Msamiati

Msamiati ni maneno yanayotumika katika lugha fulani. Hata hivyo, neno "msamiati" hutumika mara nyingi kumaanisha maneno mapya au maneno yasiyojulikana na watu wengi. Isitoshe, "msamiati" hutumika kufafanua maana ya maneno yanoyopatikana katika mukhtadha mbalimbali.

Kwa mfano, tunapoongea juu ya msamiati wa hospitalini, tunarejelea maneno yanayotumika sana katika mazingira hayo ya hospitalini, lakini hayatumiki kiasi hicho kwingineko.