Sajili ya Ajali
Hii ni lugha inayotumiwa katika ambalo ajali imetokea. Wahusika wanaweza kuwa majeruhi, polisi, walioshuhudia au wananchi wengine n.k
Sifa za lugha inayopatikana katika sajili hii
- Msamiati wa kipekee unaohusiana na ajali kama vile majeruhi, hudumanya kwanza, damu, mkasa.
- Hutumia lugha ya kudadisi dadisi ili kubaini chanzo cha ajali.
- Huwa na masimulizi – walio na habari kuhusu kisa hicho hueleza waliyoshuhudia
- Kutokana na hali ya msukosuko, lugha hii haina utaratibu – watu huwa katika hali ya hofu, kwa juhudi za kuwaokoa majeruhi.
Mfano wa Sajili ya Ajali
Mwanakijiji 1: | Nimesikia twa! Kisha kishindo kikubwa sana (akihema hema) Nikaambia kuna mlipuko tukimbie. |
Mwanakijiji 2: | Lilio la muhimu ni kuyaokoa maisha ya majeruhi kwa kuwapa huduma ya kwanza. |
Mwanakijiji 1: | Tuondoeni miili ya waliofariki kwanza. |
Mwanakijiji 2: | hatuwezi kuishika miili iliyobanwa katika gari hadi polisi wafike. Na ndio hao wanaokuja! |
Mwanakijiji 1: | (akikimbia) Ndio hao! Acheni kuiba mafuta! Polisi wanakuja! |
Polisi: | Wakitawanya wananchi walioliparamia gari kuiba bidhaa mbali mbali.Liinueni hili gari! Wapi dereva? |
Dereva: | (ambaye amelala akihema kwa maumivu, damu ikichuruzika miguuni na mikononi) Nilisitishwa na ng'ombe waliokuwa wakivuka barabara. Nilijsribu kukwepa lakini usukani ukanishinda gari likapoteza mwelekeo… |
Abiria: | Alikuwa akiendesha gari kwa kasi sana. Tukampigia kelele apunguze mwendo lakini hakutusikia. Matunda yake… |
Mwanakijiji 2: | Niliona gari likibingiria mara kadhaa mpaka likaingia humu mtaroni, ndiyo tukakimbia kuwaokoa. |
Polisi: | Nyamazeni! Achieni polisi kazi iliyobaki. Ikiwa kuna yeyote anayejuana na waathiriwa aandamane nasi. |