Alama ya Kikomo au Kituo Kikuu(.) |
1. | Kuonyesha mwisho wa sentensi. |
- Huu ndio mwisho wa sentensi hii.
- Kioo kimevunjika.
|
2. | Katika kufupisha maneno |
- U.N.O, K.B.C, Y.C.S
- Dkt. Maktaba, Bw. Msumari
|
3. | Kuonyesha Saa |
- Misa ilianza saa 4.30 za asubuhi.
- Hivi sasa ni saa 10.20.
|
4. | Katika hesabu kuonyesha sehemu isiyo nzima |
- Ukigawa tatu mara mbili, utapata 1.5
- Mtoto huyo ana uzani wa kilo 8.27
|
5. | Kuonyesha senti katika pesa |
- Bei yake ni shilingi 12.50.
- Karo ya shule mwaka huu ni 80,000.00
|
Alama ya Kituo, Kipumuo au Koma (,) |
1. | Kuorodhesha vitu zaidi ya mbili |
- Nimenunua simu, saa, redio na viatu.
- Kina mama waliimba, wakapiga ngoma na kunegua viuno vyao.
|
2. | Kugawanya mawazo katika sentensi. |
- Baada ya sala za jioni, Mzee Makosa alitoka nje na kuwasha sigara yake.
- Nilipomwuliza kama alimjua binti yule, aliniangalia tu na kucheka
- Ingawa kitabu hiki ni kizito, sina budi kukibeba.
|
3. | Kutoa maelezo zaidi. |
- Shabiba, mmojawapo ya wanawake wajawazito, amejifungua mtoto wa kike.
- Shati hili, ingawa nalichukia, nitalivalia tu.
|
4. | Katika tarakimu, kugawa elfu. |
- Shilingi 209, 408, 000 ziliporwa na serikali.
- Dawa hiyo iliua takribani mbu 61, 247.
|
Alama ya Kinukuu (' na ") |
1. | Kunukuu usemi halisi |
- "Ukitaka kufua dafu," mama akamwambia mwanawe, "lazima utie bidii."
- Alimtazama kisha akamwuliza, "Unadhani nimechanganyikiwa kama wewe?"
|
2. | Kunukuu kichwa cha kazi ya sanaa k.v kitabu, wimbo, kipindi n.k |
- Saumu na Neema ni wahusika katika riwaya "Hamu ya Sumu Tamu".
- Rose Muhando ndiye aliyeimba "Mteule Uwe Macho".
|
3. | Kuonyesha maneno yasiyo ya Kiswahili unapochanganya ndimi katika sentensi |
- Huyu ndiye mchezaji "number one"
- Amesema "keyboard" ya "computer" yake haifanyi kazi..
|
4. | Kuonyesha maneno yanayowakilisha maana tofauti na maana yake ya kawaida au kinaya. |
- Lesi alipoenda kwenye 'maktaba' alipata mimba.
- Rais wetu 'mtukufu' amewatisha mawaziri wake.
- Moto ulioteketeza shule hiyo ulitokana na kusudi la wanafunzi la 'kumshtua' mwalimu wao.
|
5. | Kuonyesha herufi iliyoachwa nje au kufupisha maneno katika ushairi hasa kwa kusudi la kutosheleza idadi ya mizani |
- 'takufuata popote wendapo,
- 'liapo ya mgambo, lazima kuna jambo
|
6. | Katika maendelezo ya sauti ya ung'on'g'o (ng') |
- Ng'ombe wa Ng'ang'a wanang'ang'ania nini?
- King'ang'i anapenda kunung'unika ovyo ovyo.
|
Alama ya Kiulizi (?) |
1. | Kuulizia swali |
- Je, utamtembelea lini?
- Ariana anaishi wapi?
|
2. | Kuonyesha pengo lililoachwa wazi |
- Ndama ni mwana wa ng'ombe ilhali _?_ ni mtoto wa mbuzi.
- ? mpokee mke wako, ?, siku ya leo umepata jiko.
|
Alama ya Hisi (!) |
1. | Kuonyesha hisia kama vile hasira, mshangao, furaha n.k |
- Lo! Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni.
- Pepo nyeusi! Shindwa! Chomeka! Kwenda kuzimu!
|
2. | Kuigiza Tanakali za Sauti |
- Amejikwaa sasa ameanguka pu!
- Moyo ulidunda ndu! ndu!
|
Alama ya Nukta-Mbili au Koloni (:) |
1. | Kutanguliza orodha |
- Harusi hiyo ilihudhuriwa na watu wa wengi: wake kwa waume; wadogo kwa wakubwa; wazee kwa vijana.
- Kuna aina kadhaa za vivumishi: vivumishi vya sifa, vivumishi vya idadi, vivumishi viwakilishi na kadhalika
|
2. | Kuelezea sababu au kuonyesha matokeo ya kitu. |
- Saumu alipoingia chumbani alipigwa na butwaa: mamake alikuwa amekufa.
- Baba alinipatia zawadi nzuri sana: nilirukaruka kwa furaha.
|
3. | Kuonyesha saa |
- Wimbo huo unachukua dakika 4:45.
- Aliingia saa 5:15
|
4. | Kunukuu ukurasa wa Bibilia |
- Padre alisoma Luka 2:1-6
- Katika kitabu cha Mwanzo 5: 2-7, Bibilia inasema...
|
5. | Kuonyesha maneno ya msemaji katika tamthilia au mchezo wa kuigiza |
- Mzee Mwanyati: Unafikiria mimi ni nyanyako?
- Kadogo: (akitetemeka) Tafadhali naomba unisamehe.
|
6. | Kuonyesha mada katika barua au kumbukumbu za mkutano |
- KUH: Ombi Lako la Kujiuzulu.
- RE: Barua ya tarehe 3/2/1999.KUM: 2/321/2000 Mbinu Mpya za Kunyamazisha Raia
|
7. | Katika kumbukumbu za mkutano |
- KUM 2/321/2000: Mbinu mpya za kunyamazisha raia.
- Ajenda 2: Kusomwa kwa kumbukumbu za mkutano uliotangulia.
|
Alama ya Nukta-Kituo au Semi Koloni (;) |
1. | Kuorodhesha vitu hasa vinapokuwa na zaidi ya neno moja |

- Wakati wa likizo tulitembelea sehemu kadhaa: Mombasa, Kenya; Dodoma, Tanzania; Kampala, Uganda na tukamalizia hapa Nairobi, Kenya.
|
2. | Kuunganisha vishazi huru viwili au kuonyesha mawazo mawili. |
- Tuliwasili darasani tukiwa tumechelewa; mwalimu alitukaribisha kwa kiboko.
- Usiwe na wasiwasi; nitakuwa pamoja nawe siku zote.
|
Alama ya Kistari Kifupi (-) |
1. | Kuunganisha maneno mawili |
- Mbwa-koko aliuma mwana-haramu.
- Nawatuma kama wana-kondoo miongoni mwa mbwa-mwitu.
|
2. | Kuonyesha hadi, au mpaka |
- Bei imepanda kutoka shilingi 20 - 30
- Tutasoma kitabu cha Matendo 2: 3 - 7
|
3. | Kama alama ya kupunguza au kutoa katika Hesabu |
- 9 - 7 = 2
- 4 - 5 = -1
|
4. | Kuonyesha neno ambalo halijakamilika litaendelezwa katika msitari ufuatao |
- Ukitaka twende kwetu nyumbani nitaku-
peleka ukamwone mamangu. - Kuna migumo kumi na mitatu kati-
ka Bustani la Kuzimu.
|
5. | Kuonyesha tarehe |
- Watu wengi walikufa tarehe 07-08-1998.
- Marehemu alikufa tarehe 06-06-2006
|
Alama ya Kistari Kirefu (‒) |
1. | Kutoa maelezo zaidi |
- Nilipokutana na Zakido ‒ ambaye aliripotiwa kupotea miaka miwili iliyopita ‒ nilimsalimia lakini hakunitambua.
- Hatimaye nimeshinda ‒ baada ya kujaribu kwa masaa matatu.
|
2. | Kuorodhesha hoja au vitu |
- Umuhumu wa fasihi simulizi:
‒ kuburudisha ‒ kuelimisha ‒ kuunganisha jamii
|
Alama ya Mabano au Parandesi () |
1. | Kutoa maelezo zaidi |
- Z. Anto (aliyeimba Binti Kiziwi) ametoa wimbo mpya.
- Shangazi yangu (ambaye ni naibu wa waziri) amenitumia zawadi.
|
2. | Kutoa neno jingine lenye maana sawa |
- Dhamira (nia) ya mshairi huyu ni kutushauri tusikimbilie maisha.
- Mabanati (wasichana) hao hutembea uchi jijini usiku wa manane.
|
Alama ya Kinyota (*) |
1. | Kuonyesha neno ambalo litaelezewa zaidi chini ya ukrasa(foot note) |
- Alipopata nafasi ya kuingia shule ya upili ya Starehe*, mwanafunzi huyo alijawa na furaha tele.
*Starehe ni mojawapo ya shule zinazofanya vizuri zaidi barani Afrika.
|
2. | Kuficha herufi/silabi katika neno ili kupunguza ukali wa maneno yasiyo na nidhamu. |
- Rais aliwaita wananchi m**i ya kuku.
- Aidha, alisema kwamba nyote ni wapu***vu.
|
Alama ya Mlazo (/) |
1. | Kuonyesha 'au' |
- Mkutano huo utahutubiwa na Rais/Waziri Mkuu.
- Wazungumzaji wengi wa Kiswahili wanatoka Kenyz/Tanzania.
|
2. | Kuonyesha neno au fungu la maneno lenye maana sawa. |
- Sheila amepewa cheo cha katibu/mwandishi.
- Hawa ndio wanaotapatapa ovyo/wasio na mbele wala nyuma.
|
3. | Katika hesabu kuonyesha kugawanya au akisami. |
- 5/7 ya siku za juma ni siku za kazi.
- 12 / 6 = 2
|
4. | Katika tarehe |
- Shule zilifunguliwa tarehe 08/01/2012
- Kamati hiyo ilikubaliana kwamba, Mwokozi alizaliwa tarehe 25/12
|
Alama ya HERUFI KUBWA |
1. | Kuanzisha sentensi' |
- Fisi hula mizoga.
- Huu ndio mwanzo wa sentensi hii.
|
2. | Kuonyesha Nomino za Kipekee |
- Bi Rangile anatoka Vikwazoni.
- Nchi ya Tanzania imebarikiwa na Mlima Kilimanjaro unaowavutia wageni kutoka Ulaya.
|
3. | Kuonyesha Kichwa au Mada |
- ALAMA ZA UAKIFISHAJI
- UFAHAMU
- Njia Tano za Kuua Mbu
|
4. | Kuonyesha maneno yaliyofupishwa |
- UKIMWI ni Ukosefu wa Kinga Mwilini.
- TUKI ni Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.