Haya ni majina ya malipo yanayotolewa kwa shughuli/haja mbalimbali.
Mifano
- ada:
malipo kwa mganga au hospitali
- fidia:
malipo ya mtu baada ya kumkosea mwengine au kumtia gharama/hasara
- karo:
malipo kwa ajili ya mafunzo (shuleni)
- kiingilio:
malipo yanayotozwa watu ili kushiriki katika jambo fulani
- kiinua mgongo:
malipo anayotoa mtu kama shukrani kwa jambo alilotendewa au analotaka kutendewa
- kodi:
malipo kwa kutumia nyumba au kiwanja. aghalabu hulipwa kila mwezi.
- marupurupu:
pesa za matumizi ya kila siku
- mtaji:
pesa ambazo mtu huhitaji ili kuanzisha biashara
- nauli:
malipo ya kusafiri
- riba:
pesa zaidi mtu anazopata kwa kuweka pesa kwenye banki kwa muda fulani au malipo zaidi mtu anayohitajika kulipa juu ya kiasi alichochukua kama mkopo.
- rushwa:
malipo yanayolipwa kinyume cha sheria ili kumfanya mtu akupendelee katika jambo fulani.
- ushuru:
malipo kwa serikali