Uainishaji wa Neno
Kuainisha ni kugawa neno katika viambishi vyake mbalimbali. Tunapoainisha neno, tunaonyesha mzizi wa neno pamoja na viambishi vyote vilivyofungamanishwa kuunda neno hilo.
Angalia:
Mifano:
Ainisha maneno yafuatayo:
-
nitasoma → ni-ta-som-a
{
ni → kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya kwanza umoja
}
ta → kiambishi kiwakilishi cha wakati ujao
som → shina la kitenzi cha kusoma
a → kiishio -
walipozipata → wa-li-po-zi-pat-a
{
wa → kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya pili wingi
}
li → kiambishi kiwakilishi cha wakati uliopita
po → kiambishi kiwakilishi cha po ya wakati au cha ngeli ya mahali PO
zi → kiambishi kiwakilishi cha kitendwa, ngeli ya I-ZI wingi
pat → shina la kitenzi cha kupata
a → kiishio -
vimeshikamana → vi-me-shik-aman-a
{
vi → kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya KI-VI wingi
}
me → kiambishi kiwakilishi cha wakati uliopita muda mfupi
shik → shina la kitenzi cha kupata
aman→ kiambishi kiwakilishi cha kauli ya kutendamana
a → kiishio -
mnayemkimbilia → m-na-ye-m-kimbi-li-a
{
m → kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya pili wingi
}
na → kiambishi kiwakilishi cha wakati uliopo
ye → kiambishi kirejeshi cha nafsi ya tatu
m→ kiambishi kiwakilishi cha mtendewa, nafsi ya tatu umoja
kimbi → mzizi wa kitenzi cha kukimbia
li → kiambishi kiwakilishi cha kauli ya kutendea
a → kiishio -
yakimwagika → ya-ki-mwag-ik-a
{
ya → kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya YA-YA
}
ki → kiambishi kiwakilishi cha KI-ya masharti au au cha KI-ya kuendelea
mwag → mzizi wa neno mwaga
ik→ kiambishi kiwakilishi cha kauli ya kutendeka
a → kiishio -
hawakukushibisha → ha-wa-ku-ku-shib-ish-a
{
ha → kiambishi kiwakilishi cha kukanusha
}
wa → kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya tatu wingi
ku → kiambishi kiwakilishi cha kukanusha wakati uliopita
ku → kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya pili mtendewa
shib → mzizi wa kitenzi cha kushiba
ish→ kiambishi kiwakilishi cha kauli ya kutendesha
a → kiishio -
lililolililia → li-li-lo-li-li-li-a
{
li → kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya LI-YA umoja
}
li → kiambishi kiwakilishi cha wakati uliopita
lo → kiambishi kirejeshi cha ngeli ya LI-YA umoja
li→ kiambishi kiwakilishi cha mtendewa, ngeli ya LI-YA
li → shina la kitenzi cha kulia
li → kiambishi kiishio cha kauli ya kutendea
a → kiishio