Ngano za Mtanziko

Hadithi za mtanziko ni ngano ambazo mhusika hulazimika kuchagua mojawapo ya hali mbili ambazo ni ngumu kuamua ili kupata suluhisho la jambo fulani. Uamuzi wowote anaoufanya huwa na mabaya yake. Ni jukumu la mhusika kufikiri sana kabla ya kufanya uamuzi

Sifa za hadithi za Mtanziko

  1. Kuna mambo mawili ambayo mhusika analazimika kuchagua moja.
  2. Uamuzi huwa mgumu kwa vile kila chaguo huwa na matokeo yake mabaya
  3. Mhusika huwa na tatizo moja kuu ambalo linaweza tu kutatuliwa na uamuzi atakaofanya.
  4. Aghalabu hutumia mbinu ya taharuki
  5. Aghalabu huishia kwa swali k.v, Ingekuwa wewe, ungefanyaje?


Umuhimu wa Hadithi za Mtanziko

  1. Kukuza uwezo wa kufikiri wa hadhira
  2. Kunasihi hadhira wafanye uamuzi wa busara.
  3. Kuzua mjadala nyeti katika jamii
  4. Kuburudisha hadhira
  5. Kupitisha muda


Mifano


  1. Zimwi linakuamuru ulipatie mama yako aliyekuzaa na kukulea au mke wako unayempenda sana