Upeo
Upeo wa Juu (climax)
Ni sehemu ya hadithi ambayo matukio yanafanyika kulingana na mapenzi ya hadhira au msomaji.
- Siri tuliyokuwa tukiisubiri kwa hamu na ghamu imefumbuliwa. Tunashusha pumzi.
- Ingawa walipitia dhuluma chungu nzima, wahusika wakuu tunaowaopenda, wanawashinda maadaui zao; wanaoana na kuishi kwa raha mustarehe.
Upeo wa Chini (anti-climax)
Ni sehemu ya hadithi ambayo matukio yanafanyika kinyume na mapenzi ya hadhira au msomaji. Aghalabu upeo wa chini hutokea baada ya upeo wa juu.
- Baada ya vifungu vilivyojaa vituko kemkem, mambo yanatulia; tushafumbuliwa mafumbo yote lakini bado hadithi inaendelea.
- Siku chache baada ya mhusika mkuu kuibuka mshindi, anavamiwa na kuuawa. Anazikwa kwa huzuni nyingi sana.