Wasifu

Wasifu ni insha inayosimulia maisha ya mtu fulani tangu kuzaliwa kwake, elimu yake, kazi, ujuzi wake n.k. Anayeandika wasifu ni tofauti na anayezungumziwa katika wasifu huo.

Kuna aina tatu za wasifu:


Wasifu

Wasifu wa kawaida ni masimulizi ya maisha ya mtu fulani yanayosimuliwa na mtu mwengine. Kwa mfano, Wasifu Wa Siti Binti Saad ulioandikwa na Mwalimu Shaaban Robert.
Katika insha, mwanafunzi anawezaambiwa aandike wasifu wa:


Tawasifu

Katika tawasifu, mwandishi huwa anasimulia maisha yake mwenyewe. Hivyo basi, tawasifu huandikwa na kusimuliwa katika nafsi ya kwanza.
Katika insha, mwanafunzi anaweza ulizwa asimulie:

Kwa mfano, katika riwaya ya Siku Njema, mhusika Kongowea Mswahili anaandika tawasifu akisimulia maisha yake tangu kuzaliwa, maisha ya nyumbani, elimu yake, kazi alizozifanya, maono yake n.k


Wasifu-Kazi

Wasifu-kazi (Resume/Curriculum Vitae) ni stakabadhi inayotumiwa kuorodhesha mambo muhimu katika maisha ya mtu kama vile elimu, kazi, ujuzi n.k inayotumiwa sanasana katika kuomba kazi. Kinyume na wasifu na tawasifu ambazo hutumia lugha natharia (ya masimulizi), wasifu-kazi hutumia muundo fulani wa orodha na/au jedwali kuwasilisha mambo muhimu tu. Isitoshe, wasifu kazi huwa fupi - aghalabu ukrasa mmoja.

Tunapoorodhesha mambo fulani katika wasifu, tunaanza na yale ya hivi karibuni hadi yale ya kitambo. Kwa mfano, anza na shule uliyosomea mwisho, iliyokuwa imetangulia hiyo n.k hadi shule uliyoenda kwanza.

Muundo wa Wasifu-Kazi

Katika wasifu-kazi unahitajika kuonyesha:

 1. Jina lako
 2. Namna ya mawasiliano (simu, anwani, barua pepe)
 3. Elimu
  • orodhesha shule zote ulizozisomea kutoka shule uliyosomea mwisho hadi shule ile uliyoihudhuria kwanza.
  • katika kila shule, onyesha miaka uliyohudhuria k.m 1996-2000
  • onyesha shahada (degrees) na diploma ulizozipata
 4. Kazi
  • orodhesha kazi zote ulizozifanya kutoka kazi ya hivi karibuni hadi kazi ulizozifanya mwanzoni
  • onyesha cheo ulichokuwa nacho katika kazi hiyo na majukumu yake
  • onyesha kampuni au mahali ulipofanya kazi hiyo
  • onyesha miaka ambayo ulikuwa katika kazi hiyo
  • taja ujuzi au taaluma uliyoipata katika kazi hiyo
 5. Ujuzi / Taaluma - taja ujuzi maalumu ulionao, taaluma au talanta zozote zinazokufanya
 6. Mapato/Mafanikio/Tuzo - taja mafanikio yoyote au tuzo zozote ulizozipata katika maisha
 7. Mapendeleo - Nini kinakupendeza katika maisha? unapenda kutumiaje muda wako wa likizo usiokuwa wa kazi
 8. Maono ya Kazi - una maono gani katika kufanya kazi? ungependa kufanya nini?

Angalia hapa baadaye kwa mfano wa wasifu-kazi.