Insha za Mdokezo

Hizi ni Insha za ubunifu ambazo mwanafunzi hupewa kifungu cha maneno kinachopaswa kujitokeza katika insha yake.

Baadhi ya insha za aina hii huwa zimetangulizwa na mwanafunzi hutakiwa akamilishe na nyinginezo huwa na kimalizio. Japo mwanafunzi ana uhuru wa kuiendeleza insha yake atakavyo, ni sharti ajifunge katika maudhui yanayojitokeza katika mdokezo aliopewa. Kwa hivyo, kabla ya mwanafunzi kuiendeleza insha yake, ni sharti atambue maudhui yaliyokusudiwa na mtahini.

Kwa mfano:

Endeleza insha ifuatayo na uifanye iwe ya kuvutia:
  1. Nikasikia sauti hiyo tena. Sikuamini masikio yangu. Moyo ukaanza kunienda mbio mbio. Mara upepo....
  2. Giza lilikuwa limechukua milki ya viumbe wote duniani. Nyota zilitoa mwanga hafifu na mwezi ulikuwa ushatua. Katika giza hilo la kaniki....

au

Andika insha inayoishia kwa dondoo hili...
  1. ... na kuniacha machozi yakinienda mbilimbili.
  2. ... Hadi wa leo, juhudi zangu za kusahau matukio ya siku hiyo hazifui dafu.