Aina za Mashairi
Mashairi yanaweza kugawanywa katika aina mbalimbali kulingana na idadi ya mishororo katika kila ubeti.
Tanbihi: Aina za Mashairi ni tofauti na Bahari za Ushairi. Aina za mashairi huzingatia idadi ya mishororo katika kila ubeti ilhali Bahari za Shairi hutegemea na muundo wa shairi kwa kuzingatia vina, mizani, vipande na mpangilio wa maneno.
Shairi moja haliwezi kuwa la aina mbili (k.v tarbia na takhmisa) lakini shairi linaweza kuwa katika bahari zaidi ya moja.
Zifuatazo ni aina za mashairi kulingana na idadi ya mishororo katika kila ubeti
AINA | MISHORORO | |
Umoja/tathmina | 1 | Tathmina au Umoja ni shairi lenye mshororo mmoja katika kila ubeti. |
Tathnia | 2 | Tathnia ni shairi lenye mishororo miwili katika kila ubeti. |
Tathlitha | 3 | Tathlitha ni shairi lenye mishororo mitatu katika kila ubeti. |
Tarbia | 4 | Tarbia ni shairi lenye mishororo minne katika kila ubeti. Mashairi mengi ni ya aina ya tarbia. |
Takhmisa | 5 | Takhmisa ni shairi lenye mishororo mitano katika kila ubeti. |
Tasdisa | 6 | Tasdisa ni shairi lenye mishororo sita katika kila ubeti. |
Usaba | 7 | Usaba ni shairi lenye mishororo saba katika kila ubeti. |
Ukumi | 10 | Ukumi ni shairi lenye mishororo kumi katika kila ubeti. |