Ratiba

Ratiba ni orodha ya mpangilio wa namna mambo yatakavyofuatana katika shughuli fulani. Lengo lake ni kuhakikisha wakati unatumiwa vizuri ili mambo fulani yasije yakakosa kutendwa kutokana na upungufu wa wakati.

Ratiba hutumika katika sherehe, mikutano, mazishi, hafla, tamasha, n.k


Sehemu za Ratiba

  1. Kichwa

    Kichwa cha ratiba hutaja mambo yafuatayo:
    1. Shughuli yenyewe - Taja jina la tukio ambalo unaandalia ratiba. Kwa mfano Harusi ya Bwana na Bi Arusi, Siku ya Zawadi
    2. Tarehe ya shughuli - je shughuli hiyo itafanyika lini?
    3. Mahali- Taja mahali ambapo shughuli hiyo itafanyikia. kwa mfano katika uwanja wa michezo wa Kasarani, kanisa la St. Mtakatifu

    Mfano wa kichwa cha ratiba:

    • Ratiba ya Hafla ya Ukimwi katika Bustani la Uhuru tarehe tano Januari.
    • Ratiba ya Mazishi ya Dkt. Marehemu tarehe 20/12/1923 Kijijini Vikwazoni

  2. Mwili

    Mwili wa ratiba hujumuisha mambo mbalimbali yatakayofanyika katika mpangilio maalum, saa mbalimbali. Ni vizuri kuzingatia vipengele vifuatavyo:

    1. Saa - Onyesha saa ambazo tukio limepangiwa kuanza hadi linapotakiwa kumalizika
    2. Mahali - Ikiwa shughuli tofauti zinafanyika katika mahali mbalimbali kama vile vyumba tofauti, inapaswa hutaje mahali ambapo kila jambo litafanyikia.
    3. Wahusika - Taja mtu au watu waliopewa wajibu wa kutekeleza jambo fulani. Hii huwasaidia kujitayarisha ipasavyo.

Mfano wa Ratiba

RATIBA YA MAZISHI YA MZEE MAUTI TAREHE 20/12/1923 KIJIJINI MIZUKANI

SAASHUGHULI
07: 00Marafiki wa Mauti watoa mwili kutoka SlowDeath Hospital
10: 30Maombi katika kanisa la G.I.Z.A yakiongozwa na Pst. Muna Fiki
11: 15Mwili kuwasilishwa nyumbani, familia ya Mauti
12: 00 Kupakuliwa kwa chakula na Bi Kamafisi, Bi Mwachafu na wapishi walioteuliwa
1: 10 Kukusanyika kwa umati
2: 00 Maombi ya kuanzisha shughuli za mazishi
2: 30 Shuhuda zikiongozwa na Mzee Siachwinyuma
3: 00 Ushuhuda wa serikali na Chifu Mtesi
3: 40 Kuteremshwa kwa mwili kaburini na vijana walioteuliwa
4: 00 Shukrani za Mwisho, na Mwenyekiti wa Chama cha Kufa Tukusaidie
6: 00 Kugawana mali ya marehemu, na wazee wa kijiji