Paneli la Kiswahili ni tovuti ya kielimu inayosaidia kukuza ukwasi wa Kiswahili miongoni mwa wanafunzi na walimu, kote Afrika Mashariki.

Lugha

Katika matumizi ya lugha, tunaangalia sarufi (sheria na kanuni) za Kiswahili kwa kuzingatia vipashio vya lugha mbalimbali kama vile sauti za Kiswahili, aina za maneno, ngeli, nyakati, ukanushaji, uakifishaji, uainishaji wa maneno, aina na muundo wa sentensi na kadhalika.

Fasihi

Fasihi ni sanaa ya lugha. Katika Fasihi tunaangazia vipera mbalimbali vya Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi kwa kuzingatia maana, sifa, umuhimu wake. Katika ushairi tutazingatia aina za mashairi, muundo wa mashairi na uchambuzi wa mashairi. Isitoshe, tutamulika tamathali za usemi (mbinu za lugha na mbinu za sanaa) mbalimbali zinazotumika Katika fasihi ya Kiswahili.

Insha

Jifunze jinsi ya kuandika insha mbalimbali - za kubuni na za kiuamilifu.

Isimu Jamii

Tumekuandalia istilahi mbalimbali za Isimu Jamii pamoja na sifa za lugha katika sajili mbalimbali.