Sauti za Kiswahili
Sauti ni sehemu ndogo kabisa ya neno ambayo haiwezi kugawika zaidi. Sauti nyingi huwa ni herufi moja ya alfabeti kama vile (a, b, d) lakini kunazo sauti zinazoundwa kwa kuungunisha herufi mbili au zaidi (kama vile ng, nd, mb).
Alphabeti ya Kiswahili: a, b, ch, d, e, f, g, h, i, k, l, m, n, o, p, r, s, t, u, v, w, y, z
Kuna aina mbili za Sauti katika lugha ya Kiswahili:
- Irabu
- Konsonanti
Irabu (Vokali)
(a, e, i, o, u)
Irabu zinapotamkwa, hewa haizuiliwi katika ala za matamshi.
Jedwali lifuatalo litakuonyesha jinsi ya kubainisha vokali kulingana na sehemu ya ulimi inayoachilia hewa, na jinsi midomo inavyobadilika
Irabu | Sehemu ya Ulimi | Midomo |
e,i | Mbele | Midomo imetandazwa |
a | Katikati; ulimi huinuka na kutandaza | Midomo imetandazwa |
o,u | Nyuma | Midomo imevirigwa |
Konsonanti
(b, ch, d, f, g, h, j, k, l, m, n, p, r, s, t, v,w, y, z)
Konsontanti zinapotamkwa, hewa huzuiliwa katika ala za matamshi ( ulimi na midomo). Kuna aina mbili kuu za sauti za konsonanti:
- Sauti Ghuna => konsonanti hizi zinapotamkwa, hewa hutikisa nyuzi za sauti
- Sauti Sighuna => konsonanti hizi zinapotamkwa, hewa haitikisi nyuzi za sauti
Jedwali lifuatalo litakuonyesha aina za konsonanti kulingana na mahali zinapotamkiwa na sauti (ghuna au sighuna)
Midomo | Midomo + Meno | Meno + Ulimi | Ufizi | Kaakaa + ufizi | Kaakaa gumu | Kaakaa Laini | Koo | Aina ya Sauti | |
Vipasuo | pd | td | j | kg | sighuna ghuna | ||||
Vikwamizo / Vikwaruzo | f v | th dh | sz | sh | khgh | h | sighuna ghuna | ||
Kipasuo - kwamizo | ch | sighuna | |||||||
Nazali / Ving'ong'o | m | n | ny | ng' | ghuna | ||||
Kitambaza | l | ghuna | |||||||
Kimadende | r | ghuna | |||||||
Viyeyusho / Nusu Irabu | y | w | ghuna |
Vipasuo ( p,b,k,g,t,d )
Hutamkwa kwa kukutanisha ala za kutamkia ili kufungilia hewa na kisha kuiachilia ghafla
- Vipasuo sighuna (p, k, t ) - hutamkwa bila kutikisa nyuzi za sauti
- Vipasuo ghuna (b, g, d ) - hutamkwa kwa kutikisa nyuzi za sauti
/p/ na /b/ hutamkwa kwa kukutanisha midomo katika meno:
- /p/ - papa, pepea, pipi, popo, pua
- /b/ - baba, bebea, bibi, bobo, bubu
/t/ na /d/ hutamkwa kwa kukutanisha ufizi na ncha ya ulimi
- /t/ - taa, tetea, titi, toto, tua
- /d/ dada, doa, dua
/k/ na /g/ hutamkwa kwa kukutanisha nyuma ya ulimi na kaakaa laini
- /k/ - kaka, koko, kuku
- /g/ - gae, gege, gogo, gugu
Vikwamizo ( d f,v,dh,th, s,z,sh,h,gh)
Pia huitwa Vikwaruzo. Hutamkwa kwa kukutanisha ala za matamshi na kisha kuachilia hewa kupitia katika mwanya mwembamba
- Vikwamizo sighuna (f,th,s,kh,h,sh) - hewa haitikisi nyuzi za sauti
- Vikwamizo ghuna (v, dh,z,gh) - hewa hutikisa nyuzi za sauti
/f/ na /v/ hutamkwa kwa kukutanisha mdomo wa chini na wa juu na kuachilia hewa kidogo kupita
- /f/ - faa, fee, fua
- /v/ - vaa, vua
/s/ na /z/ hutamkwa kwa kukutanisha sehemu ya kati ya ulimi na kaakaa gumu
- /s/ - sasa, sisi
- /z/ - zaa, zeze, zizi, zuzu
/dh/ na /th/ hutamkwa kwa kukutanisha ncha ya ulimi na meno ya juu
- /dh/ - dharau, dhani
- /th/ - thubutu
/gh/ na /kh/ hutamkwa kwa kukutanisha kaakaa laini na kilimi
- /dh/ - dharau, dhani
- /th/ - thubutu
/h/ hutamkwa kwa kukutanisha kilimi na koo na kuachilia hewa kwa nguvu
- /h/ - haha, hii, huu
Kipasuo-kwamizo: ( ch )
Pia huitwa kituo-kwamizo. Hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na ufizi, na kuachilia hewa
- /ch/ - chacha, chechea, choo
Ving'ong'o / Nazali ( m,n,ng',ny )
Hutamkwa kwa kukutanisha ala za matamshi na kuzuia hewa kupitia kinywani; hewa hupitia puani.
/m/ hutamkwa kwa kukutanisha mdomo wa juu na wa chini, ili kuzuia pumzi kupita kinywani
- /m/ - mama, umeme, mimi,
/n/ hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na ufizi, ili hewa ipitie puani
- /n/ - nana, nene, nini, nono, nunua
/ny/ hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na kaakaa gumu
- /ny/ - nyanya, nyenyea, nyinyi, nyoa, nyunyu
/ng'/ hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na kaakaa laini
- /ng'/ - ng'ang'a, ng'oa
Kitambaza ( l )
Hutamkwa kwa kukutanisha ncha ya ulimi na ufizi huku hewa ikipitia kwenye pande za ulimi bila kukwaruza ufizi
- /l/ - lala, lea, lilia, lo! lulu
Kimadende ( r )
Hutamkwa kwa kupigapiga na kukwaruza ufizi haraka haraka kwa ncha ya ulimi.
- /r/ - rai, rarua,
Viyeyusho ( y,w )
Pia huitwa nusu-irabu. Hutamkwa kwa utaratibu kwa kuleta ala za matamshi karibu sana lakini kuachilia hewa bila kuikwaruza.
/w/ hutamkwa midomo ikiwa wazi
- /w/ - wawa, wewe,
/y/ hutamkiwa kwenye kaakaa gumu
- /y/ - yaya, yeye,