Aina za Vihusishi
Vihusishi vya Mahali
mbele ya, nyuma ya | Kuna mzoga nyuma ya jengo hilo. |
chini ya, juu ya | Joto lilipozidi, watoto waliketi chini ya mti ule. |
kando ya | Kando ya mito ya Babeli ndipo tulipoketi. |
karibu na, mbali na | Fisi aliambiwa asile mifupa karibu na mtoto yule. |
Vihusishi vya Wakati
kabla ya | Ni vizuri kusali kabla ya kula chakula. |
baada ya | Watoto safi hupiga meno mswaki baada ya kila mlo. |