Tamthilia

Tamthilia au tamthiliya ni sanaa ambayo huwasilisha mchezo wa kuigiza kwa njia ya maandishi. Majina ya wahusika huandikwa katika upande wa kushoto, kisha koloni, halafu hufuatiwa na maneno halisi yaliyotamkwa na mhusika huyo.

Aina za Tamthilia

Kunazo aina kadhaa za tamthilia katika fasihi andishi:

 1. Tamthilia Cheshi/Komedia - ni mchezo wa kuchekesha. Maudhui yake huundwa kwa lengo la kutumbuiza hadhira.
 2. Tamthilia Simanzi/Trejedia - ni mchezo uliojaa huzuni, mikasa, mikosi, visa vya kutisha na aghalabu baadhi ya wahusika wakuu hufa.
 3. Tamthilia Simanzi-Cheshi/Trejikomedia - ni mchezo wenye visa vya kuhuzunisha lakini pia unawasilisha kwa njia ya kuchekesha. Aghalabu wahusika hutumia kejeli kuchekesha hadhira ijapokuwa kuna shida fulani inayowakabili. Baadhi ya wahusika wakuu hukumbwa na mikasa.
  Mfano: Kifo Kisimani (na Kithaka Wa Mberia)
 4. Tamthilia Tatizo - ni mchezo wa kuigiza ambapo wahusika huwa na tatizo/shida kuu wanalotaka kulitatua. Tamthilia hii aghalabu hutumia mbinu ya taharuki ili kuwafanya hadhira wawe makini ili kuona jinsi tatizo hilo litakavyoishia.
 5. Tamthilia ya Domestiki Drama - ni mchezo unaoangazia maisha ya kawaida ya watu kama vile familia, urafiki, ndoa n.k
 6. Tamthilia ya Melodrama - ni mchezo ambao husisitiza sifa za wahusika kwa kuunda wahusika kuunda wahusika wenye sifa zilizopigiwa chuku na zisizobadilika. Tamthilia hizi huundwa kwa namna inayowafanya hadhira wawapende wahusika fulani na wawachukie wahusika wengine. Kwa mfano:
  • Shujaa ambaye hushinda kila mara
  • Wahusika wabaya ambao hubakia wabaya kutoka mwanzo hadi mwishi
  • Wahusika wazuri ambao hufanya vitendo vizuri kutoka mwanzo hadi mwisho
  • Wapenzi ambao hata wakitenganishwa bado watapendana
  • Aghalabu huishia kwa raha mustarehe

Mifano ya Tamthilia

 1. Kifo Kisimani
 2. Shamba la Wanyama
 3. Mstahiki Meya