Kinyume

Maneno ya kinyume ni maneno yenye maana inayopingana. Inafaa ikumbukwe kwamba kuna tofauti kati ya kinyume na kukanusha. Kukanusha ni kukataa ujumbe wa sentensi bila kubadilisha maneno. Tunapokanusha, tunabadilisha viambishi pekee ili kupinga wazo la sentensi. Maneno ya kinyume huwa maneno mengine tofauti kabisa ambayo yanapingana kimaana bila kubadilisha maendelezo ya neno.

Aina za Kinyume

Kinyume cha Kawaida

Hisia, hali, dhana n.k

1. vita amani
2. furaha kilio
3. nuru giza
4. shibe njaa
5. mwanzo mwisho

Kinyume cha Sifa

Hizi ni sifa zinazopingana kimaana.

1. tamu chungu
2. kubwa dogo
3. nzuri mbaya
4. nyeupe nyeusi

Kinyume cha Jinsia (Uume - Uke)

Mara nyingine unaweza kuangalia kinyume kulingana na jinsia iliyotumika. Hapa unapata kinyume kwa kubadilisha maneno ya kike yawe ya kiume, au maneno ya kiume yawe ya kike.

1. baba mama
2. mumewe mkewe
3. mjomba shangazi
4. kaka dada
5. babu nyanya
6. mvulana msichana
7. ghulamu banati
8. shaibu ajuza

Kinyume cha Uhusiano

Hiki ni kinyume cha vitu au dhana mbili zinazohusiana.

1. mwalimu mwanafunzi
2. daktari mgonjwa
3. mzazi mwana
4. kiongozi mfuasi

Kinyume cha Vitenzi

Tunabadilisha vitenzi kwa kuweka vitenzi vingine vyenye maana inayokinzana ''

1. ongea nyamaza
2. penda chukia
3. sifu kashifu
4. simama keti
5. lia cheka
6. tabasamu nuna
7. enda kuja

Kinyume cha Kutendua

Vitenzi vinaweka katika kauli ya kutendua ili kuvikanusha.

1. fumba fumbua
2. ficha fichua
3. vaa vua
4. choma chomoa