Insha za Mazungumzo au Majadiliano

Hii ni insha ya mazungumzo baina ya watu wawili au zaidi. Ni lazima wahusika katika mazungumzo wajitokeze vizuri na sifa zao zitambulike. Hatutarajii watu katika mazungumzo wawe na fikira moja na usawa katika mapendekezo yao. Ukinzani au tofauti ya uteuzi wa maneno kati ya usemi wa mzungumzaji mmoja na mwengine ni lazima ijitokeze.

Mazungumzo yanaweza kuwa ya kutafuta suluhisho baina ya pande mbili zinazozozana kama vile mama na bintiye; kupanga jambo fulani, n.k

Insha ya Mazungumzo huandikwa katika usemi halisia, huku wasemaji wakionyeshwa kama vile mchezo wa kuigiza.

Vitendo vya wahusika huonyeshwa kwa mabano

Mfano wa Insha ya Mazungumzo

Mazungumzo baina ya Mwalimu Mkuu, Mwanafunzi na Babake kuhusu nidhamu ya mwanafunzi huyo.

Mwalimu: Bwana Juma, nimekuita umchukue mtoto wako ukamsomeshe katika shule nyingine kwa maana amtushinda sisi.
Mzazi: Ikiwa amewashinda na ninyi ndio mlio na kiboko, si ataniua mimi! Hata mimi simtaki kwa maana simwezi. Hawezi kuja kwangu
Juma: Nimesema sitaki kusoma! Nimechosha na mtindo huu…
Mzazi: (akikunja shati)... ...