Insha za Kiuamilifu

Hizi ni insha amabazo huchukua mtindo maalum wa kuandikwa. Japo mwanafunzi anaweza kubuni maudhui katika insha yake, hana uhuru wa kujichagulia muundo atakaotumia kuwasilisha utunzi wake bali anapaswa kuzingatia mtindo maalum wa kuandika insha hiyo.


Tumekuandalia Insha zifuatazo:

INSHA MAELEZO KWA UFUPI
Hotuba andika hotuba kwa hadhira kuhusu mada fulani
Kumbukumbu rekodi za mkutano
Resipe orodha ya viungo na maelekezo ya kuandaa chakula fulani.
Ratiba mpangilio wa mambo katika shughuli fulani
Mazungumzo majadiliano baina ya watu wawili au zaidi
Mahojiano mazungumzo ambapo mtu mmoja anamhoji/kumwuliza maswali mwenzake
Barua muundo wa barua rasmi, barua ya kirafiki na barua kwa mhariri
Tahariri maoni ya mwandishi/mhariri
Wasifu simulia maisha ya mtu mwengine
Tawasifu simulia maisha yako mwenyewe
Mjadala toa maoni yako kuhusu hoja fulani