Riwaya

Riwaya ni kazi ya fasihi andishi ambayo huwa ndefu na aghalabu riwaya moja hujaza kitabu kizima. Riwaya huwa na wahusika wengi na huangazia mawazo kadhaa. Aidha, riwaya hufanyika katika mazingira mbalimbali na aghalabu huchukua muda mrefu ikilinganishwa na hadithi fupi.

Aina za Riwaya

Kunazo aina kadhaa za Riwaya katika Fasihi Andishi:
  • Riwaya sahili - visa vyake husimuliwa moja kwa moja na huwa rahisi kueleweka
  • Riwaya changamano - hii ni riwaya ambayo huhitaji kusomwa kwa makini ili kueleweka.
  • Aghalabu huwa na maudhui mengi na wahusika wengi ambao wanachangia katika tatizo kuu katika riwaya hiyo. Hujengwa kwa taharuki ili kuwavutia hadhira kutazamia jinsi tatizo kuu litakavyotatuliwa. Hutumia mbinu za taharuki na visengere nyuma/mbele.
  • Riwaya ya kibarua - hutumia muundo wa barua kuwasilisha ujumbe wake.
  • Riwaya kiambo - huhusisha maswala ya kawaida katika jamii

Mifano ya Riwaya

  • Utengano
  • Siku Njema
  • Mwisho wa Kosa
  • Kiu