Mifano ifuatayo itakuonyesha umoja na wingi wa sentensi katika ngeli mbalimbali.
Ngeli ya A-WA | ||
1. | Mtoto huyu ni mvivu sana. | Watoto hawa ni wavuvi sana. |
2. | Mwizi aliyeiba ng'ombe wa mzee mkongwe amekamatwa na mwananchi. | Wezi walioiba ng'ombe wa wazee wakongwe wamekamatwa na wananchi |
Ngeli ya KI-VI | ||
1. | Kitabu chako kiko juu ya kitanda | Vitabu vyenu viko juu ya vitanda |
2. | Chumba kile kidogo kimeangukia chungu | Vyumba vile vidogo vimeangukia vyungu. |
Ngeli ya LI-YA | ||
1. | Jani lile linaficha tunda kubwa ambalo limeiva | Majani yale yanaficha matunda makubwa ambayo yameiva. |
2. | Jiko lolote lenye kaa moto litolewe nje | Meko yoyote yenye makaa moto yatolewe nje. |
Ngeli ya U-I | ||
1. | Mtaa huo hauna mti wowote | Mitaa hiyo haina miti yoyote. |
2. | Huu ndio mto uletao maji katika mji wetu | Hii ndiyo mito iletayo maji katika mito yetu. |
Ngeli ya U-ZI | ||
1. | Ukuta mwingine umepigwa kwa upembe | Kuta nyingine zimevunjwa kwa pembe. |
2. | Ubao mrefu uliokuwa kwenye ua wetu ulikatwa kwa upanga mweusi | Ndefu ndefu zilizokuwa kwenye nyua zetu zilikatwa kwa panga nyeusi. |
Ngeli ya I-ZI | ||
1. | Nyumba iliyo karibu na barabara ile imefungwa | Nyumba zilizo karibu na barabara zile zimefungwa. |
2. | Ndoo yenye maji imewekwa juu ya mbao kubwa | Ndoo zenye maji zimewekwa juu ya mbao kubwa. |
Ngeli ya U-YA | ||
1. | Uyoga uliokuwa hapa umeoza. | Mayoga yaliyokuwa hapa yameoza. |
2. | Mhindi wa kuchoma umeibiwa. | Mahindi ya kuchoma yameibiwa. |
Ngeli ya YA-YA | ||
1. | Mafuta na maji hayawezi kuchanganyika | Mafuta na maji hayawezi kuchanganyika. |
2. | Damu ni nzito kuliko maji | Damu ni nzito kuliko maji. |
Ngeli ya I-I | ||
1. | Sukari imemwagika kwenye changarawe hii. | Sukari imemwagika kwenye changarawe hii. |
2. | Ugali ni tamu lakini mboga haina chumvi. | Ugali ni tamu lakini mboga haina chumvi. |
Ngeli ya U-U | ||
1. | Uji uliopikwa kwa unga wa wimbi ni mtamu kuliko ule wa mtama. | Uji uliopikwa kwa unga wa wimbi ni mtamu kuliko ule wa mtama. |
Ngeli ya PA-PA | ||
1. | Mahali ambapo palipandwa maua panapendeza sana | Mahali ambapo palipandwa maua panapendeza sana. |
Ngeli ya KU-KU | ||
1. | Huku niliko hakuvutii kama kwangu | Huku tuliko hakuvutii kama kwetu |
2. | Kukimbia huku kunachosha. | Kukimbia huku kunachosha. |
Ngeli ya MU-MU | ||
1. | Nyumbani humu mna giza totoro. | Nyumbani humu mna giza tororo |