Maigizo

Maigizo ni sanaa katika fasihi simulizi ambayo watendaji huwa ndio wahusika. Maigizo hayasimuliwi kama mbinu nyingine za fasihi. Wahusika ndio huzungumza katika sehemu zao mbalimbali.
Mifano:
  1. Michezo ya Kuigiza (Jukwaani) - Haya ni maigizo ya jukwaani ambapo watendaji huiga maneno na matendo ya wahusika mbele ya hadhira.
  2. Miviga - Miviga ni sherehe mbalimbali katika jamii fulani. Watu hujumukika na sherehe hizi kulingana na tamaduni zao
  3. Ngomezi - ni sanaa ya ngoma. Midundo mbalimbali ya ngoma hutumika kuwasilisha ujumbe mbalimbali.
  4. Malumbano ya Utani - Malumbano ya utani ni mashindano ya kuongea jukwaani baina ya watu wa makundi au jamii mbili ambayo hutumia kejeli na chuku kukejeli tabia mbaya katika jamii au kundi fulani
  5. Ulumbi - Ulumbi ni uwezo wa kipekee wa kuzungumza mbele ya hadhira. Mtu mwenye uwezo huo wa kipekee wa kuzungumza jukwaani huitwa mlumbi.
  6. Soga - Soga ni mazungumzo baina ya watu wawili au zaidi ambayo aghalabu huwa hayana mada maalum.
  7. Vichekesho - Vichekesho ni aina ya sanaa ya fasihi simulizi ambayo watu hutoa vihadithi vifupi au sentensi zenye uwezo wa kuwafanya wasikilizaji wacheke.
  8. Maonyesho ya Sanaa - Maonyesho huhusisha watu wa jamii au kundi fulani wanaoonyesha taaluma, ujuzi au sanaa yao kwa watazamaji.