Michezo ya Kuigiza

Haya ni maigizo ya jukwaani ambapo watendaji huiga maneno na matendo ya wahusika na kuyasema wakiwa kwenye jukwaani. Jukwaa hutayarishwa ili kuiga mazingira ya tamthilia au tukio wanaloliigiza.

Sifa za Michezo ya Kuigiza

  1. Huwa na wahusika ambao huwakilishwa na watendaji.
  2. Hufanyika kwenye jukwaa mbele ya hadhira
  3. Huhitaji kumbukumbu ili kukumbuka maneno ambayo mhusika anapaswa kusema katika jukwaa
  4. Vitambaa au mwangaza hutumiwa ili kuashiria kubadilika kwa mazingira au wakati
  5. Hutumia mbinu za lugha kama vile chuku, tanakali za sauti, tamathali na nyinginezo
  6. Hujumulisha aina nyingine za sanaa kama vile ushairi na nyimbo.

Umuhimu wa Michezo ya Kuigiza

  1. Huburudisha
  2. Huelimisha
  3. Hukuza uwezo wa kukumbuka kwa watendaji