Takriri

TAKRIRI
Pia Huitwa Ukariri
Kiingereza Repetition
Kitengo Tamathali za Usemi
Aina ya Mbinu / Fani za Lugha

Prev Chuku
Next Tanakuzi

Ni mbinu ya kurudiarudia neno moja au kifungu cha maneno ili kusisitiza ujumbe fulani. Isitoshe, takriri inaweza kujitokeza kwa kurudia rudio wazo fulani katika kazi ya sanaa. Repetition .

  • Tumechoshwa na siasa mbaya. Tumechoshwa na ahadi zisizotimizwa. Tumechoshwa na miradi isiyo kamilika. Tumechoshwa na malumbano na migogoro ya kikabila. Tumechoka.
  • Hongera hongera Bwana Kisaka, hongera kwa ujasiri wako. Hongera! uliyoyatenda ni raha kwetu. hongera


  • Comments