Mwalimu: |
Mzee Kundu, ningetaka tuzungumze kwa muda kuhusu hali ya mwanao, Machome Kundu. |
Mzee: |
Machome? Ana nini mwanangu. Kuna nafasi imepatikana ya… |
Mwalimu: |
Mwanako amebadilika sana kitabia. Alikuwa akifanya vizuri sana katika masomo |
Mzee: |
Kweli kabisa. Mimi ni mlezi mwema sizai watoto mbu mbu mbu darasani. |
Mwalimu: |
Ndivyo. Lakini sasa naona ameanza kubadilika. Ameanza kulegea katika mitihani na kuzembea kazini. |
Mzee: |
Unamaanisha nini? (akiinuka) Inaonekana siku hizi hamjui kuwapa adabu watoto. Ni lazima mtoto wangu amepotoshwa na wengine, katika vikundi vibaya! |
Mwalimu: |
Hakika, mwanako ndiye anayepotosha wanafunzi wengine. Yeye ni kiongozi wa makundi haramu shuleni, yanayovuruga masomo, kuuza dawa za kulevya na mambo kama haya. Hii ndiyo sababu nimekuita tujadiliane. Ni lazima mienendo hii imechipuka nyumbani. |
Mzee: |
Ajapo nyumbani, mwanangu huzingatia vitabu pekee hata mamake anaweza kuthibitisha haya. Ikiwa kuna utovu wa nidhamu nina hakika haya yanatoka darasani. |
Mwalimu: |
Tafadhali keti mzee (akichungulia dirishani) Mtindi! Niitie Machome… |
Mwalimu: |
Toeni vitabu vyenu vya Historia mnakili haya. Ni nani atakayetukumbusha tulichosoma wiki jana? Naam Halima! |
Halima: |
Tulisoma kuhusu Chama cha Mapinduzi |
Wanafunzi: |
(Wakiinua mikono na kupiga kelele) Mwalimu Mwalimu |
Mwalimu: |
Inueni mikono nitawaona. Msipige kelele. Halima umenoa. Simama! Mwanafunzi mwengine? |
Jadaha: |
Tulisoma kuhusu kundi asi la Maji Moto lililopinga wakoloni. |
Wanafunzi: |
Mwalimu! Mwalimu! Kundi la Maji Maji. |
Mwalimu: |
Naam mmepata. Lakini nimewaambia msijibu kwa pamoja. Ukitaka kujibu uinue mikono. Jadaha, ni kundi la Maji Maji siyo Maji Moto. Leo tutasoma athari za kundi katika taifa letu la Tanzania na namna lilivyoshindwa nguvu. Lakini kabla hatujaendelea ningependa mniambie, ni matatizo yepi yaliyochochea kuchipuka kwa kundi hilo. |
Kirata: |
Mwalimu nina swali. Kiongozi wa kundi hilo alikuwa nani? |
Mwalimu: |
Kirata hukuwa darasani wiki jana. Nione baada ya kipindi hiki. (wanafunzi wakicheka) Nawe wafanyani na kitabu cha Hisabati katika somo la Historia. Kimbia ofisini uniletee kiboko. Ninyi ndio mnaorejesha nyuma darasa langu katika mitihani. |