Sajili ya Kisayansi
Sifa za Lugha ya Kisayansi
- Hutumia msamiati wa kipekee unaoambatana na taaluma inayorejelewa.
- Huwa na maelezo kwa ukamilifu.
- Huwa na mpangilio maalum na maendelezo ya hoja na ujumbe.
- Huchanganya ndimi na kutumia maneno ya kisayansi au lugha mbalimbali.
- Hutumia lugha sanifu.
- Ni lugha yenye udadisi mwingi (wakati wa kufanya utafiti)
Mfano wa Lugha ya Kisayansi
Kwa sababu zisizoweza kuepukika, kikundi chetu hakitamaliza utafiti ulioratibiwa kukamilishwa mwishoni mwa mwezi ujao. Hii ni kwa sababu ya changamoto kadhaa ambazo tumekutana nazo. Kwanza, viluwiluwi, ambao ndio tunaotafiti wamekuwa haba sana wakati huu wa ukame. Pili, kutokana na kufungwa kwa maabara ya kisayansi katika taasisi hii, ni muhali kufanya majaribio yoyote ya kazi yetu. Tatu, kumekuwa na pingamizi kubwa kutoka kwa baadhi ya wanakijiji kwamba kukusanya viluwiluwi kunawatia hofu. Aidha, tume yetu imepungukiwa na fedha baada ya serikali kusitisha kudhamini utafiti huu.
Baada ya kujadiliana kwa vikao tatu mfululizo, tume yetu inapendekeza haya: Muda wa kufanya utafiti uongezewe kwa kipindi cha miezi sita; serikali kupitia kwa taasisi hii ifadhili wachunguzi. Wananchi wahamasishwe kuhusu umuhimu wa kuwafanyia viwavi utafiti na maabara ya utafiti ikaraatiwe haraka iwezekanayo.