Hisabati na Tarakimu
Msamiati wa hesabu/hisabati unaangazia: majina mbalimbali ya tarakimu/nambari; kuandika tarakimu kwa herufi.maneno; tarakimu za kiarabu; akisami (fractions) na asilimia (percentages).
Tumekuandalia:
- Nambari za Kimsingi (0-9) Kiswahili na Kiarabu
- Kumi na (11-19) Kiswahili na Kiarabu
- Makumi/Ukumi (10-90)
- Akisami (fractions)
- Mifano Kadhaa
NAMBARI ZA KIMSINGI
Haya ni majina ya tarakimu mbalimbali zinapoandikwa kwa herufi (badala ya nambari) yenye asili ya Kiswahili/Kibantu na pia yale yenye asili ya Kiarabu. Pia, tumeongezea majina ya makumi mbalimbali (10-90)
TARAKIMU | KISWAHILI | KIARABU |
0 | sufuri | sufuri |
1 | moja | wahed |
2 | mbili | thenini |
3 | tatu | thelatha |
4 | nne | aroba |
5 | tano | hamsa |
6 | sita | sita |
7 | saba | saba |
8 | nane | themania |
9 | tisa | tisa |
KUMI NA
Majina ya ya tarakimu kutoka (11-19) kwa Kiswahili na kwa Kiarabu.
10+ | KISWAHILI | KIARABU |
11 | kumi na moja | edatashara |
12 | kumi na mbili | thenashara |
13 | kumi na tatu | thelathashara |
14 | kumi na nne | arobatashara |
15 | kumi na tano | hamsatashara |
16 | kumi na sita | sitatashara |
17 | kumi na saba | sabatashara |
18 | kumi na nane | themantashara |
19 | kumi na tisa | tisatashara |
MAKUMI
Kuandika tarakimu mbalimbali katika hali ya ukumi. (11-99).
*10 | JINA | MFANO | ||
# | KISWAHILI | KIARABU | ||
10 | kumi | 12 | kumi na mbili | thenashara |
20 | ishirini | 27 | ishirini na saba | saba wa ishirini |
30 | thelathini | 32 | thelathini na mbili | thenini wa thelathini |
40 | arobaini | 42 | arobaini na mbili | thenini wa arobaini |
50 | hamsini | 52 | hamsini na mbili | thenini wa hamsini |
60 | sitini | 61 | sitini na moja | wahed wa sitini |
70 | sabini | 76 | sabini na sita | sita wa sabini |
80 | themanini | 89 | themanini na tisa | tisa wa themanini |
90 | tisini | 93 | tisini na tatu | thelatha wa tisini |
AKISAMI
Akisami hutumiwa kuonyesha sehemu ya kitu kizima. Kwa mfano, ukigawa kilo moja kwa visehemu vinne vinavyotoshana, kila kisehemu kitakuwa na uzani wa robo kilo ( sehemu ya nne au moja kwa nne ) ya kilo.
1/# | JINA | MFANO | ||
1/2 | nusu | 1/2 | nusu | moja kwa mbili |
1/3 | thuluthi | 2/3 | thuluthi mbili | mbili kwa tatu |
1/4 | robo | 2/4 | robo mbili | mbili kwa nne |
1/5 | humusi | 3/5 | humusi tatu | tatu kwa tano |
1/6 | sudusi | 4/6 | sudusi nne | nne kwa sita |
1/7 | subui | 6/7 | subui sita | sita kwa saba |
1/8 | thumuni | 7/8 | thumuni saba | saba kwa nane |
1/9 | tusui | 3/9 | tusui tatu | tatu kwa tisa |
1/10 | ushuri | 6/10 | ushuri sita | sita kwa kumi |
1/100 | asilimia | 72/100 | asilimia sabini na mbili | sabini na mbili kwa mia moja |
MIFANO ZAIDI
Andika nambari zifuatazo kwa maneno/herufi:
3 - tatu952 - mia tisa hamsini na mbili680 - mia sita themanini4521903 - milioni nne, na mia tano ishirini na moja elfu, na mia tisa na tatu556100016 - mia tano hamsini na sita milioni, na mia moja elfu, na kumi na sita
Andika tarakimu zifuatazo kwa nambari
- sufuri -
0 - mia tatu ishirini na mbili -
322 - sabini na tatu elfu, na mia nane hamsini na tano -
73855 - mia tano sabini na nane elfu, na mia tatu hamsini na tisa -
578359 - mia sita tisini na sita milioni, na mia tisa tisini na nane elfu, na mia saba ishirini na tatu -
696998723
Andika akisami zifuatazo kwa maneno
240/295 - mia mbili arobaini kwa mia mbili tisini na tano41/45 - arobaini na moja kwa arobaini na tano26/51 - ishirini na sita kwa hamsini na moja59/74 - hamsini na tisa kwa sabini na nne1/3 - thuluthi