Msamiati wa Nyakati na Saa
Siku za Juma
Juma au wiki moja huwa na siku saba. Yafuatayo ni majina ya siku za juma. Kwa kuwa asili yake ni Kiarabu na Kiislamu, Jumamosi ndiyo siku ya kwanza ya wiki; nayo Ijumaa ndiyo siku ya saba.
SIKU YA JUMA | KIINGEREZA |
Jumatatu | Monday |
Jumanne | Tuesday |
Jumatano | Wednesday |
Alhamisi | Thursday |
Ijumaa | Friday |
Jumamosi | Saturday |
Jumapili | Sunday |
Siku Zikilinganishwa na Leo
Haya ni majina tunayotumia kurejelea siku zinazokaribiana na leo.
SIKU | MAELEZO | MFANO |
juzi | siku iliyotangulia jana | ikiwa leo ni Jumatano, juzi ilikuwa Jumatatu. |
jana | siku iliyotangulia leo | ikiwa leo ni Jumatano, jana ilikuwa Jumanne. |
leo | siku ambayo tuko sasa hivi | |
kesho | siku inayofuata | Ikiwa leo ni Jumatano, kesho itakuwa Alhamisi. |
kesho kutwa | siku itakayokuja baada ya kesho | ikiwa leo ni Jumatano, kesho kutwa itakuwa Ijumaa. |
mtondogoo | siku itakayokuja baada ya kesho kesho kutwa. siku tatu kutoka leo | ikiwa leo ni Jumatano, kesho kutwa itakuwa Jumamosi. |
Miezi ya Mwaka
Jedwali lifuatalo linaonyesha majina ya miezi katika mwaka, na idadi ya siku katika kila mwezi.
# | JINA | MWEZI WA: | SIKU |
1 | Januari | kwanza | 31 |
2 | Februari | pili | 28 |
3 | Machi | tatu | 31 |
4 | Aprili | nne | 30 |
5 | Mei | tano | 31 |
6 | Juni | sita | 30 |
7 | Julai | saba | 31 |
8 | Agosti | nane | 31 |
9 | Septemba | tisa | 30 |
10 | Oktoba | kumi | 31 |
11 | Novemba | kumi na moja | 30 |
12 | Disemba | kumi na mbili | 31 |
Masaa ya Siku
Yafuatayo ni mafungu ya masaa au nyakati mbalimbali za siku.
WAKATI | MAELEZO | MASAA |
mchana | wakati wa siku wenye jua. kutoka saa kumi na mbili asubuhi hadi saa moja jioni hivi | 6am - 7pm |
usiku | wakati wa siku usiokuwa na jua. kutoka saa moja jioni hadi saa kumi na mbili siku inayofuatia | 7pm - 6am |
alfajiri | kati ya saa tisa na saa kumi na moja asubuhi | 3am - 5am |
macheo | saa kumi na moja hadi saa kumi na mbili hivi jua linapochomoza | 3am - 5am |
asubuhi | kutoka saa kumi na mbili hadi saa sita za mchana | 6am - 12pm |
adhuhuri | saa sita za mchana hadi saa nane | 12pm - 2pm |
alasiri | saa nane hadi saa kumi na moja hivi | 2pm - 5pm |
jioni | saa kumi na moja hadi saa moja jioni | 5pm - 6pm |
machweo/magharibi | saa kumi na mbili hadi saa moja jioni; jua linapotua | 6pm - 7pm |
usiku mchanga | kati ya saa moja jioni na saa sita za usiku | 7pm - 12am |
usiku wa manane | kutoka saa sita za usiku hadi alfajiri | 12am - 3am |
Kusoma Saa
Tunaweza kusoma saa tukitumia:
Mfumo wa Kiswahili
katika mfumo wa Kiswahili/Kibantu, siku huanza saa kumi na mbili asubuhi. Kwa hivyo, saa moja ya asubuhi inakuwa ndiyo saa ya kwanza(1) ya siku.
Mfano:
- 5:00 asubuhi - saa tano kamili asubuhi
- 9:15 usiku - saa tisa na robo usiku.
- 11:30 jioni - saa kumi na moja unusu jioni
- 2:45 alasiri - saa tatu kasorobo au saa mbili na dakika arubaini na tano alasiri
- 10:23 alfajiri - saa kumi na dakika ishirini na tatu alfajiri
Mfumo wa Kimataifa/Kiingereza
Huu ndio mfumo unaokubalika kirasmi katika mataifa na lugha mbalimbali. Kulingana na mfumo huu, siku huanza saa sita za usiku. Hivyo basi, saa saba ya usiku inakuwa saa ya kwanza(1) ya siku.
Mfano:
- 6:00 macheo - saa kumi na mbili asubuhi kamili macheo
- 12:15 adhuhuri - saa sita na robo adhuhuri.
- 3:30 alasiri - saa tisa na nusu alasiri
- 6:45 jioni - saa moja kasorobo au saa kumi na mbili na dakika arubaini na tano jioni
- 11:08 usiku - saa tano na dakika nane usiku