Resipe

Haya ni maandishi yanayotoa maagizo/maelekezo ya kuandaa chakula fulani.


Sehemu muhimu za resipe ni:

  1. Kichwa- Jina la mlo unaoandaa, Idadi ya watu wanaopikiwa
  2. Orodha ya viungo unavyohitaji- majina ya viungo, Idadi au kiasi kinachohitajika
  3. Maagizo/namna ya kupika
  4. Eleza kwa utaratibu kila hatua
  5. Taja wakati utakaotumika katika kila hatua.
  6. Hakikisha kila aina ya viungo ulivyotaja, inajitokeza katika maelezo ya kupika.
  7. Tamati
  8. Baada ya chakula kuiva, eleza kinaweza kupakuliwa na chakula kipi kinginecho k.v ugali na kitoweo cha kuku

Mfano

  1. Andika resipe ya kuandaa mchuzi wa kuku kwa watu watano.
  2. Andika resipe ya kuandaa chakula kwa mgonjwa wa moyo