Msamiati wa Kazi

Huu ni msamiati wa watu wanaofanya kazi mbalimbali.

Mifano

 1. dobi:
  hufanya kazi ya kuosha nguo
 2. karani:
  anayeangalia matumizi ya pesa katika benki au kampuni fulani
 3. katibu:
  anayeweka rekodi za mambo na orodha mbalimbali katika kampuni au idara fulani
 4. kungwi:
  hufunza vijana jandoni
 5. mchuhuzi:
  anayeuza bidhaa kutoka nyumba hadi nyumba
 6. mfinyanzi:
  hufinyanga udongo kutengeza vyombo kama vyungu, n.k
 7. mhandasi:
  anayefanya kazi ya kuunda au kurekebisha injini/mashine mbalimbali
 8. mhasibu:
  mtu anayefanya kazi ya hesabu
 9. mhunzi:
  hufua vyuma
 10. mkatabi:
  anayeweka rekodi za vitabu katika maktaba, na kuwasaidia wanaotaka kuomba vitabu.
 11. tabibu:
  anayetibu watu
 12. topasi:
  kazi ya kuosha vyoo