Mighani au Visakale

Visakale ni hadithi za mashujaa wanaosifiwa katika jamii. Aghalabu mashujaa hawa walipigania jamii zao katika vita dhidi ya jamii nyingine au vita vya ukombozi. Shujaa katika visakale huitwa jagina. Maadui wa mashujaa huitwa Majahili

Sifa za Mighani

  1. Hutumia chuku kusifia matendo na uwezo wa shujaa.
  2. Majagina huwa na uwezo wa ukiamaumbile (uwezo unaozidi wa binadamu)
  3. Huwa ni vigumu sana kwa shujaa kuuawa minghairi ya idadi ya maadui wake
  4. Shujaa huwa na siri kuu ya nguvu zake (kama nguvu kuwa kwenye kivuli, nywele, n.k)
  5. Jagina hupigania haki za jamii yake
  6. Jamii ya jagina huwakilisha wema ilhali maadui wao huwakilisha ubaya.
  7. Jagina hufa mwishoni, haswa baada ya kusalitiwa na mtu wake.
  8. Hadithi hizi huaminika kuwa za kweli ama zenye kiwango fulani cha ukweli; kwamba mashujaa hao walikuwa.

Sifa za Jagina (Shujaa)

  1. Huwa na nguvu zinazotokana na siri fulani
  2. Wana uwezo wa ukiamaumbile
  3. Hupigania haki za jamii yao
  4. Huwa na kimo kisichokuwa cha kawaida k.v mfupi sana, mrefu sana n.k
  5. Aghalabu huwa watu wema kulingana na maadili ya jamii zao.


Umuhimu wa Visakale

  1. Kuunganisha jamii
  2. Kuhifadhi historia ya jamii
  3. Kuelimisha, kunasihi na kuelekeza
  4. Kuburudisha
  5. Kupitisha muda


Mifano ya Majagina


JAGINAKABILA
Mekatilili wa MenzaGiriamaMwanamke aliyeongoza wanandi dhidi ya wakoloni
Fumo wa LinyongoWapateVita dhidi ya Sultani wa Pate
Kinjeketile NgwaleWamatumbiMajimaji Rebellion
Luanda MagereLuoVita dhidi ya Wanandi
Koitalel arap Samoei NandiNandi Rebellion
ShakaZuluAliongezea ufalme wa Kizulu