Virai na Vishazi
Sentensi huwa na vifungu mbalimbali. Baadhi ya vifungu hivi ni vishazi na virai.
Virai (phrase)
Kirai ni fungu la maneno lisilokuwa na kitenzi.PhraseKuna aina nne za virai:
Kirai Nomino:
Kirai Nomino ni fungu la maneno katika sentensi lenye nomino (Kikundi Nomino/Kiima)
- Redio na runinga hutumika kutupasha habari.
- Bintiye Mchungaji Boriti anapenda kuwasaidia watu.
- Miembe mirefu itakatwa.
Kirai Kiwakilishi
Kirai Kiwakilishi ni fungu la maneno linalowakilisha nomino katika sentensi
- Zenyewe zimekwishaharibika.
- Watakaovumilia hadi siku ya mwisho wataokolewa
- Yeye alijitumbukiza majini na kufariki papo
Kirai Kivumishi
Kirai Kivumishi ni fungu la maneno katika sentensi linalotupa habari zaidi kuhusu nomino.
- Matokeotuliyokuwa tukiyasubiri yametangazwa.
- Duka zenye bei nafuu zimefungwa.
- Msichana mrembo kama malaika ameolewa.
Kirai Kielezi
Kirai Kielezi ni fungu la maneno linaloelezea zaidi kuhusu kitenzi au kivumishi.
- Walevi wana mazoea ya kupayuka ovyo ovyo.
- Viumbe vyote vyenye uhai vinamshangilia kwa furaha milele na milele.
- Kwaya ya Chuo Kikuu cha Nairobi huimba kwa sauti za kimalaika
Vishazi (clause)
Kishazi ni sehemu ya sentensi yenye kitenzi. Kuna aina mbili za virai:
Kishazi Huru (Independent Clause)
Kishazi Huru huwa na maana kamili na kinaweza kujisimamia chenyewe kama sentensi.
- Amina ameanza kuimba baada ya kumaliza kusali.
- Watakaopatikana wakichekacheka ovyoovyo, watang'olewa meno.
- Nitakupatia nusu ya ufalme wangu, iwapo utanipigia magoti.
Kishazi Tegemezi (Dependent Clause)
Kisha Tegemezi huhitaji kuunganishwa na kishazi kingine ili kuleta maana iliyokusudiwa. Aghalabu huwa na kirejeshi k.v amba-, -enye n.k
- Amina ameanza kuimba baada ya kumaliza kusali.
- Watakaopatikana wakichekacheka ovyoovyo, watang'olewa meno.
- Nitakupatia nusu ya ufalme wangu, iwapo utanipigia magoti.