Vitate, Vitawe na Visawe

Baadhi ya maneno ya Kiswahili yanaweza kuwa na maana sawa, maana zaidi ya moja au matamshi yanayotatiza. Vikundi hivi vitatu ni:
 1. Vitate - maneno yanayotatiza kimatamshi. ⇒ '' Vitate hutatiza kimatamshi
 2. Vitawe - maneno yenye maana zaidi ya moja. ⇒ Vitawe hugawanywa kwa matawi au maana zaidi
 3. Visawe - maneno tofauti yenye maana sawa. ⇒ Visawe huwa na maanasawa

Vitate

Maneno yanayotatiza kimatamshi.
 1. ndoa na doa :
  1. ndoa ⇒ kuungana kwa watu wawili na kuishi pamoja kama mume na mke
  2. doa ⇒ alama ya uchafu, kasoro au dosari
  • baba na papa :
  1. baba ⇒ mzazi wa kiume
  2. papa ⇒ mnyama wa baharini
  • fua na vua :
  1. fua ⇒ osha nguo, tengeneza vyuma
  2. vua ⇒ shika samaki kutoka majini; toa nguo
  • faa na vaa :
  1. faa ⇒ inayostahili, inayopaswa
  2. vaa ⇒ weka nguo juu ya mwili
  • ngoma na goma :
  1. ngoma ⇒ ala ya muziki itoayo sauti inapopigwa
  2. goma ⇒ acha kufanya kazi
  • shinda na shida :
  1. shinda ⇒ ongoza katika makabiliano, mashindano
  2. shida ⇒ taabu au matatizo
  • shindano na sindano :
  1. shindano ⇒ makabiliano baina ya watu wawili au zaidi ili kutambua atakayeongoza
  2. sindano ⇒ kifaa kinachotumika kushonea vitu
  • pinga na piga :
  1. pinga ⇒ kutokubaliana na jambo fulani
  2. piga ⇒ kugonga au kuchapa
  • fahali na fahari :
  1. fahali ⇒ ng'ombe wa kiume. pia ndume
  2. fahari ⇒ kujivunia, furaha
  • haba na hapa :
  1. haba ⇒ kisichokuwa kingi
  2. hapa ⇒ mahali karibu
  1. }

  Vitawe

  Mano yenye maana zaidi ya moja
  1. paa :
   1. kwea (enda juu)
   2. mnyama wa porini anayefanana na mbuzi
   3. sehemu ya juu ya nyumba
   • shinda :
   1. kaa au ishi mahali/wakati fulani
   2. ongoza katika shindano
   3. tupu
   • kaa :
   1. sehemu yenye moto ya kuni
   2. mnyama wa majini
   3. keti chini
   4. kuwa mahali fulani kwa muda
   • mbuzi :
   1. mnyama anayefugwa kama ng'ombe
   2. chombo cha kukunia nazi
   • mlango :
   1. ukoo au watu wenye asili smoja
   2. sehemu ya kuingia kwenye nyumba
   3. kitu kinachotumika kifunga nyumba
   • fua :
   1. unda vyombo/vifaa mbalimbali kwa kupiga chuma
   2. osha nguo
   • vua :
   1. toa nguo kutoka mwilini
   2. toa samaki kwenye maji
   • kiboko :
   1. mnyama mkubwa wa baharini
   2. silaha inayotumika kwa kuchapa au kupiga
   • tembo :
   1. aina ya ndovu
   2. aina ya pombe
   1. }

   Visawe

   Maneno tofauti yenye maana sawa.
   1. msichana au banati : ⇒ kijana wa jinsia ya kike
   2. mvulana au ghulamu : ⇒ kijana wa jinsia ya kiume
   3. huzuni au majonzi : ⇒ hali ya kilio na huruma
   4. mazishi au matanga : ⇒ shughuli za kumzika marehemu
   5. wakati au mwia : ⇒ wakati au muda
   6. mtu au mja : ⇒ mnyama atembeaye kwa miguu miwili mwenye uwezo wa kuongea na kufikiri kimantiki
   7. barua au waraka : ⇒ kartasi inayoandikwa na kutumwa ili kuwasilisha ujumbe fulani
   8. siri au faragha : ⇒ jambo lisilopaswa kujulikana na mtu mwengine
   9. macho au maninga : ⇒ sehemu za mwili zinazotumika kuangalia na kuona
   10. mwangaza au nuru : ⇒ miyale inayowezesha watu kuona vitu
   11. Mungu au Mola au Rabana au Jalali au Rabuka : ⇒ Majina ya Mwenyezi Mungu