Msamiati wa Walemavu

Haya ni majina yanayopewa watu waliolemaa sehemu mbalimbali za mwili. Kiungo cha mwili husemekana kwamba kimelemaa pale ambapo hakiwezi kufanya kazi yake vizuri kama inavyohitajika. Kwa mfano, macho yasiyoweza kuona chochote, miguu isiyoweza kutembea n.k.

Mifano

  1. bubu:
    mtu asiyeweza kuongea
  2. chongo:
    mtu mwenye jicho moja
  3. gumba:
    mwenye nundu mgongoni
  4. kibogoyo:
    mtu asiye na meno
  5. kigugumizi:
    mtu mwenye shida ya kutamka maneno
  6. kilema:
    mtu aliyelemaa miguu na mikono - asiyeweza kutembea wala kushika chochote
  7. kipofu:
    mtu asiyeweza kuona.
  8. kiwete:
    mtu aliyelemaa miguu. asiyeweza kutembea
  9. kiziwi:
    mtu asiyeweza kusikia.
  10. matege:
    mwenye miguu iliyopinda
  11. punguani:
    mtu asiyekuwa na akili timamu