Sajili ya Mtaani

Lugha ya mitaani ni lugha inayozungumzwa na vijana mtaani.

Sifa za Lugha ya Mtaani

  1. Ni lugha legevu isiyozingatia kanuni za kisarufi
  2. Huchanganya ndimi
  3. Hutumia misimu kwa wingi
  4. Hukosa mada maalum

Mfano wa Sajili ya Mtaani

Chali: Hey, niaje msupaa?
Katosha: Poa. So, mathee yako alikushow naweza kuja?
Chali: Ha! Masa hana noma. Si unajua nita...
Katosha: Chali! Unataka aniletee problem?
Chali: Mimi ni boy wa maplans. Ngoja nifikirie venye tutamshow
Katosha: Na by the way, kwani umejipaka mafuta ya manzi. Ama ulikuwa na msichana mgani?
Chali: Oh! Niliscoop mafuta ya Anita. Si unajua nataka kunukia hmmmm...
Katosha: Ok. So, umefikiria tumshow nini masa yako? Ama nikona idea poa.
Chali: Nishow hiyo plot, na by the way, nataka unisaidie kuhusu ile deal yangu na Kaunda. Ile ya siz yangu.
Katosha: Kwanza tutaplan na huyo siz yako, niwe ndiye nimekuja kuvisit. Mamako atakubali
Chali: Wow! Idea poa. Utakuwa umekuja kufanya homework. Halafu masa akiishia kwa bed. Homework tutaitupa mbali.
Katosha: So, utamshow Anita nakuja tufanye homework...