Sajili Katika Isimu Jamii

Sajili- ni mukhtadha/rejista mbalimbali au mitindo maalum ya lugha katika mazingira/hali mbalimbali.

Kuna sajili anuwai za matumizi ya lugha katika jamii. Hapa tutazingatia mifano michache ya sajili mbali mbali.Kila sajili huwa na sifa mbalimbali zinazoitofautisha sajili hiyo na nyinginezo. Ili kubaini sifa za lugha katika sajili fulani, ni muhimu kuzingatia baadhi ya maswali yafuatayo:
  • ni mazungumzo baina ya nani na nani?
  • kuna uhusiano gani baina ya wanaozungumza?
  • yanapatikana wapi?
  • yanatumika katika hali gani?
  • yana umuhimu ama lengo gani
  • ni istilahi zipi istilahi (maneno maalum) zinazopatikana katika mazingira hayo?
  • umaizi wa lugha baina ya wazungumzaji ni wa kiwango gani?
  • ni mtindo gani wa lugha unaotumika?