katika msitari wa mbele japo huenda hawana ujuzi wa kutosha katika jambo lilo.